RAKI BIG
JF-Expert Member
- Apr 26, 2020
- 394
- 456
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa Shule, makanisa, misikiti, vilabu, vilabu vya usiku, maeneo ya kufanyia mazoezi na saluni za urembo zitaendelea kufungwa ili kuepuka maambukizi ya virusi vya corona.
Museveni amesema kuwa si rahisi kwa maeneo hayo kufuata masharti ya kutochangamana. Rais Museveni pia amesema muda wa kuwa ndani ya nyumba utaendelea kuwa kuanzia saa moja usiku mpaka saa kumi na mbili kamili asubuhi kwa siku 21 zaidi.
Makanisa, vilabu vya pombe, vilabu vya usiku , maeneo ya kufanya mazoezi na sauna yataendelea kufungwa kwa siku 21, huku kufungua shule kwa wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani kukiwa kumeahirishwa wakisubiri kwa mwezi mmoja.
''Tumeamua kuahirisha kufunguliwa kwa shule kwa wanafunzi wanaotarajiwa kufanya mitihani kwa mwezi mmoja zaidi tukijiandaa zaidi na kutazama hali ilivyo''.Alisema
Usafiri wa umma unatarajiwa kurejeshwa Alhamisi ya wiki hii kwa masharti maalum.
BBC Swahili