Uganda: Ajali ya boti yaua watu 9, wengine hawajulikani walipo

miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
1,954
Points
2,000
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
1,954 2,000
Msemaji wa jeshi la polisi nchini Uganda Bw. Fred Enanga amesema, maiti mbili zimepatikana na watu kati ya 13 hadi 16 hawajulikani walipo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika Ziwa Albert, wilaya ya Hoima, magharibi mwa Uganda Jumapili jioni.

Bw. Enanga ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kuwa, ajali hiyo ilitokea mita chache kutoka Runga kwenye sehemu ya Ziwa inayotumika kwa pamoja na sehemu ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Watu wengine 32 waliokuwa katika boti hiyo walifanikiwa kuogelea na kufika pwani.

Msemaji huyo amesema, kazi ya uokoaji inaendelea leo, na polisi na jeshi la majini wamepelekwa kwenye eneo la tukio ili kufanya operesheni ya utafutaji na uokoaji.

=======

UPDATES: 20 May 2019

Hadi sasa waliofariki wamefikia 9.

26 Disemba 2016 Watu 30 Walifariki. Abiria wengi walikuwa wanasoka na mashabiki wao waliokuwa wakielekea katika mechi ya kirafiki ya kuadhimisha siku ya Krismasi.
 
B

Balacuda

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2013
Messages
1,185
Points
1,250
B

Balacuda

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2013
1,185 1,250
katika ajari za majini ni 1/100,000,000,000 chance ya kuwapata wasiojulikana walipo wakiwa hai
 

Forum statistics

Threads 1,304,890
Members 501,583
Posts 31,530,825
Top