Ugali wa moto, mboga ya moto, pilipili kali, Machozi blublublublu

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Yaani bado nacheka,

Niko kwenye foleni barabarani, amenifuata muuza icecreem (na baiskeli yake ya Azam, ananifahamu). Akaniuliza, "bro, mjengoni si tarehe 8 mwezi wa pili eh?"

nikamwabia ndiyo, akasema "hapo ccm walipo nakuambia bro, ugali wa moto mboga ya moto na pilipili kali. Yaani wanakula ndiyo lakini machozi machozi yanawamiminika blublublublu na makamasi juu. Wanatamani February isifife. Mi nasubiria tu bro, labda wazuie wabunge wa Chadema wasiingie bungeni."

nimefurahi jinsi huyu kijana alivyoweza kuwasilisha kwa upana kiasi hicho hali halisi ya siasa na uchumi wa nchi yetu kwa kutumia maneno machache hivyo. Huyu kijana hana uwezo wa kutumia internet wala kununua gazeti.

Lakini ana ufahamu kamili wa nini kinaendelea na matarajio yake kwa bunge na wabunge wa upinzani ni thabiti

je, wabunge wa Chadema watamfurahisha au kumkatisha matumaini huyu kijana? Matarajio makubwa namna hii na thabiti ni makubwa mno kwa wabunge wa Chadema kutekeleza?
 
hao vijana wanaojishughulisha na biashara ndogondogo wanatambua ubovu wa CCM na wana uchungu nayo sana,tatizo lipo kwa lile kundi kubwa la vijana wa vijiweni wasiojua hata tofauti ya chama na serikali
 
je, wabunge wa Chadema watamfurahisha au kumkatisha matumaini huyu kijana? Matarajio makubwa namna hii na thabiti ni makubwa mno kwa wabunge wa Chadema kutekeleza?

Hebu acheni kuwapa mzigo wabunge wetu, waelimisheni hao wanaodhani wabunge wa CDM wanao uwezo wa kubadili kitu.
 
Hebu acheni kuwapa mzigo wabunge wetu, waelimisheni hao wanaodhani wabunge wa CDM wanao uwezo wa kubadili kitu.

Aliyekwambia hawawezi kubadilisha kitu ni nani?Kitendo cha kuwatoa mafisadi jasho tu na kuwanyima usingizi ni mabadiliko tosha maana ndiyo yatakayowafanya waogope kuumiza wananchi zaidi!
 
Gurudumu, kabla ya kuukabidhi huo mzigo kwa wabunge wa CDM huyo kijana ameukabidhi kwako. Nashukuru umetimiliza alichokitegemea kwako. Kwanza anajua kwamba wewe unajua. Ndio maana akataka confirmation kwako. Pili amekuonyesha kwamba anajua kinachomsumbua na amekushirikisha. Tatu umemsaidia kufikisha ujumbe wake. Na umefika.

Watanzania wameamka na wanatambua haki zao na watazipigania. Safari imeanza ya ukombozi. Tutafika!
 
hao vijana wanaojishughulisha na biashara ndogondogo wanatambua ubovu wa CCM na wana uchungu nayo sana,tatizo lipo kwa lile kundi kubwa la vijana wa vijiweni wasiojua hata tofauti ya chama na serikali

Hao wa vijiweni ni jeshila la dharura, kwenye maandamano watakuwa mstari wa mbele
 
Gurudumu, kabla ya kuukabidhi huo mzigo kwa wabunge wa CDM huyo kijana ameukabidhi kwako. Nashukuru umetimiliza alichokitegemea kwako. Kwanza anajua kwamba wewe unajua. Ndio maana akataka confirmation kwako. Pili amekuonyesha kwamba anajua kinachomsumbua na amekushirikisha. Tatu umemsaidia kufikisha ujumbe wake. Na umefika.

Watanzania wameamka na wanatambua haki zao na watazipigania. Safari imeanza ya ukombozi. Tutafika!

Niseme ukweli, sikujua kama mwananchi wa ngazi yake atakuwa anajua wajibu wa bunge na mbunge kwa kiwango hicho. Kwamba anahesabu tarehe! Pili, mara nyingi sisi hushabikia sauti na kauli za viongozi wa kisisa, nadra tunatafuta kujua mwananchi wa kawaida anafikiri nini na anasema nini. Tunajiona kwamba sisi tunajua kuliko wananchi wa kawaida, so the media keeps recycling same "used" ideas from same few individuals
 
hao vijana wanaojishughulisha na biashara ndogondogo wanatambua ubovu wa CCM na wana uchungu nayo sana,tatizo lipo kwa lile kundi kubwa la vijana wa vijiweni wasiojua hata tofauti ya chama na serikali
inabidi waelimishwe
 
Wacha vyote viwe vya moto!

Yaani falsafa ya huyo kijana nimeivulia kofia, nikatamani kama wananchi wa ngazi hiyowangekuwa na uwezo wa kufika Hapa JF na kupakua fikra na feelings zao. JF ingechimbika!
 
CCM itabakia kuchakachua vijijini tu pale wanapo wa wadanganya kwa kanga na kofia, Mtu wa mjini ni yule mwenye maslahi yake binafsi ataitetea kula yake.
CDM matumaini ya watanzania mmei beba. Tume waamini na tuna mategemeo makubwa. Mliyo yafanya ni makubwa mlipokuwa na idadi ndogo.
Tunategemea mashambulizi yatakuwa makali zaidi.
 
Back
Top Bottom