Namshauri Rais Samia awachukulie hatua kali sana waliofuja pesa za umma ili kuwafuta machozi wavuja jasho wa Taifa hili

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,308
9,737
Ndugu zangu watanzania,

Kitendo Cha ripoti ya CAG kuonyesha ufujaji wa mabillioni ya pesa zao katika baadhi ya maeneo kimewaumiza Sana watanzania,kimewatoa machozi ,kimewapiga ganzi mioyo Yao,kimewapa ubaridi mioyo Yao,kimewasikitisha,kimewahuzunisha Sana,kimewapa maumivu mioyo Yao,kimewafanya wakae chini kwa kukosa nguvu.

Hii ni kutokana na uchungu walio nao katika fedha zao, watanzania wanajuwa kuwa hizo ni fedha zao, ni michango yao ni Kodi zao, ni tozo zao, ni ushuru wao, ni fedha wanazochanga watanzania kwa ujumla wao bila kujali ni yatima au mgonjwa au mjane au mzee ,wote wanalipa Kodi kupitia kununua bidhàa.

Hata Marehemu nao wanapokuwa wamefariki na kuaga Dunia na kutangulia mbele za haki nao kabla ya kuzikwa wanalipa Kodi kupitia ndugu zao kwa Taifa letu kwa Mara ya mwisho kupitia manunuzi ya jeneza, sanda, mafuta ya kumpaka Marehemu,sabuni ya kumuogeshea Marehemu,mashada,msalaba,usafiri wa kusafirisha mwili wa Marehemu maana hata Kama gari lilikuwa la Marehemu bado litawekwa mafuta ili litembee kwenda kubeba mwili wa Marehemu ambapo mafuta yanayotumika kwenye gari tayari yanakuwa yamekatwa kodi.

Ndiyo maana watanzania wanaumia Sana wanaposikia ripoti ikionyesha ufujaji wa mabillioni ya pesa zao, wanaumia kwa kuwa wanaona fedha hizo zingewasaidia au kuwekezwa katika Afya maana Kuna watu wakati mwingine wanaishiwa fedha Hadi kufikia hatua hospital inashikilia mwili wa Marehemu mpaka fedha za matibabu zilipwe na ndugu licha ya kuwa huduma iliyotolewa haijamponya aliyekuwa mgonjwa,

Wanaona mapesa hayo yangewekezwa hata kwenye huduma za maji, Miundombinu,umeme, au kupeleka kwenye shule za kata ili zinunue hata vifaa vya maabara au serikali ingezitumia kuajiri vijana na kuwalipa mishahara ili wakaongeze Kasi ya utoaji huduma kwa watanzania katika maeneo yenye uhitaji mkubwa Kama vile Elimu na Afya.

Lakini watanzania wamebaki watulivu mioyoni mwao kwa kuwa Wana Imani na Rais wao pamoja na serikali yao,wanasema kwa kuwa Rais Samia Ni msikivu, mzalendo, Jasiri, shupavu, madhubuti na imara, Wana Imani naye kubwa Sana mh Rais na ndio maana hawana wasiwasi Wala hofu.

Ndio maana kupitia jukwaa hili napenda Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani afikishiwe ujumbe huu kuwa wale wote waliobainika kufuja fedha za umma wawekwe pembeni haraka Sana ili wasije haribu Nyaraka muhimu zitakazo saidia katika upelelezi, wakamatwe na wafunguliwe mashitaka, wasiruhusiwe kutoka ndani ya mipaka ya Tanzania, wafuatiliwe mienendo Yao na ya mitandao, akaunti zao benki na za watu wa karibu yao Kama vile mke au mume au watoto zifuatiliwe kuangalia Kama zinaendana na vipato vyao, miradi na vitega uchumi vyao vifuatiliwe na kuchunguzwa kwa jicho la kijasusi ili kuangalia Kama vinaendana na vipato vyao,pia iangaliwe Kama vimewahi kulipa Kodi na kutambuliwa.

Namshauri Rais wangu kwa unyenyekevu na kwa magoti kwa heshima na kwa upendo mkubwa Sana kuwawajibisha bil hirum wala haya Wala simile Wala kuchelewa Wala hofu maana asiye na makosa atabainikaga mbele y safari kwa kadri upelelezi utakavyokuwa unafanyika kwa kuwa hii itamfanya kila mtu kuziogopa pesa za umma Kama ukoma, kila mtu atatambua kuwa pesa za umma Ni za Moto, kila mtu atatambua kuwa huwezi ukabaki salama katika uongozi wa Rais Samia ukibainika kugusa pesa za umma, hata Hawa wa chini kiuongozi nao watafanya vitu kwa uadilifu mkubwa Sana na heshima kubwa Sana kwa pesa za umma maana watakuwa wameona Moto unaowaka mlimani ,hivyo watajuwa moto huo utakuwa mkubwa Sana kwao na wenye kuacha maumivu na majeraha na majuto makubwa Sana ukiwafikia pale watakapo gusa pesa za umma.

Lazima wababaishaji wapitishwe katika njia ya Moto na njia ya majuto kisheria na kinidhamu kwa mujibu wa sheria zetu.

Niseme wazi bila unafiki kuwa hata mimi nimeumia Sana kusikia ufujaji huu,maana nikiangalia tunavyohangaika mitaani katika jua na katika mvua mpaka sura zetu zinakuwa na kubakia kama wazee kutokana na kupambana katika utafutaji wa maisha inaumiza Sana unaposikia wale tuliowapa dhamana ya uongozi wanapokosa uzalendo, uchungu, utu, uungwana, uadilifu na weledi katika pesa za umma na kubakia Kuchezea Fedha za Umma,Inatupa hasira Sana vijana kwa kuwa tunatambua Taifa letu Lina wasomi wa kutosha ambapo haina hata sababu ya kuwabembeleza Hawa wachache walioshindwa kuridhika na vipato vyao.

Nasema tena Hawa wabadhirifu wasibembelezwe Wala kupewa nafasi ya Kuendelea kuhudumu katika nafasi zao,watolewe haraka Sana na kuletea wazalendo watakao kuwa na uchungu na watanzania.

Rais Samia suluhu Hassani tuondolee watu Hawa, waambie warudishe fedha zetu, wakabe mpaka waziteme, wabane mpaka waziachie, hatupendi kusikia hivyo juu ya Fedha zetu, tunaumia, inatuumiza Rais, inatutia machozi mh Rais, inatuvunja nguvu Rais na hata wewe mwenyewe Itakuumiza na kukukwamisha katika utafutaji wa fedha maana itakuwa Ni Kama unajaza maji katika ndoo iliyotoboka au kikapu chenye matobo au pipa linalovuja.

Rais Samia suluhu Hassani Rais wetu mpendwa na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama tunakuomba utufute machozzi watanzania.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Hakika ukiisikia ripoti ya CAG utajua kuwa viongozi wa nchi hii hawana uchungu kabisa na fedha za serikali. Kama ni kuonya umewaonya sana lakini bado wanaiba.

Pamoja na agizo lako la kuwa watupishe binafsi nakuomba usiishie hapo wale wote waliotuibia na kusababisha upotevu wa fedha za serikali wote wakamatwe na kufunguliwa kesi za ufisadi na kuwataka warudishe hizo fedha kwani hawana uchungu na wananchi. Haiwezekani watu wachache wale keki ya taifa kwa kuiba na kuisababishia serikali hasara.

Halmashauri zetu kumekuwa mchwa fedha zinapigwa wanavyotaka bil.11 eti zimeyeyuka

Mashirika kama atcl tanesco tra ttcl kote huko ni wizi bado kuna mabilioni ya plea bargaing yamepigwa na wahusika wapo wanakucheka.

Rais wakati umefika wa kuonyesha kukasirika kwako kwa vitendo tunakuomba sana agiza vyombo vyako viwabane wahusika warudishe fedha hizo nakuapia watazirudisha tu hakuna aliye juu yako wewe ni rais na amiri jeshi mkuu.
JamiiForums1563802633.jpg
JamiiForums619449509.jpg
JamiiForums1814050645.jpg
JamiiForums-671446292.jpg
JamiiForums1342636393.jpg
JamiiForums839866055.jpg
 
Kwenye

Mshahara wangu nakatwa 1.1 million as PAYE kila mwezi.inauma sana aisee mpaka nappenda kazini kwangu hakuna lami kumbe watu wanakula Kodi zetu
Watanzania wengi wameumia Kama ambavyo mh Rais wetu mpendwa mama Samia ameumia na Tunaamini atawachukulia hatua kali Sana wahusika wote
 
wapandishwe vyeo na wanunuliwe VX V8 mpya za kutumia, HUO ndio Uzalendo wamefanya. kuwafukuza kazi na kuwafunga utakuwa udikteta kama yule dhalimu...
Rais wetu anao uchungu mkubwa sana na Watanzania pamoja na Taifa letu,juhudi zote ambazo amekuwa akifanya zimekuwa ni kwa ajili ya kutaka kutimiza Ndoto yake ya kuona kila Mtanzania anainuka kiuchumi na Taifa letu linasonga mbele kimaendeleo,hivyo hawezi kumfumbia macho yeyote atakayebainika kufuja pesa za umma
 
Ndugu zangu watanzania,

Kitendo Cha ripoti ya CAG kuonyesha ufujaji wa mabillioni ya pesa zao katika baadhi ya maeneo kimewaumiza Sana watanzania,kimewatoa machozi ,kimewapiga ganzi mioyo Yao,kimewapa ubaridi mioyo Yao,kimewasikitisha,kimewahuzunisha Sana,kimewapa maumivu mioyo Yao,kimewafanya wakae chini kwa kukosa nguvu.

Hii Ni kutokana na uchungu walio nao katika fedha zao, watanzania wanajuwa kuwa hizo Ni fedha zao,Ni michango yao ,ni Kodi zao,Ni tozo zao,,Ni ushuru wao,Ni fedha wanazochanga watanzania kwa ujumla wao bila kujali ni yatima au mgonjwa au mjane au mzee ,wote wanalipa Kodi kupitia kununua bidhàa.

Hata Marehemu nao wanapokuwa wamefariki na kuaga Dunia na kutangulia mbele za haki nao kabla ya kuzikwa wanalipa Kodi kupitia ndugu zao kwa Taifa letu kwa Mara ya mwisho kupitia manunuzi ya jeneza,sanda, mafuta ya kumpaka Marehemu,sabuni ya kumuogeshea Marehemu,mashada,msalaba,usafiri wa kusafirisha mwili wa Marehemu maana hata Kama gari lilikuwa la Marehemu bado litawekwa mafuta ili litembee kwenda kubeba mwili wa Marehemu ambapo mafuta yanayotumika kwenye gari tayari yanakuwa yamekatwa kodi.

Ndio maana watanzania wanaumia Sana wanaposikia ripoti ikionyesha ufujaji wa mabillioni ya pesa zao,wanaumia kwa kuwa wanaona fedha hizo zingewasaidia au kuwekezwa katika Afya maana Kuna watu wakati mwingine wanaishiwa fedha Hadi kufikia hatua hospital inashikilia mwili wa Marehemu mpaka fedha za matibabu zilipwe na ndugu licha ya kuwa huduma iliyotolewa haijamponya aliyekuwa mgonjwa,

Wanaona mapesa hayo yangewekezwa hata kwenye huduma za maji, Miundombinu,umeme, au kupeleka kwenye shule za kata ili zinunue hata vifaa vya maabara au serikali ingezitumia kuajiri vijana na kuwalipa mishahara ili wakaongeze Kasi ya utoaji huduma kwa watanzania katika maeneo yenye uhitaji mkubwa Kama vile Elimu na Afya.

Lakini watanzania wamebaki watulivu mioyoni mwao kwa kuwa Wana Imani na Rais wao pamoja na serikali yao,wanasema kwa kuwa Rais Samia Ni msikivu,mzalendo ,Jasiri , shupavu ,madhubuti na imara, Wana Imani naye kubwa Sana mh Rais na ndio maana hawana wasiwasi Wala hofu.

Ndio maana kupitia jukwaa hili napenda Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani afikishiwe ujumbe huu kuwa wale wote waliobainika kufuja fedha za umma wawekwe pembeni haraka Sana ili wasije haribu Nyaraka muhimu zitakazo saidia katika upelelezi ,wakamatwe na wafunguliwe mashitaka ,wasiruhusiwe kutoka ndani ya mipaka ya Tanzania,wafuatiliwe mienendo Yao na ya mitandao,akaunti zao benki na za watu wa karibu yao Kama vile mke au mume au watoto zifuatiliwe kuangalia Kama zinaendana na vipato vyao,miradi na vitega uchumi vyao vifuatiliwe na kuchunguzwa kwa jicho la kijasusi ili kuangalia Kama vinaendana na vipato vyao,pia iangaliwe Kama vimewahi kulipa Kodi na kutambuliwa.

Namshauri Rais wangu kwa unyenyekevu na kwa magoti kwa heshima na kwa upendo mkubwa Sana kuwawajibisha bil hirum wala haya Wala simile Wala kuchelewa Wala hofu maana asiye na makosa atabainikaga mbele y safari kwa kadri upelelezi utakavyokuwa unafanyika kwa kuwa hii itamfanya kila mtu kuziogopa pesa za umma Kama ukoma,kila mtu atatambua kuwa pesa za umma Ni za Moto,kila mtu atatambua kuwa huwezi ukabaki salama katika uongozi wa Rais Samia ukibainika kugusa pesa za umma,hata Hawa wa chini kiuongozi nao watafanya vitu kwa uadilifu mkubwa Sana na heshima kubwa Sana kwa pesa za umma maana watakuwa wameona Moto unaowaka mlimani ,hivyo watajuwa moto huo utakuwa mkubwa Sana kwao na wenye kuacha maumivu na majeraha na majuto makubwa Sana ukiwafikia pale watakapo gusa pesa za umma.

Lazima wababaishaji wapitishwe katika njia ya Moto na njia ya majuto kisheria na kinidhamu kwa mujibu wa sheria zetu.

Niseme wazi bila unafiki kuwa hata mimi nimeumia Sana kusikia ufujaji huu,maana nikiangalia tunavyohangaika mitaani katika jua na katika mvua mpaka sura zetu zinakuwa na kubakia kama wazee kutokana na kupambana katika utafutaji wa maisha inaumiza Sana unaposikia wale tuliowapa dhamana ya uongozi wanapokosa uzalendo ,uchungu ,utu,uungwana, uadilifu na weledi katika pesa za umma na kubakia Kuchezea Fedha za Umma,Inatupa hasira Sana vijana kwa kuwa tunatambua Taifa letu Lina wasomi wa kutosha ambapo haina hata sababu ya kuwabembeleza Hawa wachache walioshindwa kuridhika na vipato vyao.

Nasema tena Hawa wabadhirifu wasibembelezwe Wala kupewa nafasi ya Kuendelea kuhudumu katika nafasi zao,watolewe haraka Sana na kuletea wazalendo watakao kuwa na uchungu na watanzania.

mh Rais ,mh Rais mh Rais mama Samia suluhu Hassani tuondolee watu Hawa,waambie warudishe fedha zetu,wakabe mpaka waziteme,wabane mpaka waziachie,hatupendi kusikia hivyo juu ya Fedha zetu,tunaumia mh Rais ,inatuumiza mh Rais ,inatutia machozi mh Rais,inatuvunja nguvu mh Rais na hata wewe mwenyewe Itakuumiza na kukukwamisha katika utafutaji wa fedha maana itakuwa Ni Kama unajaza maji katika ndoo iliyotoboka au kikapu chenye matobo au pipa linalovuja.

Mh Rais mh Rais mh Rais mh Rais mama Samia suluhu Hassani Rais wetu mpendwa na Amiri Jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama tunakuomba utufute machozzi watanzania.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

Naomba moderator wasiunganishe Uzi wangu na mwingine wowote kwa kuwa wangu unajitegemea kimaudhui.
Umesahau hili wa jina

moderator wasiunganishe na nyuzi nyingine kwa kuwa uzi wako unatafuta"Teuzi" kwa udi na uvumba.
 
Umesahau hili wa jina

moderator wasiunganishe na nyuzi nyingine kwa kuwa uzi wako unatafuta"Teuzi" kwa udi na uvumba.
Hapana wajina Mimi Ni sitafuti uteuzi Bali naandika kwa maslahi ya Taifa na siku zote wazalendo hufanya kazi kwa kujitolea pasipo kusubiri kulipwa Fadhira.
 
Back
Top Bottom