Ugali wa jana

Kuna familia niliwahi kwenda binti wa kazi anaambiwa mpakulie mgeni, binti akasema chakula kimeisha umebaki ugali wa kaka(shamba boy). Hadi leo sijaielewa ile kauli kwa kweli.

Mkuu ugali uliolala hua tuna uweka kwenye mfuko wa plastiki then tunaweka kwenye sufulia lenye maji tunachemsha fresh kabisa
 
Dah! Umenikumbusha mbali. Hii mbinu hawa kina "Junior" hawawezi kuijua.
 
Reactions: ABJ
Wasukuma hula ugali asubuhi, mchana, usiku na wakati mwingine usiku wa manane huamka na kuusonga Tena ule ulio mgumuuuu.
 
Mkuu Bujibuji ngoja nikupe njia ninayotumia mie kutotupa ugali. Hakikisha ugali unaobaki unauhifadhi kwenye friji ukiwa bonge Moja (unaweza kuuviriga kwa shepu unayotaka).
Asubuhi chukua Ugali ukate slesi jinsi unavyopenda, hizo slesi zinyunyizie chumvi na pilipili manga Kwa mbali. Andaa kikaango na mafuta (samli nzuri zaidi). Weka kwenye moto vikaange had viwe na rangi ya njano brown. Ipua weka mezani kula na familia. Lete mrejesho.
 
Nimeipenda hiii mbinu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…