Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
Nami nashika Kalamu
Kuundeleza utamu
Mtamu au si mtamu
Ngoja nitie mashamsham
Ukila na supu ya pweza
Kuna vingi waongeza
Ulimini wa teleza
Kwa mlenda utaweza
Kwa karanga ya kusaga
Hawaujui wachaga
Wazaramo waumega
Kuimarisha laliga!!
Umeutaja ugali, nami nataka usifu
Imenipasa ugali, kuupa sifa sanifu
Ugali si wa hoteli, wa nyumbani ni yakinifu
Ugali kweli mtamu, wa mahindi pia muhogo
Uweke mashamushamu, na mtindi usio chongo
Ugali watia hamu, unanikumbusha Bongo
Ugali yake mchana, usiku utavimbiwa
Kwa bamia unajichana,au kisamvu cha sawasawa
Ugali kweli mwanana, unanikumbusha Maswa
Kwa samaki au nyama, ugali utaupenda
Tena upikwe na mama, baba atautenda
Ugali watia hima, hongera kwa kuupenda
mwasifia ugali, ugali chakula gani
mwasifia ugali, ugali chakula duni
mwasifia ugali, chakula cha maskini
Hunilishi mi ugali kwa bakora matakoni
bora nijilie wali, chakula chetu cha pwani
ugali ni wa makuli, wapagazi bandarini
Muungwana na ugali, wapi na wapi jamani
hawali kwenye shughuli, wala kule matangani
sijaona wakila ugali, hata uko harusini
Leo wasifia ugali, eti chakula makini
Ugali kula mchana, sasa masharti ya nini
Kama ugali mwanana, usiku mwaukimbiani
A utavimbirwa sana, sasa usiku mwalani
Nimejaribu ugali na kisamvu
Kweli mchanganyiko mtamu
Nikanyunyuzia chachandu
Na nyama kuongezea hamu
Ugali uchanganyike na makange
Huwezi kufananisha na makande
Upate mtaalam akutengenezee
Utatamani kila siku ujipendelee
Ugali naupenda kula na dagaaa
Jamani siwezi kueleza yake raha
Wawe ni wa Kigoma au Mwanza
Nakwambia kitamu hicho chakula
Nimejaribu tu ila napenda kula ugali...
SMU, kumbe na wewe makange unayapenda tena pale RG (rozigadeni) ni mazuri sana. Ushindwe wewe tu mana kuna ya kuku, ng'ombe au mbuzi.Umenikumbusha makange na week end ndo inaanza...Lol
Nimejaribu ugali na kisamvu
Kweli mchanganyiko mtamu
Nikanyunyuzia chachandu
Na nyama kuongezea hamu
Ugali uchanganyike na makange
Huwezi kufananisha na makande
Upate mtaalam akutengenezee
Utatamani kila siku ujipendelee
Ugali naupenda kula na dagaaa
Jamani siwezi kueleza yake raha
Wawe ni wa Kigoma au Mwanza
Nakwambia kitamu hicho chakula
Nimejaribu tu ila napenda kula ugali...
Belinda na Mwanakijiji, Poleni kwa kusifia
Chakula cha wanakijiji,Ugali kufakamia
Mie ugali wa nini,na wali nimuachie nani??
Ugali chakula gani, nyie wote kukisifia??
Ugali chakula gani, Watu kukisifia
Ugali kwa mboga ya majani, wanakijiji kujilia
Ugali si chakula ghali,kwa fedha kidogo kujinunulia
Ugali chakula gani,nyie wote kukisifia??
Mie ugali sili,hata kwa ngumi na bakora
Hata shuleni walikiri,mpaka kuchapwa bakora
Ugali siupendi nakiri,Hata kama ni chakula bora
Ugali chakula gani,nyie wote kukisifia??
Ugali kwa mandondo haupandi,bora unipatie wali
Hata watoto hawapendi,weye pitisha wali
Huwezi kula kwa mtindi, Bora jaribu kwa wali
Ugali chakula gani,nyie wote kukisifia???
Mkubwa nimekupata, sikuwezi wewe kwa wali
Nakushauri siku moja, jaribu kuupika huo ugali
Na uipendayo mboga, uzoee angalau kila wiki
Bado debe naupigia, hakika kitamu chakula hiki.
Mtu wa kawaida ujue, kuna aina tele za vyakula
Ila kwa wakati uleule, fulani aina zaidi utapenda
Labda wali na kunde, biriani na pia ndizi nyama
Jitahidi nao ugali ule, utauona mtamu kupitiliza.
Raha ya kula huo ugali, uivishe vizuri kwa kupika
Wakati mambo ya wali, makini mchele kupembua
Mawe kutoa kiumakini, muda unapotea kuandaa
Wali siyo tu kula wali, hadi uive ni kazi kuvumilia.
Ugali ukiacha unafuu, nakwambia hiki kinashibisha
Mwili kuupa zake nguvu, mwili kuupatia na wanga
Mpinzani hamna kiutamu, ukiula na mboga mboga
Tena nakusisitizia mkuu, ugali ndo chakula bomba.