Ugali kweli mtamu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,463
39,929
Ugali kweli mtamu,
Kwa huo ninayo hamu,
Kwa mboga yenye saumu!

Ugali tangu shuleni
Jamani hadi jeshini
Nikaula na chuoni

Ugali iwe mchana
Kwenye upepo mwanana
Mwenzenu ninajichana

Ugali hata jioni,
Mezani au jikoni
Nikishatoka kazini

Ugali iwe kwa mboga
Sima kwa kweli yanoga
Kwa tembele na maboga!

Ugali kwa kurumagia
Vidole kujilambia
Na nyama inanukia!

Ugali ule kwa mchuzi
Wa samaki hata mbuzi,
Mwanawane kama kazi!

Ugali msosi wa nguvu
Haupikwi kwa wavivu,
Au walio wachovu

Ugali uwe kiporo
Alfajiri na mmajoro
Kwa mapanki ya Nyamanoro!

Ugali nimesifia
Wali ninautungia
Beti nitaupangia,

Ugali nafakamia
Matonge navingiria
Nakula nafikiria

UGALI KWELI MTAMU!!

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
 
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
__________________

HII KIBOKO MZEYA!halafu pia nadhani ulikuwa na 'C' ya kiswahili O-LEVEL,au sio?
 
Nami nashika Kalamu
Kuundeleza utamu
Mtamu au si mtamu
Ngoja nitie mashamsham

Ukila na supu ya pweza
Kuna vingi waongeza
Ulimini wa teleza
Kwa mlenda utaweza

Kwa karanga ya kusaga
Hawaujui wachaga
Wazaramo waumega
Kuimarisha laliga!!
 
Aaah, hii safi sana wazee!
Mie nimependa zaidi pale alipotumia neno la kilugha "mmajoro"
 
Nami nashika Kalamu
Kuundeleza utamu
Mtamu au si mtamu
Ngoja nitie mashamsham

Ukila na supu ya pweza
Kuna vingi waongeza
Ulimini wa teleza
Kwa mlenda utaweza

Kwa karanga ya kusaga
Hawaujui wachaga
Wazaramo waumega
Kuimarisha laliga!!

ahahahahahahaha, angalia sirikali itakukamata. ze*****.com
 
Umeutaja ugali, nami nataka usifu
Imenipasa ugali, kuupa sifa sanifu
Ugali si wa hoteli, wa nyumbani ni yakinifu

Ugali kweli mtamu, wa mahindi pia muhogo
Uweke mashamushamu, na mtindi usio chongo
Ugali watia hamu, unanikumbusha Bongo

Ugali yake mchana, usiku utavimbiwa
Kwa bamia unajichana,au kisamvu cha sawasawa
Ugali kweli mwanana, unanikumbusha Maswa

Kwa samaki au nyama, ugali utaupenda
Tena upikwe na mama, baba atautenda
Ugali watia hima, hongera kwa kuupenda
 
mwasifia ugali, ugali chakula gani
mwasifia ugali, ugali chakula duni
mwasifia ugali, chakula cha maskini

Hunilishi mi ugali kwa bakora matakoni
bora nijilie wali, chakula chetu cha pwani
ugali ni wa makuli, wapagazi bandarini

Muungwana na ugali, wapi na wapi jamani
hawali kwenye shughuli, wala kule matangani
sijaona wakila ugali, hata uko harusini
Leo wasifia ugali, eti chakula makini

Ugali kula mchana, sasa masharti ya nini
Kama ugali mwanana, usiku mwaukimbiani
A utavimbirwa sana, sasa usiku mwalani
 
Nimejaribu ugali na kisamvu
Kweli mchanganyiko mtamu
Nikanyunyuzia chachandu
Na nyama kuongezea hamu

Ugali uchanganyike na makange
Huwezi kufananisha na makande
Upate mtaalam akutengenezee
Utatamani kila siku ujipendelee

Ugali naupenda kula na dagaaa
Jamani siwezi kueleza yake raha
Wawe ni wa Kigoma au Mwanza
Nakwambia kitamu hicho chakula

Nimejaribu tu ila napenda kula ugali...
 
Ugali watia nguvu, kwa mtu mchapa kazi
Wali ni wa wavivu, na wasio wachapa kazi
Wanauonea wivu, waswahili wa kaskazi

Ugali wa masikini, na matajiri pia
Ugali chakula makini, wali hutofikia
Hakuna mfano yakini, ugali kuukaribia

Matangani na harusini, ugali wamebaini
Harusi zote makini, ugali ni namba wani
Wasomi wameubaini,na wanazuoni makini

Wali wakifu mapema, ugali huwezi kamwe
Wali waweza tema, mara nyingi una mawe
Ugali chakula chema, katu hauna mawe

Wali wanyima 'choo', tabibu atakwambia
Kwa nini wajipa soo, wali kuukimbilia
Wali chakula hovyo, watoto tu hukimbilia

Ugali yake mchana, na usiku mara chache
Wali katu mchana, sitaki ‘choo’ cha mche
Ugali chakula mwanana, sifa zake si chache
 
Nimejaribu ugali na kisamvu
Kweli mchanganyiko mtamu
Nikanyunyuzia chachandu
Na nyama kuongezea hamu

Ugali uchanganyike na makange
Huwezi kufananisha na makande
Upate mtaalam akutengenezee
Utatamani kila siku ujipendelee

Ugali naupenda kula na dagaaa
Jamani siwezi kueleza yake raha
Wawe ni wa Kigoma au Mwanza
Nakwambia kitamu hicho chakula

Nimejaribu tu ila napenda kula ugali...

Umenikumbusha makange na week end ndo inaanza...Lol

Belinda amejaribu, wa kisamvu amebaini
Nyama choma na chachandu, mchanganyiko makini
Ugali kweli mtamu, jaribu wa ‘rozigadeni' (Rose Garden! Lol)

Ugali ule kwa ‘makange', mpishi utamsifu
Haufanani na makande, ingawa nayo nadhifu
Ugali yake makange, kila siku utausifu

Ugali pia mtamu, hata kwa dagaa chaza
Ukitaka dagaa watamu, ni wa Kigoma au wa Mwanza
Ugali dagaa mtamu, hakika huwezi saza
 
Ugali ugali gani, wa muhogo si mtama?
Ugali wataka fani, si urongo kufakama
Pate kula na mwandani, tonge kama danadana
Matumbo yaache ghani, kwa yabisi kukakana

Ugali upate moto, kamwe si wa kupooza
Weka kati na mtoto, na kitoweo kutoza
Viringo kipara ngoto, kwa samaki wa kufyonza
Tonge kubwa ka kokoto, sijepaliwa kuponzwa

Weka bondo katikati, livute kama manati
Kama muhogo bahati, kwa bada tafanya pati
Silifiche kwa kabati, weka pahali pa chati
Sitotamani chapati, lau kwa vikalimati

Ugali pata Sikonge, Wanyamwezi wa Tabora
Wanaoukata tonge, utafikiri kombora
Ugali wa afya bonge, timiza chakula bora
Wallahi naona donge, ugali watia fora

Wala wali wala nini?, ugali nauamini
Nimeulia yamini, lazima niweke chini
Bila mboga kwa jibini, au mtindi makini
Ugali nauthamini, ni kweli si magirini

Upate wa mamsapu, aliejulia mabuja
Unga kibaba kwa kapu, kikatulizwa kwa kuja
Hutamani lapulapu, rojorojo la kuvuja
Hutaki hata vishapu, karafuu za Unguja

Ugali tangu Kibondo, mpaka wa Mnyasini
Hauhitaji vionjo, marashi mdalasini
Rahisi pata uhondo, tena bila walakini
Ya kweli wala si rongo, si chakula masikini

Ugali kula ushibe, upate nguvu za kazi
Ugali kula ushinde, bila ya mang'azing'azi
Ugali kula upinde, kisha tafuta malazi
Usije kula ulinde, usingizi wazi wazi

Shurti uchume mboga, inayoungwa bunifu
Ugali si kama togwa, utalinywa bila kifu
Shurti hata kwa boga, lilochemshwa na bifu
Ugali kama kulogwa, hakika ya yakinifu
 
Last edited:
Umenikumbusha makange na week end ndo inaanza...Lol
SMU, kumbe na wewe makange unayapenda tena pale RG (rozigadeni) ni mazuri sana. Ushindwe wewe tu mana kuna ya kuku, ng'ombe au mbuzi.

Bado nipo na ugali.....

Kuna siku niliusonga ugali
Na sato aliyeungiwa nazi
Kushushia nikanywa maji
Hakika ulikuwa mlo kamili

Ugali pia ukiliwa nao mtindi
Tanga fresh ni mtamu zaidi
Kama upo kijijini mtindi asili
Uliovundikwa huko kibuyuni

Ugali pia wanogea maharage
Mboga ya majani uchanganyie
Iwe mnafu au mchicha vilevile
Kajaribu kula na uje unisimulie
 
Nimejaribu ugali na kisamvu
Kweli mchanganyiko mtamu
Nikanyunyuzia chachandu
Na nyama kuongezea hamu

Ugali uchanganyike na makange
Huwezi kufananisha na makande
Upate mtaalam akutengenezee
Utatamani kila siku ujipendelee

Ugali naupenda kula na dagaaa
Jamani siwezi kueleza yake raha
Wawe ni wa Kigoma au Mwanza
Nakwambia kitamu hicho chakula

Nimejaribu tu ila napenda kula ugali...

Belinda na Mwanakijiji, Poleni kwa kusifia
Chakula cha wanakijiji,Ugali kufakamia
Mie ugali wa nini,na wali nimuachie nani??
Ugali chakula gani, nyie wote kukisifia??

Ugali chakula gani, Watu kukisifia
Ugali kwa mboga ya majani, wanakijiji kujilia
Ugali si chakula ghali,kwa fedha kidogo kujinunulia
Ugali chakula gani,nyie wote kukisifia??

Mie ugali sili,hata kwa ngumi na bakora
Hata shuleni walikiri,mpaka kuchapwa bakora
Ugali siupendi nakiri,Hata kama ni chakula bora
Ugali chakula gani,nyie wote kukisifia??

Ugali kwa mandondo haupandi,bora unipatie wali
Hata watoto hawapendi,weye pitisha wali
Huwezi kula kwa mtindi, Bora jaribu kwa wali
Ugali chakula gani,nyie wote kukisifia???
 
Mkubwa nimekupata, sikuwezi wewe kwa wali
Nakushauri siku moja, jaribu kuupika huo ugali
Na uipendayo mboga, uzoee angalau kila wiki
Bado debe naupigia, hakika kitamu chakula hiki.

Mtu wa kawaida ujue, kuna aina tele za vyakula
Ila kwa wakati uleule, fulani aina zaidi utapenda
Labda wali na kunde, biriani na pia ndizi nyama
Jitahidi nao ugali ule, utauona mtamu kupitiliza.

Raha ya kula huo ugali, uivishe vizuri kwa kupika
Wakati mambo ya wali, makini mchele kupembua
Mawe kutoa kiumakini, muda unapotea kuandaa
Wali siyo tu kula wali, hadi uive ni kazi kuvumilia.

Ugali ukiacha unafuu, nakwambia hiki kinashibisha
Mwili kuupa zake nguvu, mwili kuupatia na wanga
Mpinzani hamna kiutamu, ukiula na mboga mboga
Tena nakusisitizia mkuu, ugali ndo chakula bomba.
 
Katika vyakula vyema, hakuna kama muhogo
muhogo hauwi mwema, kwa makambare ngogo
sharti upate nyama, japo ngozi ya kichogo
 
Mkubwa nimekupata, sikuwezi wewe kwa wali
Nakushauri siku moja, jaribu kuupika huo ugali
Na uipendayo mboga, uzoee angalau kila wiki
Bado debe naupigia, hakika kitamu chakula hiki.

Mtu wa kawaida ujue, kuna aina tele za vyakula
Ila kwa wakati uleule, fulani aina zaidi utapenda
Labda wali na kunde, biriani na pia ndizi nyama
Jitahidi nao ugali ule, utauona mtamu kupitiliza.

Raha ya kula huo ugali, uivishe vizuri kwa kupika
Wakati mambo ya wali, makini mchele kupembua
Mawe kutoa kiumakini, muda unapotea kuandaa
Wali siyo tu kula wali, hadi uive ni kazi kuvumilia.

Ugali ukiacha unafuu, nakwambia hiki kinashibisha
Mwili kuupa zake nguvu, mwili kuupatia na wanga
Mpinzani hamna kiutamu, ukiula na mboga mboga
Tena nakusisitizia mkuu, ugali ndo chakula bomba.

Belinda mkuu wangu,Ugali kwangu bado
Hata upikwe kwangu,Bado hii ni bondo
Sitaki umiza roho yangu, Kwa kuila hii bondo
Ugali kwangu sili, Hata kama chakula bora

Ugali huwezi tia nazi, Wala katia mbatata
Ugali sharti ulie mchuzi, Wakati wali hata kwa mbata
Ugali wapeni wachuuzi,Mie wala hamtanipata
Ugali kwangu sili , Hata kama chakula bora

Ugali chakula gani,Kina pishi aina moja
Uende hata mtaa gani, Pishi ni hilo hilo moja
Toka Kigoma mpaka Pwani, Mpikowe ni mmoja
Ugali kwangu sili, Hata kama chakula bora

Wali pishi mbalimbali, zote zakubalika
Wali mataifa mbalimbali,kote inakubalika
Ugali sio cha wambali, ni cha watanganyika
Ugali kwangu sili, Hata kama chakula bora
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom