Ugaidi watikisa tena Morogoro Tanzania

Ugaidi watikisa tena Morogoro Tanzania

waltham

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2014
Posts
2,522
Reaction score
1,045
POLE POLE SHABAAB WANAENDELEA KUMEA MIZIZI TANZANIA. NILIWAI SEMA HAPA USIMDHARAU JIRANI YAKO NA NYUMBA YAKO IMEEZEKWA NA VIOO. USIRUSHIA MAWE KAMWE!

Ugaidi watikisa tena Morogoro




majeruhi.jpg
Mmoja wa majeruhi wa bomu lililorushwa kwa mkono katika Kijiji cha Msolwa wilayani Kilombero jana akiwa Hospitali ya Mt Kizito iliyopo Mikumi mkoani Morogoro. Picha na Liliani Lucas
Na Lilian Lucas, Mwananchi

Posted Jumapili,Mei3 2015 saa 10:16 AM

KWA UFUPI

  • Aprili 14 mwaka huu, watu tisa walikamatwa katika msikiti wa Suni katika kijiji cha Nyandeo kata ya Kidatu wakiwa na milipuko 30, sare za jeshi, bendera nyeusi, majambia, bisibisi, maski, misumeno ya chuma, spana piperange, madaftari, vitabu mbalimbali vikiwemo vya risiti wakituhumiwa kwa ugaidi.




n



Morogoro. Tishio la ugaidi limezidi kuwa tete baada ya watu wanaoshukiwa kufanya vitendo hivyo kulipua bomu na kusababisha watu watano kujeruhiwa wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa, kilichoko Kata ya Sanje wilayani Kilombero.

Hili ni tukio la pili kutokea kwenye Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro baada ya watu tisa kukamatwa kwenye Msikiti wa Suni wakiwa na silaha na vifaa vingine vinavyohusishwa na harakati za kigaidi.

Mbali na matukio hayo ya Morogoro, hivi karibuni vikosi vya ulinzi na usalama vilipambana vikali na watu wanaoshukiwa kuwa ni magaidi kwenye mapango ya kihistoria ya Amboni mkoani Tanga. Hadi sasa polisi haijatoa taarifa ya kina kuhusu tukio hilo lililopoteza maisha ya mwanajeshi mmoja.

Kamanda wa polisi mkoani Morogoro hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo, wakati msemaji wa Jeshi la Polisi alisema tukio hilo liko ndani ya mipaka ya mkoa hivyo linatakiwa lizungumzwe na mamlaka hiyo badala ya makao makuu ya chombo hicho cha dola.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea walieleza kuwa bomu hilo lilirushwa kuelekea kwenye gari la mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero saa 2:00 usiku. Bomu hilo lilirushwa na watu wawili ambao awali walidhibitiwa na wananchi baada ya kuwashuku kuwa siyo raia wema.

Baada ya kuwatilia shaka, wananchi waliwaweka watu hao chini ya ulinzi na wakati wakiwapekua, walitoa bomu na kulirusha kwenye gari hilo lililokuwa limeegeshwa na kujeruhi watu watano, akiwamo dereva.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, David Ligazio aliwataja waliojeruhiwa katika tuko hilo kuwa ni Novatus Ngapi, ambaye ni dereva na Thomas Manjole, ambaye ni mgambo na hali yake inadaiwa kuwa siyo nzuri.

Wengine waliojeruhiwa ni Amos Msopole, Azama Naniyunya, ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo Mikumi wilayani Kilosa na Anna Pius ambaye amepata majeraha kidogo na kuruhusiwa.

Ligazio, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, alisema baada ya kumaliza kuhutubia alikuwa akizungumza na wananchi huku akielekea kwenye gari na ndipo aliposikia kishindo kikubwa na kuona vioo vya gari yake vikivunjika na watu kadhaa kujeruhiwa.

Ofisa mtendaji wa Kata ya Sanje, Hawa Ndachuwa alisema siku ya tukio watu wawili walikodi pikipiki kutoka Kata ya Kidatu na kuomba wapelekwe Kata ya Mkula na walipofika Msolwa Ujamaa, dereva wa bodaboda aliwatilia shaka na kujifanya anawaomba wamuongezee fedha za malipo kwani walipatana kiasi kidogo mwanzoni wakati safari ilikuwa ya mbali.

Ndachuwa alisema ilibidi watu hao wakubali kumuongezea fedha na walimwambia watafute sehemu ya kutolea fedha na yeye akawapeleka eneo la kutolea fedha. Alisema wakati watu hao wakihangaika kutoa fedha, mwendesha bodaboda huyo alitoa taarifa kwa uongozi wa kitongoji ambao waliwasiliana na polisi kwa ajili ya kuwafuata na kuwapekua watuhumiwa hao.

Alisema baada ya watu hao kuwa katika mabishano, wananchi walipatwa na mshtuko kutokana na mavazi waliyovaa na kisha kuwaweka chini ya ulinzi na kuanza kuwapekua.







 

Similar Discussions

Back
Top Bottom