Ugaidi katika utamaduni wa binadamu

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
20,897
63,783
"Katika dunia ya leo ambayo silaha za Kinyuklia zimeyafanya majeshi yasiwe na umaana wowote ule, ugaidi pekee ndiyo silaha yetu kuu" - Jenerali Aleksandr Sakharovsky mkuu wa idaya ya kijasusi wa nje ndani ya K.G.B ( Kikao cha ndani baina ya G.R.U na K.G.B)

SEHEMU YA KWANZA:
HISTORIA FUPI YA UGAIDI KATIKA HISTORIA YA UTAMADUNI WA MWANADAMU.

Kwanza kabisa chimbuko la ugaidi ni la muda mrefu hata kabla ya Marekani, Uingereza, Urusi wala mataifa mengi ya leo kuwepo, . Miaka ya nyuma Ugaidi ulikuwa ni mlengo wa kisiasa, kifalsafa au kidini unaoamini katika kutumia vurugu, mauaji na fujo dhidi ya raia wasio na hatia au mali zao ili kuwafanya wakubaliane na matakwa yenu. Mfano mzuri tu ni kile kilichowahi kufanywa na wapiganaji wa kanisa la Katoliki maarufu kama THE KNIGHT TEMPLERS dhidi ya waumini wa dini ya Kiislamu na Kiyahudi mnamo karne ya kumi na moja wakati wa vita za kidini (Crusades).

Kwenye hiyo vita wapiganaji wa Kikatoliki waliwashinda Waislamu na kuwakamata wanawake na watoto na kuwachoma visu, kuwatesa na kuwachoma moto huku wakiimba "Tunakupenda Yesu". Dhana nzima ilikuwa siyo dini lakini ni kutuma ujumbe kwa Masultani wa Kiislamu kwamba msipokubaliana na Kanisa na mkiendelea kuwashambulia wakristo wanaokuja mashariki ya kati hasahasa Yerusalem ni lazima mtakufa kama wake zenu na watoto zenu. Japo kadiri miaka inavyoenda ugaidi ukazidi kubadilika hasa hasa baada ya kugunduliwa kwa Unga wa bunduki barani Ulaya. Hili liliwezesha kufanya ugaidi ambapo mtu anaweza kujilipua mwenyewe akiwa na mlengo fulani. Mfano baada ya Vita ya mwaka 1601 ambapo Uingereza ilipundua utawala wa Kanisa la Katoliki nchini mwake na kuanzisha Uanglikani, na kulikuwa na hekaya nzito za kuwazima wakatoliki na wafuasi wake. Mwaka 1605 mtu anayeitwa Guy Fawkes alitaka kujilipiua kwa baruti chini ya bunge la Uingereza lakini akashindwa.

Dhumuni la Guy Fawkes lilikuwa na mlengo wa kigaidi. Kuwatishia raia wa Uingereza kwamba hawawezi kushindana na Kanisa la Katoliki; maana angefanikiwa kuwaua Wabunge na Mawaziri basi utawala wa Katoliki ungerudi kwa kasi nchini Uingereza kwasababu raia wasingekuwa tena na Imani na serikali mpya hivyo kukubali kurudi kwa Papa ambaye aliaminiwa kuwa ni mwakilishi wa Mungu hapa duniani hivyo kumpinga isingewezekana kabisa.

SEHEMU YA PILI:
HISTROIA FUPI YA KUKUA KWA DHANA YA UGADI MNAMO KARNE YA 15 HADI 20.

Ikumbukwe kwamba kuanzia karne ya 15 hadi 19 kulikuwa na mabadiliko makubwa ya kifalsafa. Ambapo wengi hupenda kuuita wakati wa mnuruisho (Age of Enlightenment). Mataifa mengi yalianza kuachana na falsafa za kidini na falsafa za kifalme zisizokuwa na maana, mbele wala nyuma. wanadamu wakaanza kutumia ubongo wao kufikiri, walijiuliza maswali kama: Je, kuna Mungu? Je, Kwanini Mfalme atawale bila kuulizwa? Je, Kwanini nisipate haki zangu? Je, nikinyimwa haki zangu nifanyaje? Watu waliamini kwamba kila jawabu la mwanadamu linapatikana kwa kupitia ubongo na nguvu zake pekee. Na ni lazima kila mwanadamu aheshimiwe utu wake kwasababu tu ni mwanadamu.

Mfumo huu mpya wa kimapinduzi ya kifikra haukuwapendeza sana watawala wa Ulaya, pamoja na kanisa lililokuwa linanufaika kwa moja kwa moja na mfumo. Wafalme wakaanza kuwaua watu wote wanaoonekana wana fikra tofauti kidogo. Mfano mzuri mwanasayansi Galileo Galilee, alipokuwa anatafutwa na kanisa kwasababu aliamini tu dunia ni duara. Baada ya kuona haya yanafanyika suluhu ikawa ni kufanya mapinduzi ili kuwafanya wafalme na kanisa wawaogope na kuwaheshimu watu. Wanafalsafa kama Rousseau , John Locke, Hegel, Marx, Engels , Voltaire na nk waliamini kwamba mapinduzi pekee ndiyo yatakayoleta mabadiliko ya kweli. Kwa bahati mbaya watu walitumia ugaidi kuwafanya wafalme wawaheshimu watu hivyo kuleta demokrasia Ulaya.

Makundi ya wanamapinduzi wenye mlengo wa kigaidi waliua wafalme wao.
Mfano mzuri Ufaransa kundi la Kigaidi la Jacobins liliua Mfalme wao Luis , Uingereza matajiri na Puritans walinyonga mfalme wao Charles na Urusi walinyonga Nicolas. Hivyo ugaidi ulikuwepo tangu miaka ya nyuma na mlengo mkubwa ulikuwa ni kulazimisha kufanyika kwa matakwa ya kisiasa au kidini. Japo zamani ugaidi ulikuwa unafanywa na kikundi ambacho kina imani fulani, siku hizi hata mtu moja tu anweza kuwa gaidi na akafanya vitu mbali na mlengo wa kisiasa au kidini. Anaweza kufanya kwa dhumuni la kipesa, mfano mzuri Uharamia wa meli ni moja ya ugaidi dhidi ya raia na mali zao na mara nyingine kabisa ugaidi unaweza kufanywa na taifa kubwa kama njia ya kupigana vita na adui au kupenyeza maslahi yake ya kiuchumi katika eneo fulani.

SEHEMU YA TATU:
UGAIDI BAADA YA VITA KUU YA DUNIA , VITA BARIDI KUFIKIA LEO 1945-2016

Baada ya Vita ya pili ya dunia mataifa ya Marekani na Urusi ya Kisovieti yaliibuka kuwa yenye nguvu sana hapa duniani hivyo kufanya dunia kugawanywa katika kambi mbili. Wakati huu dunia ilishuhudia kukua kukua kwa teknolojia, mifumo ya kisiasa, mbinu za ujasusi, mifumo ya kisheria za kimataifa, muunganiko wa chumi za dunia na uwepo wa majeshi makubwa na yenye nguvu tofauti na miaka yoyote katika historia ya mwanadamu.

Ulikuwa ni Ulimwengu ambao taifa haliwezi kujitenga na mataifa ya duniani. Kwa bahati mbaya sana kukawa na kambi mbili kubwa duniani, Kambi ya Magharibi ikiongozwa na taifa la Marekani huku Kambi ya Mashariki ikiongozwa na taifa la Urusi ya Kisovieti. Kila kambi ilikuwa inataka kutawala dunia kisiasa na kiuchumi hivyo kuanza kuleta mnyukano mkali. Marekani anataka dunia huru ya kibepari, Urusi anataka dunia yenye utawala wa pamoja na Ukomunisti.

Kabla ya mwaka 1945 nchi zikiwa na mnyukano wa kisiasa zilikuwa zinamaliza mambo kwa kutumia nguvu ya kijeshi. Lakini baada ya Einstein kutuletea laana ya Nyuklia ambapo dunia ilishudia alichofanywa Japan kwenye visiwa vya Hiroshima na Nagasaki. Raisi wa Marekani Truman akajua kwamba njia pekee ya Kumaliza vita ni kutumia silaha nzito za maangamizi ili kummaliza adui haraka na kupunguza athari za vita upande wake: Kwasababu kama Marekani ingeamua kuwavamia wajapani kichwa kichwa wangeshinda lakini wangekufa wamarekani wengi sana.

Mwaka 1949 Urusi naye baada ya kuona atazidiwa kivita na Marekani akaamua kutengeneza Makombora ya nyuklia na kuyalipua hadharani. Ikumbukwe kwamba Marekani na Uingereza walikuwa na Mkakati wa kijeshi uitwao TOTALITY ambao Jenerali Eisenhower alipewa ausimamie. Kwa kifupi Winston Churchill aliwashauri Wamarekani walipue Urusi na nyuklia mara moja na vita uishe na Ukomunisti uwe historia, lakini baada ya kukuta Urusi ana nyuklia basi mpango ukasitishwa. Miaka imeenda Urusi na Marekani wanajitanua sana katika nyanja ya silaha za maangamizi kama silaha za kikemikali na kibaiolojia. Magonjwa kama Ndui, tetekuwanga, Sulua na hata Malaria sugu kutengenezwa ambapo mbu wa kawaida anaongezewa vitu kisha anapandikizwa sehemu.

SEHEMU YA NNE:
MBINU MPYA ZA UGAIDI ZATAMBULISHWA RASMI NA KUANZA KUTUMIKA DUNIANI.

Baada ya kuona kwamba Mrusi na Marekani hawawezi kupigana vita hata siku moja kwasababu vita ya Kinyuklia ya vingewaangamiza wote basi nchini Urusi K.G.B mwaka 1967 wakaona suluhu ni UGAIDI. Ikumbukwe kwamba kabla ya ugaidi walikuwa wanapigana kwa kupitia vivuli (Proxy War) ambapo Marekani anakuwa upande moja wa nchi fulani na Urusi anakuwa upande wa pili. Mfano Vita ya Korea mwaka 1950-1953 Marekani korea Kusini na Urusi Korea Kaskazini, Vita ya China ya 1945-1949 Urusi upande wa Wakomunisti na Marekani upande wa Mfalme wa China.

Lakini baada ya kuona vita hazizai matunda Mazuri na kuna hatari ya kupoteza wanajeshi wengi na kutupa pesa au kuweza kutokea vita baina yao wenyewe kama ilivyotokea pale CUBA mwaka 1962 baada ya Mrusi kupeleka makombora ya Kinyuklia kwenye Kisiwa cha Cuba ili kujibu mapigo ya Marekani kuweka Makombora aina ya JUPITER NA THOR nchini Uturuki kwenye mpaka wake na Urusi. Marekani na Urusi wote wakajifikiria na kuanza kujipanga upya. Hasahasa Urusi mwaka 1967 alipoteza pesa kibao na kupata hasara na madonda makubwa baada ya Israeli kuwatwanga waarabu na kulipua silaha zote ambazo Urusi alikuwa amewapa.

Mkurugenzi mpya wa Shirika la K.G.B Yuri Andropov aliwatafuta wataalamu wagundue njia mpya ambayo itawafanya wapigane na Marekani bila kwenda wao wenyewe wala kupata hasara kubwa. Walianzisha Ugaidi wa kidini ambapo ili kuendeleza adhma yao walianza kuwasomesha vijana wakiarabu waliooneka na uwezo wa kipekee. Wakaanzisha Chuo Cha Lumumba ambapo C.I.A wanasema ulikuwa ni mtambo wa kuzalisha magaidi na majasusi wa kikomunisti. Vijana walikuwa wanachukuliwa na wakienda mle ndani wanaaminishwa kwamba wanapigana kwa ajili ya taifa na Mungu lakini kumbe ni njama za wakomunisti kupeleka sera zao mbele. Naomba niseme wazi kabisa kwamba Uislamu siyo ugaidi lakini magaidi wengi wanatumia uislamu kuhalalisha Ugaidi.

SEHEMU YA TANO:
UGAIDI KATIKA DOLA LA URUSI YA KISOVIETI

Warusi walitumia mwanya wa ugomvi baina ya Israel na nchi za Kiarabu kutengeneza magaidi japo wao walijiita ni wapigania uhuru. Wasomi wengi wa kikundi cha P.L.O kuanzia Yasser Arafat walifundishwa Urusi na kurudishwa mashariki ya kati. Pia kuna PFPL (Popular Front For Palestinian Liberation) ambapo mbali na kupigana vita walikuwa na mbinu za kuteka ndege na kufanya uharibifu ili kuwafanya watu wa Mashariki waogope na kukubaliana na kuiacha palestina peke yake.

Moja ya magaidi hatari kabisa alikuwa anaitwa Wadie Haddad ambaye alifundishwa na K.G.B na mwaka 1970 akapewa jina la siri (Code-name) NATSIONALIST. Huyu jamaa alipenyezwa kwenye makundi ya Ukombozi ya Kipalestina na akawa na anapenyeza ajenda za Kirusi na kusambaza ugaidi. Anakumbukwa kwasababu alishawahi kuteka ndege tatu na kuzilipua. Mchezo wa kuteka ndege ukawa ndiyo unafanywa sana na P.L.O, K.G.B na G.R.U. Mara ya mwisho PFPL wanafanya utekaji wa ndege chini ya uratibu Haddad Wadie mwaka 1970 ambapo walimtuma gaidi wa kike kutoka Iraq anayeitwa Leila Khaleed kupeleka ndege Jordan lakini kwa bahati mbaya mle ndani ya ndege kulikuwa na jasusi la Mossad hivyo kuwathibiti vilivyo wakina Leila hadi kukamatwa.

Gaidi mwingine ambaye amefanya kazi na Urusi anaitwa CARLOS THE JACKAL na kwa jina halisi ni Illych Ramirez Sanches. Huyu jamaa ni mtu wa Venezuela lakini inasemekana mwaka 1966 alipelekwa CUBA na huko akapewa mafunzo na shirika la kijasusi la CUBA (DGI) na baada ya hapo akaenda kujiunga na chuo kikuu cha Lumumba nchini Urusi mwaka 1968. Lakini ukweli ni kwamba K.G.B ilitafuta sababu ya kumpeleka Carlos mashariki ya kati. Jamaa atakumbukwa kwa unyang'au wa kuwa fundi wa kutoroka na kujua sana kujificha. Mwaka 1975 alienda Ufaransa na majasusi wakatumwa kumkamata jamaa akawaua na kutoroka. Carlos alikuwa anatumiwa sana kufanya mauji na viongozi wa nchi mbali mbali duniani wenye mlengo wa kushoto.

Mwaka 1975 alifanya shambulio la Vienna nchini Austria ambapo viongozi wa nchi za OPEC walikutana wakiwepo mawaziri. Carlos akaingia na kuteka na kuu watu. Baada ya hapo waliteka watu kama sitini na kuwapandisha kwenye ndege na kuanza kuwazungusha nchi mbali mbali. Lakini muda wote huu Urusi ya Kisovieti alikuwa nyuma ya vivuli na akiwatumia hawa jamaa bila Marekani na wenzake kujua.

Taarifa hizi kuhusu mitandao ya kigaidi zilivuja baada ya majasusi kutoka Urusi na nchi za Warsaw Pact kuasi ni kupeleke taarifa kwamba Urusi ndiyo inahusika na magaidi hawa. Jenerali Ion Pacepa ambaye alikuwa nchini Romania na kuasi anasema kwamba Jenerali wa Kirusi kutoka K.G.B Alexandr Sakharovysky alisema msemo ambao nimeuweka hapo juu mwanzo wa hii habari kwamba katika dunia hii ambapo silaha za nyuklia zimefanya majeshi yakose umuhimu basi ugaidi ndiyo suluhu. Kwenye kitabu chake kinachoitwa Russian FootPrints kwamba Jenerali Alexandry ndiye aliyebuni mbinu ya kuteka na kulipua ndege.

Mbinu ya ugaidi ilifanikiwa sana kupeleka mambo ya Urusi na kambi ya kushoto mbele ambapo ilitumika vema nchini Vietnam kwenye vita ya mwaka 1965 hadi 1975 hadi kumfanya Marekani na wshirika wake kukimbia. Hochi Minh alifundishwa vizuri sana na K.G.B na hadi kuanzisha kundi linaloitwa VietCong ambao walikuwa wanapigana kwa kutumia mbinu za ugaidi. Raia wa vietnam waliogopa sana kuwapinga kwasababu kundi lilikuwa linaua wasaliti wa aina yoyote. Jamaa walijifanya raia wa kawaida na wakulima huku wanaenda kulipua sehemu yoyote ambayo wanajeshi wa Marekani wapo hata kama kuna raia. Mwishowe wamarekani walichanganyikiwa wakaanza kuua kila mtu wanayehisi hana makosa na huo ndiyo ulikuwa ni mpango wa K.G.B. Nchini Marekani ilionekana C.I.A wanawaua raia na kweli walikuwa wanawaua raia wasio na hatia, maandamano makubwa yalitokea na serikali pamoja najeshi la Marekani walikosa imani ya Ummah wa Wamarekani na mwishowe wakakimbia Vietnam.

ITAENDELEA.........................................

Mods naomba msiunganishe hili bandiko, maana mimi nimegusia Ugaidi katika Ujumla wake. Tunategemea kuongezea vitu vingine tofauti kidogo na mada ya ndugu Abubaro ambapo umezungumziwa Ugaidi na taifa la Marekani peke yake.
Tumeshauriana naye tuanzishe mada itakayozungumzia ugaidi kwa Ujumla.

CC: Abubaro , MSEZA MKULU , asigwa , eden kimario , Red Giant , Apollo , Bukyanagandi , Consigliere , big gift , Elungata , Dotworld , FisadiKuu
 
Katika ugaidi huwa naumia sana kuona mtu mweusi akijilipua kuua mwafrika mwenzake maskini.
Hebu pita na huku boko haram na alshababu. Mbona enzi za vita vya biafra, Kagera, Congo huko, Mozambique hata unita hatukuwahi kuona mtu mweusi akijilipua yaani afe sokoni na mama ntilie wapigadebe wamachinga na watafutaji wasio na kitu. Hebu pita na huku mkuu Malcom. Niliona picha ya mama mmoja mtu mweusi huko kano sokoni alivyolipuka mwenyewe kabla ya target ambapo alipanga kuua watu sokoni brainwashed boko haramu huyu. So sad aisee
 
Mkuu ugaidi Afrika ulitumiwa sana, Mfano mzuri tu:
Magaidi ya RENAMO yalipewa mafunzo na Majasusi ya Rhodesia wakisaidiwa na C.I.A, BOSS na M.I.6
Magaidi ya MPLA yalipewa mafunzo na C.I.A , MOSSAD,M.I.6 na BOSS (Shirika la kijasusi la makabulu)
Ukisoma jinsi haya makundi yalivyowafanya Waafrika wenzao utasikitika sana.
 
Mkuu zungumzia na huu wa kujitoa muhanga ambao Sasa unaingia kwa watu weusi barani kwetu
 
Documentary nzuri nasubili muendelezo kama ulivyo tuhaidi hapo
 
Tunayaangalia mambo haya kwa namna tofauiti sana tena sana......

Yote hapo kwangu mim i hayana uhalisia kabisa,yaani hayo yote ni mambo ya kupanga tu....

Kama kuna ugaidi basi ni ugaid wa namna moja tu ambao ni ugaidi wa kuwafanya wengine wakubaliane na kile ambacho hybrid human wameandaa kwaajili ya ulimwengu ujao.....

Namna ya kuwafanya watu wa kawaida wakubaliane nao ni kutengeneza matukio kama haya ambayo wewe umeyasiulia hapo juu,yaani waone ni reaity ili wakileta suluhu mkubali tu.....
 
Kwa hiyo mkuu na wewe unaamini kwamba kuna kundi la watu ndiyo linaongoza hii dunia yote?
Kwamba maisha yetu sisi yanaendeshwa kama mashine na kikundi fulani tu?
Hivyo basi wewe unataka kutuambia kuwa wanadamu hatujawahi kuwa huru katika maisha yetu?
Hakujawahi kuwepo na uhuru kwa maana ya uhuru mkuu,hata kwa Mungu hakuna uhuru.....

Kuna udanganyifu mkubwa sana unaoebndelea duniane eti tutakuja kuwa huru....

Kusema kuna kikundi cha watu kinachoratibu maisha ya kila mmoja ni kweli na siyo kweli maana wanaoratibu maisha haya siyo binadamu kwa asilimia 100 bali ni zaidi ya hapo.....

Kuna viumbe ambao wana uwezo mkubwa sana wa kifikra kuliko mimi na wewe,viumbe ambao wanajua kile kitu na hata namna binadamu alivyoumwa kwakuwa walikuwepo wakati binadamu anaumbwa.Viumbe ambao wanaijua dunia kwa kiwango cha kutisha kabisa,mbali sana na namna tunavyodhani tunaijua maana walikuwepo wakati ikiumbwa.....

Mkuu kwa kukushauri tu ni kwamba,chukua yote unayoyajua kuhusu kila kilichopo halafu yageuze kinyume chake,huo ndiyo ukweli wenyewe.....
 
Mkuu,
From what i see i that you have read too much of The Book of Enoch hence you have a hard time processing the reality.
I understand that you are speaking about The Watchers/The fallen angels/The Nephilim/ B'nai Elohim.
But i am sorry for you that you believe that they own and run this world and humanity is doomed to extinction.
Huwa napenda zaidi kujadili kwa lugha ambayo tunaifahamu vyema kuliko kutumia lugha za watru wengine maana ni tatizo kubwa sana....

Ningependa zaidi kama ungeandika kwa kiswahili maana sioni sababu yoyote ya maana kwa wewe kuandika Kiingereza kujibu post ya Kiswahili iliyoko kwenye forum ya Kitanzania inayotumiwa na Watanzania wengi.....

Ngoja niangalie ulichojibu....
And worse enough you believe that human beings since the dawn of time have been slave of the supernatural.
Hii umeitoa wapi mkuu?
Henceforth before the fall of man Adam and Eve were slaves of The Almighty God (Elohim, Yahweh, Jehovah);
Ninachokiona hapa unaandika unachokifikiria wewe ukidhani ndiyo mawazo yangu...

Ulipaswa kuniuliza nilikuwa nina maana gani kusema kuwa hakuna uhuru hata kwa Mungu,kusema hivyo sikumaanisha kuwa kutokuwa na uhuru ni kuwa watumwa....

Unanikumbusha jamaa yangu mmoja ambaye alikuwa akilazimika kuisifia CCM kwasababu alikuwa akidhania kuwa kuikosoa CCM ni kuisifia CHADEMA.....

Haya mawazo yako yanafanana na huyu jamaa,uhuru unaozungumzwa na wengi siyo uhuru unaouzungumza kwenye maana ya Free will,by the way,free will siyo freedom,weka akilini hiyo....
and after the fall they were bound to the servitude of The Devil (Lucifer, The fallen, Prince of lies) and his legions of demons.
Kwa context ya ulichokisema hapa uko sahihi.....
I don't mean to be rude but this type of thinking is very lame.
Hii ni aina yako wewe ya kufikiri,nakukumbusha hili maana umetoa kichwani mwako na unataka kunilisha maneno.....

Hii ni namna yako ya kufikiri mkuu....
At first this very thinking undermines the basic foundation of Free Will and henceforth it is a direct insult against God.
Yaani unasoma maandiko unayaelewa kinyume halafu unasema ni kosa la wandishi,hii ni kali kuliko....

Ni sawa na jamaa wanne wamesimama kando ya barabara,watatu wanaona gari linalopita barabarani halafu mmoja halioni,badala ya kufikiria kuwa inawezekana macho yake yana matatizo yeye anaanza kuwaambiwa wale jamaa ni waongo.....

Ni wapi na kwanini unadhani kuwa hiki ulichoandika hapa ndicho nilichomaanisha?
Secondly, your inclination asserts that there won't be a judgement day because human actions are controlled by demons.
Duuuh!! Wewe jamaa ni noma sana....

Nani kasema kwasababu matendo ya binadamu yanaongozwa na Shetani hivyo hakuna hukumu?

Biblia inasema kwamba Shetani ndiyo mungu wa ulimwengu huu,pia inasema kwamba matendo maovu yote Shetani ndiyo anahusika,je inakuwa inamaanisha kuwa wanadamu hawatakuwa kwenye hukumu kwasababu hii?

Hii umeitoa wapi?

Nikikuambia unaandika mawazo yako hapa unabisha,jitahidi sana kuuliza maswali badala ya kuwa unajijibu maswali yako mwenyewe maana unajiingiza kichakani.....
Here you mean that even if we commit sin, its never our fault.
No,no,no,no,no,nooo.Sijamaanisha hivi,sema wewe ndiyo umedhania hivi....

Usiniwekee maneno mdomoni,haya ni mawazo yako....
Thirdly, your inclination insults the Bible and undermines the basic principles you once believed in. Jesus said "I will set thee free, and thou shalt be free indeed" . Yet you say there is no freedom in God.
Bandiko lako lote limejaa mawazo yako halafu unataka eti yawe yangu,nimejikuta nacheka sana aisee.....

Jifunze kuuliza kile usichokielewa na siyo kutaka kujivika mawazo ya watu wengine ambao hata huwajui......
Yote tisa, hii mada ni ya siku nyingine.
Hii mada nina wasi wasi huiwezi maana unaonekana huna kawaida ya kuuliza kile wengine wanachokifikiria na badala yake unajijibu mwenyewe huku ukitaka yaonekane ni majibu ya wengine.....
Lakini kwa sasa tujikite kwenye Ugaidi ambao unaonekana kwa macho.
Hakuna ugaidi kwa maana uliyozungumzia matukio hapo juu....

Ugaidi ni kitu kisichokuwepo.Umeambiwa kuna ugaidi umeamini na kuchukua kama ilivyo,nani anamtishia nani na kwanini?
 
Uwe unaelewa wewe,
Mimi nimezungumzia ugaidi kama Kitenzi na siyo Ugaidi Nahau: Hivi ni vitu viwili tofauti sana.
Kitendo chochote kinachofanywa kwa nje ya sheria za vita kwa mijali ya kutishia raia ni Ugaidi, hapa lazima uelewe.
Ndiyo maana kama ungekuwa msomaji mzuri tokea hapo juu ungeona mapema kabisa kama nazungumzia ugaidi (vitendo).
Jitahidi kuelewa lugha katika muktadha wake.

Pili,
Neno Uhuru katika kamusi ya Kiswahili lina maanisha "kujikomboa, kujikwamua, Kufanya mambo yako bila kuingiliwa"
Neo Uhuru kinyume chake ni "Utumwa, Kifungo, kuingiliwa"
Unaposema kwa "Mungu hakuna Uhuru" ina maana kuwa ni kinyume chake.
Labda uniambie maana yako binafsi ya nini maana ya neno Uhuru.

Tatu,
Labda mimi ni mgumu kuelewa na nimekurupuka.
Lakini hao viumbe ambao walikuwepo tangu uumbaji wa binadamu ni wakina nani??
Na hao viumbe wanahusika vipi na Ugaidi???
Naomba unieleweshe ili tuwe na mada endelevu.
Mkuu huyu mdau huwa Kuna vitu anaamini lkn hayuko huru kuyazungumzia kwa kuogopa Labda atakuwa backfired na wahusika. Kiukweli dunia ya Sasa hakuna siri sana. Kama mimi nimesoma kitabu au nimeangalia documentary nitaweka mawazo humu mwenye uelewe zaidi ataweka record Sawa.
Mkuu Eiyer sema unaamini nini na ujue hapa tunajadili truths/perspectives ambazo sio lazima ziwe facts kwa sasa. Ila utaelewa baadae
 
Ndiyo maana nikasema kwamba.
Viumbe ambao wanadaiwa kuwepo zaidi ya binadamu ni malaika ambao Biblia inawaita wana wa Mungu.
Ukisoma The Torah kwa Kihebrania wanaitwa B'nai Elohim ambayo inaweka utofauti kabisa na binadamu. (Ha'adam)
Ukisoma The Book of Enoch ndiyo wanaitwa The Watchers ambao ni malaika waliopewa kazi ya kuwaangalia binadamu na dunia. Lakini kwenye Biblia inasemekana walizaa na binadamu wakatoa majitu au jamii ya Wanefili.

Tena kuna wasomi wengine wanasema kwamba mbali na malaika kuna vitu ambavyo Mungu hakuviumba kabisa.
Wanasema hakuna sehemu ambayo Mungu aliumba maji na hakuna sehemu alipoumba giza na kuna viumbe wengine kama mauti walikuwepo wakati wa uumbaji. Kuna mwana theolojia anaitwa Dake amefanya utafiti kwa kupitia tamaduni mbali mbali kwa zaidi ya miaka 30 na akaja na majibu yafuatayo japo mimi sikubaliani naye hata kidogo.

Dake anasema,
Maji yameumbwa na Mungu na ile kusema dunia ilikuwa ukimya tena utupu ilitokana na kuanguka kwa Lucifer na vita iliyotokea mbinguni. Anadai kwamba kulikuwa na dunia na wanadamu waliishi yeye anawaita (Pre-Adamites) ambao waliungana na Lucifer pamoja na malaika zake dhidi ya Mungu na Mungu akawagharikisha na dunia ikaharibika na kuwa ukiwa tena utupu. Anasema katika uumbaji wa mwanadamu malaika ndiyo waliokuwa wanafanya kazi kubwa ya kumtengeneza malaika kutoka kwenye udongo huku wakipewa maelekezo na Mungu. Huku akisema Biblia inaposema Mungu kwenye agano la kale huwa inamaanisha B'nai Elohim ambao ni Mungu.

Anakuja kuthibithisha hili kwa kusema Jacob alishindana na Mungu na kushinda,
Lakini alishindana na Malaika na kushinda na upande wa pili anasema Malaika walimtembelea Abraham lakini Biblia inasema kwamba Bwana alimuambia Sarah muda kama huu utakuwa na mtoto. Hivyo yeye anaseme Biblia imejaa mafumbo. Mkuu tafuta hiyo Makala inachangamsha fikra japo binafsi siiamini.

The Book of Enoch,
Kinadai kwamba mwanadamu alipewa huu utaalamu wote na hao malaika walioanguka.
Kuanzia kujiremba, silaha za kivita, ushirikina na uchawi ndiyo wameleta wao.
Wanasema haya mambo yalimuuzi Mungu ndiyo maana akaleta Gharika ya Nuhu ili kuwatoa katika miili ya kibinadamu.
Sasa wanaosoma haya mambo wanakuambia wanadamu ndiyo wanaongozwa na hawa viumbe mpaka leo hii.
Wengine wanasema hadi Aliens ndiyo hawa viumbe na ndiyo wanaongoza serikali kubwa hapa duniani.

Naye mkuu wetu Eiyer amekuja na nadharia yake kwamba kuna viumbe vina akili sana kuliko binadamu.
Vilikuwepo tangu uumbaji na hivyo basi hata ugaidi haupo kwasababu mwanadamu hajawahi kuwa huru kwasababu ya hawa viumbe. Japo mpaka sasa hajatutajia ni viumbe gani zaidi zaidi kushambulia kwamba hatujui bila kuleta ushahidi wowote wa hao viumbe.
Nimecheka sana leo watu wanaamini sana haya mambo hadi wanapoteza uhalisia wa dunia. Kila kitu kwao kinakuwa uongo kabisa, jamaa anakataa kabisa hakuna vitendo vya ugaidi.
Nakupata chief, ila Mimi huwa naamini Katika vitabu 66 vya bibilia kama source of all valid information kuhusu Mungu na Dunia.
Hivi vingine naamini lazma viwe na Coherence na hivyo vitabu 66 nje ya hapo kuamini nimefunga ila huwa nasoma kujua wengine wanaamini mini.

watu tumeumbwa na free will hapa panaua HOJA ya kuwa kuna kumbe njema yetunanarun Maisha yetu.

Nitapita hivyo vitabu nione pia ila ndio nasikia Leo . Dunia inakila sina ya wanaphilosophia ila wengine wanapijenyeza kwa lengo la kucontaminate brain zetu ili tusiamini chochote chema na kuacha wanadamu bila matumaini.

Ndio maana tunamuomba huyu mkuubatupe full perspective Yake ili tujue anataka kasema nini
 
Uwe unaelewa wewe,
Mimi nimezungumzia ugaidi kama Kitenzi na siyo Ugaidi Nahau: Hivi ni vitu viwili tofauti sana.
Kitendo chochote kinachofanywa kwa nje ya sheria za vita kwa mijali ya kutishia raia ni Ugaidi, hapa lazima uelewe.
Ndiyo maana kama ungekuwa msomaji mzuri tokea hapo juu ungeona mapema kabisa kama nazungumzia ugaidi (vitendo).
Jitahidi kuelewa lugha katika muktadha wake.
Hili la lugha tuliache maana halina faida yoyote hapa tukianza kuoneshana umwamba wa namna ya kujua lugha......
Pili,
Neno Uhuru katika kamusi ya Kiswahili lina maanisha "kujikomboa, kujikwamua, Kufanya mambo yako bila kuingiliwa"
Neo Uhuru kinyume chake ni "Utumwa, Kifungo, kuingiliwa"
Unaposema kwa "Mungu hakuna Uhuru" ina maana kuwa ni kinyume chake.
Labda uniambie maana yako binafsi ya nini maana ya neno Uhuru.
Kama unatumia nejo uhuru kwa muktadha wa Kiswahili uko sahihi lakini kila mtu,kundi na falsafa fulani fulani wana maana yao ya uhuru....

Kuna watu,kwa mfano,wanaamini na kujua kuwa amani [peace] ni kutokuwepo watu wanaowapinga wao,hawa ukiwapelekea maana yako ya neno amani kutoka katika kamusi ya kwamba kutokuwepo kwa mauaji au watu kuwa na hofu ya chochote hawatakuelewa....

Uhuru,kwa maana ya kwenye maandiko matakatifu,nijuavyo mimi,ni ile hali ya kuishi katika maelekezo ya Mungu na Mungu kukupa ulinze wake ambao utakufanya uwe salama,lakini kitendo cha kufuata maelekezo hayo siyo lazima bali ni hiyari,huu ndiyo uhuru ninaouzungumzia mimi....

Sasa basi,ni kwanini nilisema kwa Mungu hakuna uhuru?

Nilisema hivyo nikimaanisha maana nzima ya neno uhuru katika lugha ya Kiswahili,yaani kama ulivyosema hapo juu.Kwa Mungu hakuna ruhusa ya kufanya utakalo,huna ruhusa hii na hii ni kinyume cha uhuru kwa maana uliyosema hapo juu.....

Sijui kama umenielewa....
Tatu,
Labda mimi ni mgumu kuelewa na nimekurupuka.
Lakini hao viumbe ambao walikuwepo tangu uumbaji wa binadamu ni wakina nani??
Malaika waasi....
Na hao viumbe wanahusika vipi na Ugaidi???
Naomba unieleweshe ili tuwe na mada endelevu.
Maelezo marefu kidogo yanahitajika hapa,lakini "from the scratch" kuna movement moja kuu ambayo ni "restoration"....

Kurejesha dunia ambayo ilikuwepo mwanzo kabla ya mwanadamu kuanguka dhambini.Mungu ana njia yake ya kuirudisha dunia hiyo na upande wa Shetani naye ana mipango yake.

Ijulikane kwamba pande hizi mbili zipo kwenye vita kali kabisa ambayo mimi na wewe hatuijui vizuri tu,tunachukulia kawaida kawaida,yaani simple....

Shetani alijua mipango ya Mungu tangu mwanzo,alijua ni namna ipi atamuokoa mwanadamu kutoka dhambini,first atempt ya Shetani kuzuia Mungu asimuokoe mwanadamu ni kitendo cha yeye na malaika wake kutaka kuvuruga gene ya mwanadamu ili mwokozi asizaliwe wakati ule wa Nephilims,Shetani alijua kuwa Mungu alipanga kumuokoa mwanadamu kwa kupitia yeye Mungu kuzaliwa na mwanadamu 100% hivyo alitaka kuliondoa hilo akashindwa baada ya Mungu kuingilia kati kwa kuleta gharika....

Next attempt ni kwa kumtumia Herode wakati Yesu alipokuwa amezaliwa,akashindwa pia na kilichotokea wote tunakijua....

Shetani alizuia yote haya kwasababu alijua kuwa kwa kufanya hivyo Mungu atafanikiwa kurejesha kile kilichopotea kwa kusababishwa na Shetani huyo huyo pale Eden....

Baada ya kushindwa Shetani aliweka mikakati mingi sana ya kupambana na watu wa Mungu,kwasababu Shetani na malaika waasi walikuwepo wakati Mungu anaumba dunia na mwanadamu kwa ujumla wake walijua kila kitu ambacho kilifanyika...

Shetani alileta kitu kinachoitwa elimu,elimu ambayo kimsingi inaondoa kabisa uwezekano wa wanaoipata kujua uwepo na ukuu wa Mungu.Akaleta maarifa mengi sana ambayo nadhani nitajaza sever za JF kwa kuanza kuyaelezea hapa,lakini kikubwa ni kwamba alitengeneza dini fake ili kukabiliana na watu wa Mungu ambao watakuwa wakimfuata kwa uaminifu.....

Ikumbukwe kuwa,lengo la Shetabni ni kumtawala mwanadamu na kumfanya awe mfuasi wake ili afuate maelekezo yake na kuirejesha dunia ya kwanza kwa namna na mpango yake,ili watu wote waweze kufuata atakacho alitengeneza njia za hiyari na lazima,hiyari ni dini zake na lazima ni kwa kutumia vitisho na hapa ndipo tunakutana na vikundi vya kigaidi....

Mataifa yote duniani yana mpango wa kuifanya dunia kuwa mahali salam kwa kuleta dini na serikali moja chini ya kiongozi mmoja,jambo hili linatendeka kwa hiyari na lazima.Kwa kutumia elimu aliyowapa "watu wake" wameweza kujaribu ali ya hewa na kufanya mvua zisiwepo na kufanya pia uoto wa asili usiwepo,magonjwa fake kama Ukimwi,matukio ya uharibifu fake kama Tsunami,vikundi vya kigaidi na mengine...

Hayo yote,kwakuwa wao ndiyo waliyoyatengeneza kuna siku atakuja "mtu" mmopja na kuyaondoa na mtu huyo ataonekana kama amekuja kuwaokoa wanadamu na kwa kufanya hivyo kila mwanadamu atamkubali isipokuwa wale tu wachunguzi wa maandiko na mambo yanayotokea hapa duniani,kwa maana hii vikundi vya kigaidi lengo lake ni hili na siyo jingine....

Nimejaribu kudonoa donoa na sijui kama utaweza kuunganisha dots,lakini ni maelezo marefu sana hadi kuweza kuyaona haya kwa uwazi unaopaswa kuwa.Naweza kuandika maelezo mengi sana tena kwa siku kadhaa,lakini natumai kwa kudonoa donoa huku utakuwa umeelewa point yangu ya msingi.....
 
Ndiyo maana nikasema kwamba.
Viumbe ambao wanadaiwa kuwepo zaidi ya binadamu ni malaika ambao Biblia inawaita wana wa Mungu.
Ukisoma The Torah kwa Kihebrania wanaitwa B'nai Elohim ambayo inaweka utofauti kabisa na binadamu. (Ha'adam)
Ukisoma The Book of Enoch ndiyo wanaitwa The Watchers ambao ni malaika waliopewa kazi ya kuwaangalia binadamu na dunia. Lakini kwenye Biblia inasemekana walizaa na binadamu wakatoa majitu au jamii ya Wanefili.

Tena kuna wasomi wengine wanasema kwamba mbali na malaika kuna vitu ambavyo Mungu hakuviumba kabisa.
Wanasema hakuna sehemu ambayo Mungu aliumba maji na hakuna sehemu alipoumba giza na kuna viumbe wengine kama mauti walikuwepo wakati wa uumbaji. Kuna mwana theolojia anaitwa Dake amefanya utafiti kwa kupitia tamaduni mbali mbali kwa zaidi ya miaka 30 na akaja na majibu yafuatayo japo mimi sikubaliani naye hata kidogo.
Mungu aliumba maji,hili mbona liko wazi kabisa?
Dake anasema,
Maji yameumbwa na Mungu na ile kusema dunia ilikuwa ukimya tena utupu ilitokana na kuanguka kwa Lucifer na vita iliyotokea mbinguni. Anadai kwamba kulikuwa na dunia na wanadamu waliishi yeye anawaita (Pre-Adamites) ambao waliungana na Lucifer pamoja na malaika zake dhidi ya Mungu na Mungu akawagharikisha na dunia ikaharibika na kuwa ukiwa tena utupu. Anasema katika uumbaji wa mwanadamu malaika ndiyo waliokuwa wanafanya kazi kubwa ya kumtengeneza malaika kutoka kwenye udongo huku wakipewa maelekezo na Mungu. Huku akisema Biblia inaposema Mungu kwenye agano la kale huwa inamaanisha B'nai Elohim ambao ni Mungu.
Hii ni dhana yake ambayo haina back up ya Biblia,pia kuna dhana nyingine ambayo inasema kuwa Mungu aliumba wanawake wawili,Lilith na Eve,Eve aliumbwa baadaye baada ya Lilith kukataa kuwa chini ya Adam,hii nayo ni dhana ambayo haina back up ya Biblia....

Hilo la Malaika kumsaidia Mungu linataka kuendana na dhana ya Jehovah Witness ambao wao wanadai kwamba hiyo kazi aliifanya Yesu baada ya Mungu kumuumba kwanza,again,dhana hii nayo haina back up ya Biblia.....
Anakuja kuthibithisha hili kwa kusema Jacob alishindana na Mungu na kushinda,
Lakini alishindana na Malaika na kushinda na upande wa pili anasema Malaika walimtembelea Abraham lakini Biblia inasema kwamba Bwana alimuambia Sarah muda kama huu utakuwa na mtoto. Hivyo yeye anaseme Biblia imejaa mafumbo. Mkuu tafuta hiyo Makala inachangamsha fikra japo binafsi siiamini.
Kwenye ishu ya Jacob,naweza kusema ni jambo lisilowezekana Jacob amshinde Mungu,sijui alipambana na nani lakini ni vigumu kusema tu kuwa alikuwa ni Mungu....

Kwa Ibrahimu maandiko hayawataji wale ni akina nani wakati wapo kwa Ibrahimu,maandiko yalikuwa yanasema "Bwana" akamwambia Sara,lakini wakati maandiko yanasema Bwana ni wakati wale "watu" walipokuwa wakizungumza,lakini "watu" hao ndiyo waliondoka kuelekea Sodoma na Gomorah ambako walitajwa kuwa ni malaika,so naweza kusema kuwa malaika anapoleta taarifa ni Mungu kaleta,siyo mbaya kusema Bwana kasema pale ambapo malaika anaposema......
The Book of Enoch,
Kinadai kwamba mwanadamu alipewa huu utaalamu wote na hao malaika walioanguka.
Kuanzia kujiremba, silaha za kivita, ushirikina na uchawi ndiyo wameleta wao.
Wanasema haya mambo yalimuuzi Mungu ndiyo maana akaleta Gharika ya Nuhu ili kuwatoa katika miili ya kibinadamu.
Sasa wanaosoma haya mambo wanakuambia wanadamu ndiyo wanaongozwa na hawa viumbe mpaka leo hii.
Wengine wanasema hadi Aliens ndiyo hawa viumbe na ndiyo wanaongoza serikali kubwa hapa duniani.
Kimsingi kitabu cha Enock hakipingani na Biblia kinazungumza mambo haya kwa uwazi mkubwa sana.Kitabu hiki kilizuiwa kusomwa na watu na wale ambao hawakutaka kabisa wengine waelezwe ukweli juu ya mambo haya....

Kitabu hiki ndiyo kinawataja malaika hawa kwa majina,malaika waasi.Kinaeleza hadi kazi zao.Kitabu hiki kiirejewa hata na Yuda,hii inamaana kwamba kilisomwa na wanafunzi wa Yesu pia.....

Kuna vitabu vingine ambavyo ni vizuri lakini vimepigwa ban,The Book of Jasher,The Book Of the Giant na The Book Of The Dead,hivi vina mambo madogo ya kweli na mengine ya uongo,lakini ni vitabu vizuri sana kuvisoma.....
Naye mkuu wetu Eiyer amekuja na nadharia yake kwamba kuna viumbe vina akili sana kuliko binadamu.
Vilikuwepo tangu uumbaji na hivyo basi hata ugaidi haupo kwasababu mwanadamu hajawahi kuwa huru kwasababu ya hawa viumbe. Japo mpaka sasa hajatutajia ni viumbe gani zaidi zaidi kushambulia kwamba hatujui bila kuleta ushahidi wowote wa hao viumbe.
Nimecheka sana leo watu wanaamini sana haya mambo hadi wanapoteza uhalisia wa dunia. Kila kitu kwao kinakuwa uongo kabisa, jamaa anakataa kabisa hakuna vitendo vya ugaidi.
Kucheka siyo jambo baya,najua ni kwanini unacheka,hawa watu ni mafundi sana na ndiyo maana unacheka sana.BNi mambo ambayo "hayaingii akilini kabisa" lakini bahati mbaya sana ndiyo ukweli wenyewe....

Kusema kwangu hakuna ugaidi nilikuwa namaanisha kwa maana ya ugaidi inayosemwa na watu na siyo kwamba hakuna ugaidi kwa maana ya ugaidi kwasababu hata misheni za hawa "The Watchers" ni ugaidi tosha.....

Natumai umenipata angalau kidogo.....
 
Ndiyo maana nikasema kwamba.
Viumbe ambao wanadaiwa kuwepo zaidi ya binadamu ni malaika ambao Biblia inawaita wana wa Mungu.
Ukisoma The Torah kwa Kihebrania wanaitwa B'nai Elohim ambayo inaweka utofauti kabisa na binadamu. (Ha'adam)
Ukisoma The Book of Enoch ndiyo wanaitwa The Watchers ambao ni malaika waliopewa kazi ya kuwaangalia binadamu na dunia. Lakini kwenye Biblia inasemekana walizaa na binadamu wakatoa majitu au jamii ya Wanefili.

Tena kuna wasomi wengine wanasema kwamba mbali na malaika kuna vitu ambavyo Mungu hakuviumba kabisa.
Wanasema hakuna sehemu ambayo Mungu aliumba maji na hakuna sehemu alipoumba giza na kuna viumbe wengine kama mauti walikuwepo wakati wa uumbaji. Kuna mwana theolojia anaitwa Dake amefanya utafiti kwa kupitia tamaduni mbali mbali kwa zaidi ya miaka 30 na akaja na majibu yafuatayo japo mimi sikubaliani naye hata kidogo.

Dake anasema,
Maji yameumbwa na Mungu na ile kusema dunia ilikuwa ukimya tena utupu ilitokana na kuanguka kwa Lucifer na vita iliyotokea mbinguni. Anadai kwamba kulikuwa na dunia na wanadamu waliishi yeye anawaita (Pre-Adamites) ambao waliungana na Lucifer pamoja na malaika zake dhidi ya Mungu na Mungu akawagharikisha na dunia ikaharibika na kuwa ukiwa tena utupu. Anasema katika uumbaji wa mwanadamu malaika ndiyo waliokuwa wanafanya kazi kubwa ya kumtengeneza malaika kutoka kwenye udongo huku wakipewa maelekezo na Mungu. Huku akisema Biblia inaposema Mungu kwenye agano la kale huwa inamaanisha B'nai Elohim ambao ni Mungu.

Anakuja kuthibithisha hili kwa kusema Jacob alishindana na Mungu na kushinda,
Lakini alishindana na Malaika na kushinda na upande wa pili anasema Malaika walimtembelea Abraham lakini Biblia inasema kwamba Bwana alimuambia Sarah muda kama huu utakuwa na mtoto. Hivyo yeye anaseme Biblia imejaa mafumbo. Mkuu tafuta hiyo Makala inachangamsha fikra japo binafsi siiamini.

The Book of Enoch,
Kinadai kwamba mwanadamu alipewa huu utaalamu wote na hao malaika walioanguka.
Kuanzia kujiremba, silaha za kivita, ushirikina na uchawi ndiyo wameleta wao.
Wanasema haya mambo yalimuuzi Mungu ndiyo maana akaleta Gharika ya Nuhu ili kuwatoa katika miili ya kibinadamu.
Sasa wanaosoma haya mambo wanakuambia wanadamu ndiyo wanaongozwa na hawa viumbe mpaka leo hii.
Wengine wanasema hadi Aliens ndiyo hawa viumbe na ndiyo wanaongoza serikali kubwa hapa duniani.

Naye mkuu wetu Eiyer amekuja na nadharia yake kwamba kuna viumbe vina akili sana kuliko binadamu.
Vilikuwepo tangu uumbaji na hivyo basi hata ugaidi haupo kwasababu mwanadamu hajawahi kuwa huru kwasababu ya hawa viumbe. Japo mpaka sasa hajatutajia ni viumbe gani zaidi zaidi kushambulia kwamba hatujui bila kuleta ushahidi wowote wa hao viumbe.
Nimecheka sana leo watu wanaamini sana haya mambo hadi wanapoteza uhalisia wa dunia. Kila kitu kwao kinakuwa uongo kabisa, jamaa anakataa kabisa hakuna vitendo vya ugaidi.
leo nimekuelewa ulimaanisha nini baada ya mkuu kufunguka
 
Back
Top Bottom