Ufutaji uchaguzi Zanzibar, nani nyuma ya pazia?

Ufutaji uchaguzi Zanzibar, nani nyuma ya pazia?

simplemind

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2009
Posts
16,788
Reaction score
9,720
1.Mwenyekiti ZEC hana maamlaka ya kufuta uchaguzi Zanzibar.

2.Katika hali ya kawaida, siyo polisi wala JWTZ wanayo maamlaka kuzuia ZEC kutimiza majukumu.

Swali, nani yupo nyuma ya pazia ufutaji uchaguzi Zanzibar?
 
Zanzibar inaweza ingia kwenye historia duniani kama nchi pekee ambayo badala ya mgombea kulalamika kuwa uchaguzi haukuwa wa huru na haki, mwenyekiti wa tume ndio analalamikia matokeo. MAAJABU YA MUSA
 
Aliye nyuma ya pazia ni kushindwa kwa ccm Zanzibar. Kitakachofuata ni kuwakamata viongozi wa Cuf, kurudia uchaguzi huku wakiingiza janjaweed wengi, kumtangaza shein ameshinda na kumuapisha fasta.
 
Mungu anatuvumilia sana watanzania. Ila ipo siku yanayotokea kwa wenzetu yatahamia kwetu. Kuna miungu watu hapa tz wanaloamua liwe wanahakikisha linakuwa. Tulipofikia kubaya
 
Hata kama sio mwanasheria mbona nyingi ya sababu zilizotolewa na ZEC zina uwezo pia wa kuathiri uchaguzi wa wabunge na Rais wa Jamhuri?

Ukisema kulikuwa na wapiga kura hewa, nani kathibitisha kuwa hawa walipiga tu kwa Rais wa Zanzibar na Wawakilishi? Mpiga kura hewa si aliingia mara moja kuwapigia kura wote?

Jamani hebu tuwe na huruma kwa nchi yetu na watu wake! Hili linaweza kutupeleka pabaya. Tulishasifiwa kwa uchaguzi mzuri na wenye amani. Sasa huu ni ulevi gani? Hivi kuna watu wa kutoa ushauri sahihi kabla ya kufanya maamuzi kama haya?
 
Naomba TUWEKE Usahihi Ktk. Hilo Sio ZEC IMEFUTA UCHAGUZI!! Kilichofutwa Ni MATOKEO Ya UCHAGUZI, Ambao Umeshafanyika, Kura Zimehesabiwa, MATOKEO Yametolewa Na KUTANGAZWA BAADHI Ya Majimbo!!!! Hili Limedhihirisha Ile Kauli " HATUTOI NCHI KWA VIKARATASI " Ndio Tunachokiona Zanzibar!!!
 
Mkiambiwa TUME za UCHAGUZI NEC & ZEC ni sio HURU, ni vyombo vya CCM watu hawaelewi...!!!

Mungu anaonyesha wazi sasa...Mwenyekiti wa ZEC hawezi FUTA UCHAGUZI Mkuu MWENYEWE KAMWE... hana mamlaka hayo...!!! Ni Jukumu la WAJUMBE WOTE WA TUME KUKAA na KUAMUA...!!!

Mwenyekiti wa ZEC kapewa AMRI toka kwa Wakuu, kuona CCM imeshindwa vibaya Zanzibar, AFUTE MATOKEO YOOOOOOTE...!!! Hii ajabu ya maajabu..!! 😨😨😨😨
 
Mkuki kwa nguruwe mtamu. Let it be fair uchaguzi urudiwe pote bara na visiwani.
 
Pasco ukipata nafasi tafadhali njoo useme lolote kuhusu 'karma' .
Hivi ni kweli Zanzibar hasa kwa wenye mamaka hil itapita hivi hivi bila kuwa na consequences zozote?
Yaani wazanzibar wamchague rais wao alafu wababe wabadili mambo kirahisi rahisi tuu!
 
Last edited by a moderator:
Tanzania tumeingizwa na viongozi waroho kwenye AIBU ya karne, wanamhubiri Mwl Nyerere lakini wanatenda tofauti, dah nchi yangu sijui inaelekea wapi, Hii ni nchi yetu sote na sio ya wachache jamani
 
Mkiambiwa TUME za UCHAGUZI NEC & ZEC ni sio HURU, ni vyombo vya CCM watu hawaelewi...!!!

Mungu anaonyesha wazi sasa...Mwenyekiti wa ZEC hawezi FUTA UCHAGUZI Mkuu MWENYEWE KAMWE... hana mamlaka hayo...!!! Ni Jukumu la WAJUMBE WOTE WA TUME KUKAA na KUAMUA...!!!

Mwenyekiti wa ZEC kapewa AMRI toka kwa Wakuu, kuona CCM imeshindwa vibaya Zanzibar, AFUTE MATOKEO YOOOOOOTE...!!! Hii ajabu ya maajabu..!! 😨😨😨😨

Mungu anawapiga upofu, wanachi tujue tunaishi nchi ya namna gani
 
Uovu uliotuzunguka unatisha. Tuimarishe dua na maombi zaidi.
 
Zanzibar inaweza ingia kwenye historia duniani kama nchi pekee ambayo badala ya mgombea kulalamika kuwa uchaguzi haukuwa wa huru na haki, mwenyekiti wa tume ndio analalamikia matokeo. MAAJABU YA MUSA

Asante! kuingia kwenye historia haitoshi labda kwenye yale maajabu ya dunia(hii ni aibu)
 
Pasco ukipata nafasi tafadhali njoo useme lolote kuhusu 'karma' .
Hivi ni kweli Zanzibar hasa kwa wenye mamaka hil itapita hivi hivi bila kuwa na consequences zozote?
Yaani wazanzibar wamchague rais wao alafu wababe wabadili mambo kirahisi rahisi tuu!
At last, it's done!.
RIP mhusika mkuu wa karma hii!
P
 
Haijalishi ni nani, wenyewe Wazanzibari wameshafanya maridhiano wanajipanga uchaguzi mwengine.

Tena upinzani wa Zanzibar sasa wameingia kiakili huku bara, wanavitumia vyama vya upinzani vya huku kuidai Zanzibar yenye mamlaka kamili.
 
Back
Top Bottom