Mimi ni mmoja kati ya watu wanaokerwa sana na tabia za makonda kunyanyasa wanafunzi hasa wa jinsia ya kike. Kuna wakati fulani nilitembelea KENYA na kushangaa kutoliona tatizo hili. Mwanzoni nilidhani shule zote zina mabasi ya wanafunzi lakini nikagundua kuwa ni chache tu zenye mabasi, ila nauli ni sawa kwa wakubwa na wadogo.
Naona ufumbuzi wa tatizo ni kuweka viwango sawa vya nauli kati ya wakubwa na wadogo kama ilivyo kwenye huduma zingine kama vile vyakula, mavazi, malazi n.k. Tukifanya hivi, naamini wanafunzi watakimbiliwa kama wafalme na kama kutakuwa na unyanyasaji itakuwa ni kwa wakubwa tu ambao wana uwezo wa kujitetea.
Nawasilisha hoja kwenu wana JF