Ufumbuzi wa tatizo la wanafunzi kunyanyaswa na Makonda wa Daladala

Aalim

Member
Jan 17, 2011
36
4
Mimi ni mmoja kati ya watu wanaokerwa sana na tabia za makonda kunyanyasa wanafunzi hasa wa jinsia ya kike. Kuna wakati fulani nilitembelea KENYA na kushangaa kutoliona tatizo hili. Mwanzoni nilidhani shule zote zina mabasi ya wanafunzi lakini nikagundua kuwa ni chache tu zenye mabasi, ila nauli ni sawa kwa wakubwa na wadogo.

Naona ufumbuzi wa tatizo ni kuweka viwango sawa vya nauli kati ya wakubwa na wadogo kama ilivyo kwenye huduma zingine kama vile vyakula, mavazi, malazi n.k. Tukifanya hivi, naamini wanafunzi watakimbiliwa kama wafalme na kama kutakuwa na unyanyasaji itakuwa ni kwa wakubwa tu ambao wana uwezo wa kujitetea.

Nawasilisha hoja kwenu wana JF
 
Mkuu naona kama vile pendekezo lako limekaa ki maslahi zaidi bila kuangalia hali zetu duni za maisha.Naamini huu utakuwa ufumbuzi wa kufanya watoto wa wasikini wasiende shule kwa kukosa nauli.
Maoni yangu daladala kutokuwa na konda,yaani gari linakuwa na dereva na mashine ya kutumbukiza pesa au kusoma kadi,hii itakuwa ni suluhu kwa wanafunzi na hata walemavu na wagonjwa.Maana suala kero ya makonda sio kwa kwanafunzi hata kwa watu wazima ulisha kuwa tandika mida ya jioni unataka kwenda tabata kama ni mgonjwa au mlemavu utakubidi utafute utaratibu mwingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom