Ufugaji wa Nguruwe: Fahamu faida, hasara na mbinu bora za ufugaji

Hapana sikufanikiwa kiongozi eneo nililotarget changamoto ilikuwa lina wakazi wengi wa dini ya ndugu zetu hivyo kufanya project kama hiyo ni ngumu kwa ushauri wa wazoeafu
Pole sana mkuu,
Kwahiyo umefuga kuku ama ulibadili kabisa mawazo mkuu?
 
Nilibadili mawazo nikaanza kilimo cha karanga huko mpanda na April natarajia kununua japo ekari mbili hapa Mlandizi nianze bustani mkuu
 
Namtafuta sana huyo jamaa nikae nae tuongee mana ndo naanza mradi wang

Mkuu ulimpata huyu jamaa anayefugia mikese? Ninataka kuanzisha mradi wa namna hii maeneo ya mikese ningependa kujua kuhusu upatikanaji wa mashamba (maana nitachanganya na kilimo cha mazao ya bustani), naomba unipe hints juu ya hili au niunganishe na jamaa.
 
Habari za jioni wanajanvi kwa uzoefu nilionao na utaalamu wangu kuhusu nguruwe naweza kukushauri hvi
Kwanza inabid ujue tabia za nguruwe anapenda au anahitaji nini ili akue vizuri ,
Tambua kwamba nguruwe wakiwa wadogo uhitaji joto kiasi jopo si kali sana na hata wakikua baada ya mwezi mmoja huwa hawaitaji joto sana ,ili kupunguza joto bandani inabid ufanye haya kupunguza idadi ya nguruwe yani wawe wachache au uwaweke kwenye chumba kikubwa,
Kama hilo ni tatizo tofautisha ujenzi wa banda yani kulingan na umri wa nguruwe mfano banda la nguruwe waliozaa na weners liwe tofauti na wale wanotaka kupandwa,wenye mimba, wakuchinja na nk,kama kuna mtu aliwahi kwenda Tandan farm Mkuranga ndo mwanzilishi wa pale kwa hiyo naushaid ndo maana tukafikisha 1800 pigs with 400 sows,NB si lazima mabanda yawe kama ya Tandan
 
wapendwa naomba radhi kwanza kwa wote walionipigia simu wakitaka tujadili zaidi mradi huu, kutokana na sababu zilizokua nje ya uwezo wangu imekua ngumu mno kufanya ushirika kwenye mradi huu kama nilivyoomba hapo mwanzo juu. sasa hivi ninanaendelea na ujenzi wa banda hapa nyumbani wa kuweka nguruwe watatu plan yangu nichukue jike wawili na dume mmoja mungu akijalia mpka ijumaa nitakua namaliza ujenzi wa banda, ninajenga mwenyewe banda la miti kwa kuwa ni rahisi zaidi kwangu nitawatumia picha na nitawapa mrejesho nikimaliza ujenzi.
 
Mkuu na
Fika pale tegeta kuna mama mfanyabiashara maarufu anashamba kubwa la nguruwe na ni muuzaji mkubwa kwenye mabucha mbalimbali jijini. Ulizia kwa DC Mama Fatuma Joseph kimario utapelekwa, ni maarufu sana maeneo hayo hata mtoto mdogo atakuelekeza.
Mkuu naomba kukuuliza ni tegeta sehemu gani tegeta nyuki au tegeta kwa ndevu?
 
mimi ninavo vitoto lakini naona vinaumizana mikia mpka inatoa damu kabis,,anyejua shida ni nini au niwape dawagani
 
View attachment 324772

- Nguruwe watoto 20 @ 20000 = 400000
- Banda la mabanzi=1,000,000
- Chakula = 1,000,000
- Dawa= 200000

After 1yr: Nguruwe 20 watazaa vitoto kama 160,utachakuwa vitoto jike 100,
mama zao wote watauzwa, huku shambani kwetu nguruwe
mkubwa ni Tsh 200,000 tu, utapata 4,000,000.

After 2yrs: Nguruwe 100 wanaweza kuzaa 700. Kati ya 700 chagua majike 500,(unaweza kuuza watoto dume ukanunua jike).

Year 3: Nguruwe 500 watazaa watoto 3500, chagua watoto 1500 tu
Kutoka hapo unamentein Number 1500, kila mwaka unaweza kuuza
watoto zaidi ya 3000, na nguruwe wakubwa 1500.
1500*200000= Tsh 300,000,000/= kwa mwaka
Nusu ya hiyo pesa ni gharama zingine, unabaki na 150mil.
Welcome to the club

Kabla hujajitumbukiza kaone mifano, au nenda sokoine ukaonane na wataalamu.

Kila mwaka nalima Mahindi, alizeti, maboga ekari 30 kwa ajili ya chakula cha nguruwe tu.

Nakupenda saana mpwa..
Wewe unapatikana mkoa gan?








==========

USHUHUDA

======================================================
 
Back
Top Bottom