Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Ni njia bora sana maana ukimhasi inamaana unawanyima wenzako fursa yakupata mbegu.

..kaka kuna mabeberu wengine wana vurugu mpaka inakuwa fedheha kama kuna kina mama au watoto wa kike karibu na boma la mbuzi. unaweza kukuta beberu siku nzima mashine iko nje, mayowe mtindo mmoja, na linakimbiza mbuzi jike kila mahali.
 
Kwahiyo mbuzi wako walishughulikiwa barabara but uzi mzuri nitakucheki unipe ma ujanja
 
Karibu Mzee japo kanga ni mayai ikiwa utahitaji kutotolesha yanapatikana
Mimi sijui nafeli wapi nilinunua kanga wanne. Ilifika hatua hawarudi ndani. Watatu walitokomea kusikojulikana.... Nipe uzoefu mwenzangu ulifanikiwaje?
 
Boss mara nyingi kanga wa kununua wanakuaga watata Sana kuzoea mazingira labda kama Una uzio, me Nina uzio so wanashinda ndani na wanataga Hawa ndege askwambie mtu aisee nilichofanya ni nmewakata mbawa zao Kwa kutumia mkasi ili zisiote tena wamezoea na wanalala na kutagia ndani
Mimi sijui nafeli wapi nilinunua kanga wanne. Ilifika hatua hawarudi ndani. Watatu walitokomea kusikojulikana.... Nipe uzoefu mwenzangu ulifanikiwaje?
 
..kaka kuna mabeberu wengine wana vurugu mpaka inakuwa fedheha kama kuna kina mama au watoto wa kike karibu na boma la mbuzi. unaweza kukuta beberu siku nzima mashine iko nje, mayowe mtindo mmoja, na linakimbiza mbuzi jike kila mahali.
Huyo sasa ndio Super charger kama isiolo anafaa sana huyu
 
Weekend ya usafi Mbuzi wangu wa maziwa huyu na anasifa ya kuzaa mapacha kwasasa ndo Kwanza ana mimba ya miezi miwili , natumia sabuni ya unga nachanganya na dawa wadudu wanakufa Sana Kwa sabuni ya unga
IMG20210314182635.jpeg
 
Mambo vp ndugu zangu, ebwana ndugu yenu nmerudi tena ili tuendelee kupeana elimu kuhusu maswala mbali mbali yenye manufaa.

Leo nataka nikueleze maajabu nilioyashuhudia kwenye ufugaji wa Mbuzi wa kienyeji, ndugu zangu ufugaji watu wanauchukulia poa Sana lakini Una faida kubwa na za kushangaza.

Mnamo mwezi wa Saba mwaka 2020 nilinunua Mbuzi nane majike, na kwakua skua na Banda nilienda kuwaweka Kwa rafki yangu mwalimu wa shule ya masingi ambae nae pia alikua akifuga Mbuzi kadhaa.

Ilipofika mwezi wa 10 tayari nilikua nmepaua mabanda yangu na hii ilinifanya nipate hamu ya kuwafata Mbuzi wangu, mapema mwezi wa 11 niliwafata Mbuzi wangu na kuanza kuwafuga nyumbani kwangu, nikiwa tayari nmepata kijana wa kuwachunga.

Mbuzi Hawa kipindi nawanunua walikua kwenye muda wao wa kuanza kupandwa, namshkuru Mungu huyu rafki yangu mwl alikua na Dume bora kabisa so Mbuzi wangu alipofika kwake walianza kushughulikiwa barabara,

Tarehe moja Dec Mbuzi wangu wa 1 akazaa kitoto jike, tarehe 17mwezi huo huo Mbuzi wangu mwingine akazaa watoto wawili mmoja dume na mwingine jike, mpk kufkia tarehe za mwishoni mwa mwezi wa Kwanza Mbuzi wangu Saba walikua wamezaa na alikua kabaki mmoja tu nae alikua na mimba

Mwezi huu wa pili nae huyu akazaa vitoto viwili, na yule Mbuzi aliezaa mweiz wa 12 tayari amepandwa tena na atazaa mwaka huu huu,

Baada ya kuona namna Mbuzi wangu walivyozaa mfululizo kwakweli nilifurahi Sana, na nikaamua kuingia moja Kwa moja kwenye ufugaji wa Mbuzi wa kienyeji huku nikiwa na malengo lukuki, mwezi huu wa pili mwanzoni niliamua kuingia tena mnadani na kuongeza Mbuzi wengine nane ambao nao wawili walipofika tu wakanipatia ndama wawili, ukawa mwanzo rasmi wa me kuingia kwenye ufugaji wa Mbuzi.

Hivyo basi bila hiyana wala choyo, nmeamua kuandika hapa ili kuwapa motisha ndugu zangu ambao wanatamani kuingia kwenye ufugaji wa mbuzi wa kienyeji, hakika Mbuzi Wana faidia Sana,wanazaa Kwa muda mfupi na ndama wa miezi mitatu ukimuangalia unaweza usiamini, wanakua kwa Kasi Sana., Karibuni tuendelee kupeana ujuzi na elimu mbali mbali kuhusu ufugaji ,vile vile najihusisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji,kanga,bata mzinga,bata wa kawaida,na ng'ombe wa kienyeji.

Karibuni sana.

Instagram unaweza nicheki Kwa jina la
@rashidmbuzi89
View attachment 1714808View attachment 1714809View attachment 1714810
 
h

ongera kwa hatua ulioifikia na binafsi ningependa kujua upande wa chanjo na dawa za mbuzi
 
Sawa dawa za Mbuzi zipo nyingi Sana ni lazima uwasiliane na wataalamu wa mifugo, kuna chanjo za mapafu,dawa za minyoo za kunywesha na sindano kwaajili ya minyoo ya ngozi hizi baadhi tu dawa za Mbuzi Ila zipo nyingi sana
h

ongera kwa hatua ulioifikia na binafsi ningependa kujua upande wa chanjo na dawa za mbuzi
 
Vijana Watakiwa kujikita katika ufugaji-TALIRI​

0
BY VERONICA KOMBA ON JANUARY 20, 2021HABARI
NA MWANDISHI WETU
MTAFITI kutoka kituo cha Utafiti wa Mifugo (TALIRI) Kongwa ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa kituo hi cho Dkt. Wilfred Munis amewataka vijana kuacha kulalamika hakuna ajira na badala yake wajikite katika ufugaji kwani ni sekta inayolipa hapa nchini.

Aidha Dr.munisi amesema kuwa hakuna sekta ambayo inalipa kama sekta ya ufugaji nchini huku akiwataka vijana kujishughulisha ili kuendana na kasi ya mabadiliko katika sekta ya kilimo na ufugaji.

Dkt. Munis aliongea hayo hivi karibuni katika ziara ya waandishi wa habari na watafiti wa Kisayansi iliyoandakiwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia COSTECH na kufanyika Jijini hapa.

“Hivi nyie vijana acheni kulalamika hakuna kazi za kuajiliwa kwanini msifuge kisasa ili mnufaike na mifugo yenu mnayoihudumia huko nyumbani,sekta ya ufugaji na kilimo ni sehemu kubwa ya mafanikio njooni vituo vya utafiti tuwape mbinu za kufuga’’, alisema Dkt. Munisi.

Dkt. Munisi alibainisha kuwa endapo wafugaji watatumia mbinu bora za ufugaji wanauwezo wa kutengeneza pesa nyingi na kujiongezea kipato kikubwa kitakachowapelekea kuishi maisha mazuri na kusahau njaa.

Dkt. Munisi alisema kuwa wafugaji wakibadilika na kufuga kisasa wanauwezo wa kubadili maisha yao kwa asilimia 70 na kuwataka wafugaji kutembelea vituo vya utafiti wa mifugo nchini ili kujionea shughuli zinazofanyika ili kuboresha ufugaji wano na mifugo yao.

“Tunafanya utafiti wa mifugo ili jamii ya kitanzania inufaike na ijipatie kipato maana ufugaji ni sehemu ya utajiri lakini jamii haitambui na sisi kama Taasisi ya utafiti hapa kongwa milango ipo wazi kwa yule anayehitaji kujifunza namna ya kuboresha mifugo yake” alisema Dokta huyo.

Kwa upande wake Mtafiti idara ya mbuzi Christopher mtwange alisema kuna mbuzi aina ya gogo white na buchosa ambao wana uwezo wa kuzaa mapacha Watatu hadi sita endapo mfugaji atamtunza vizuri anaweza kupata idadi kubwa ya mbuzi kwa muda mfupi.

Serikali kupitia COSTECH kuanzia mwaka 2010 imetumia zaidi ya Sh. Billion 50 kufadhili miradi ya utafiti na ubunifu nchini.

Lengo la kufadhili miradi ya utafiti na ubunifu ni kusambaza hizi tafiti ili ziwafikie Wananchi huku wakitumia zaidi vyombo vya habari kuhabarisha umma kuhusu tafiti zinazofanyika katika taasisi mbalimbali za Kisayansi.
 
..kulingana na taarifa za wataalamu, mbuzi wa toka maeneo ya Dodoma " Gogo White ," na mbuzi toka maeneo ya Buchosa, wana sifa ya kuzaa mapacha.
 
Hbr mkuu Wakaliwetu,

Hii breed unetowa wapi..?
Mini utofauti (sifa maalum) wake n breed nyengine..?
Natoa Arusha ndugu, sifa kubwa ya Galla 1, wana nyama na uzito mzuri.2, Hawasumbuliwi sana na magonjwa.3, Ukuaji wao ni wa haraka na niwakujaza nyama tofauti na hawa wa kawaida.
Ukiwapata utafurahia ufugaji wako.
 
Back
Top Bottom