Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Manchid

JF-Expert Member
May 29, 2016
217
445
Mambo vp ndugu zangu, ebwana ndugu yenu nmerudi tena ili tuendelee kupeana elimu kuhusu maswala mbali mbali yenye manufaa.

Leo nataka nikueleze maajabu nilioyashuhudia kwenye ufugaji wa Mbuzi wa kienyeji, ndugu zangu ufugaji watu wanauchukulia poa Sana lakini Una faida kubwa na za kushangaza.

Mnamo mwezi wa Saba mwaka 2020 nilinunua Mbuzi nane majike, na kwakua skua na Banda nilienda kuwaweka Kwa rafki yangu mwalimu wa shule ya masingi ambae nae pia alikua akifuga Mbuzi kadhaa.

Ilipofika mwezi wa 10 tayari nilikua nmepaua mabanda yangu na hii ilinifanya nipate hamu ya kuwafata Mbuzi wangu, mapema mwezi wa 11 niliwafata Mbuzi wangu na kuanza kuwafuga nyumbani kwangu, nikiwa tayari nmepata kijana wa kuwachunga.

Mbuzi Hawa kipindi nawanunua walikua kwenye muda wao wa kuanza kupandwa, namshkuru Mungu huyu rafki yangu mwl alikua na Dume bora kabisa so Mbuzi wangu alipofika kwake walianza kushughulikiwa barabara,

Tarehe moja Dec Mbuzi wangu wa 1 akazaa kitoto jike, tarehe 17mwezi huo huo Mbuzi wangu mwingine akazaa watoto wawili mmoja dume na mwingine jike, mpk kufkia tarehe za mwishoni mwa mwezi wa Kwanza Mbuzi wangu Saba walikua wamezaa na alikua kabaki mmoja tu nae alikua na mimba

Mwezi huu wa pili nae huyu akazaa vitoto viwili, na yule Mbuzi aliezaa mweiz wa 12 tayari amepandwa tena na atazaa mwaka huu huu,

Baada ya kuona namna Mbuzi wangu walivyozaa mfululizo kwakweli nilifurahi Sana, na nikaamua kuingia moja Kwa moja kwenye ufugaji wa Mbuzi wa kienyeji huku nikiwa na malengo lukuki, mwezi huu wa pili mwanzoni niliamua kuingia tena mnadani na kuongeza Mbuzi wengine nane ambao nao wawili walipofika tu wakanipatia ndama wawili, ukawa mwanzo rasmi wa me kuingia kwenye ufugaji wa Mbuzi.

Hivyo basi bila hiyana wala choyo, nmeamua kuandika hapa ili kuwapa motisha ndugu zangu ambao wanatamani kuingia kwenye ufugaji wa mbuzi wa kienyeji, hakika Mbuzi Wana faidia Sana,wanazaa Kwa muda mfupi na ndama wa miezi mitatu ukimuangalia unaweza usiamini, wanakua kwa Kasi Sana., Karibuni tuendelee kupeana ujuzi na elimu mbali mbali kuhusu ufugaji ,vile vile najihusisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji,kanga,bata mzinga,bata wa kawaida,na ng'ombe wa kienyeji.

Karibuni sana.

Instagram unaweza nicheki Kwa jina la
@rashidmbuzi89
IMG_20210228_010318_447.jpeg
IMG20210228112803.jpeg
IMG-20210204-WA0011.jpeg
 
Uzi wako umekaa vyema sana nakupongeza sana kwa hatua uliyo ifikia, nakushauri tu unapochukuwa Mbuzi mnadani uwapatie huduma za afya kwanza kabla ya kuwachanganya na hao wengine hasa unapokuwa na Mbuzi wachanga.

usiwe mbali na kijana wa kazi hasa hichi kipindi ambacho wana zaa, pili usiruhusu hao watoto kwenda machungani na mama zao mpaka wamalize wiki 4.

Mama anae nyonyesha mpatie pumba na mchanganyiko wa mashudu ya alizeti au pamba, chumvi,chokaa na kuwawekea jiwe la kulamba maana lina madini ya kutosha, na uwapatie dawa za minyoo kwa muda muafaka.
 
Shukrani sana Kwa elimu boss
Uzi wako umekaa vyema sana nakupongeza sana kwa hatua uliyo ifikia, nakushauri tu unapochukuwa Mbuzi mnadani uwapatie huduma za afya kwanza kabla ya kuwachanganya na hao wengine hasa unapokuwa na Mbuzi wachanga. usiwe mbali na kijana wa kazi hasa hichi kipindi ambacho wana zaa, pili usiruhusu hao watoto kwenda machungani na mama zao mpaka wamalize wiki 4.
Mama anae nyonyesha mpatie pumba na mchanganyiko wa mashudu ya alizeti au pamba, chumvi,chokaa na kuwawekea jiwe la kulamba maana lina madini ya kutosha, na uwapatie dawa za minyoo kwa muda muafaka.
 
Back
Top Bottom