Ufugaji wa Mbuzi, Kanga, Bata Mzinga na Kuku

Nipo Singida mkuu nakukaribisha sana
Kwa Singida hapo wewe ni Maskini tu bado!! Mkoani hapo kila mnyama anakubali hali ya hewa tena bure kabisa bila dawa ulipaswa kuwa mbali sana, Mie niko Itigi lkn sasa hivi niko nje ya nchi na safari yangu iligharimiwa na faida ya wanyama na mpaka leo wapo natumiwa pesa ya mazao kila baada ya miezi mitatu!
 
mkuu kweli nilikua huko napiga kaz hao mbuz wanapatikana sana na niwakubwa. nilionyeshwa mbuz ambae bado mdogo ananyonya nilishangaa jinsi alivyo na umbile kubwa. ila bei nayo imechangamka sana hapo longido

..wasomaji wa mjadala huu wangependa kujua namna, na maeneo ya kuwapata mbuzi aina ya galla kutokea Longido.

..kwa hiyo kama unaweza tunaomba utuhabarishe zaidi, na ikiwezekana uweke contacts za wauzaji wa mbuzi galla walioko Longido.
 
kweli mkuu lkn naogopa kutoa mawasiliano sbb mimi binafsi nimewafahamu hao jamaa kwa kipindi kifupi nilichokaa hapo longido so siwajui tabia zao kwa undani, watu wakizurumiwa humu ndani reference ni mimi kitu ambacho sipendi. Lkn kuna mmoja nahisi ni dereva serikalini ngoja ni hakikishe, huyu anauza hawa mbuzi anaweza kutusaidia sbb kumtrace kama akifanya utapeli ni rahisi na namba zake za simu ninazo.
 
..nimekuelewa kabisa.

..hata mimi niliona video kwenye mtandao mhusika anadai ni muagizaji wa ng'ombe toka Kenya.

..nimeweka mawasiliano yake hapa Jamii Forums, lakini pia nimetoa ANGALIZO kwamba sijawahi kutumia huduma zake.

..pia inabidi uujulishe na upande wa pili, if it is OK kuweka mawasiliano yake hapa Jamii Forums, ili wanaohitaji mbuzi wa galla wamtafute.
 
Habarini za leo ndugu zangu, nimepatwa na janga kidogo kwenye ufugaji wa Mbuzi nimepatwa na ugonjwa unaitwa Goat Pox, Mbuzi wanapata mafua makali sana na kuvimba vidonda mwili mzima mpaka mdomoni hivyo kupelekea Mnyama kushindwa kula kabisa, ulimi unabadilika kuwa wa bluu, na vidonda vingi. Kwa sasa nimeshapoteza wanyama 15 na wengine 7 bado hali zao sio nzuri. Kwa wafugaji hiki kipindi ni cha huu ugonjwa tuwe na taadhari. Mungu awabariki nyote.
 
Mkuu POLE sana
na tafadhali usikate tamaa kabisa
Vipi kwenye kuhangaika, huu ugonjwa una chanjo, kama ipo inapatikana na ni maduka yapi
Mkuu pole saana, na Mungu aendelee kukuwekea mikono wanyama wako wapone
 
Habarini za leo ndugu zangu, nimepatwa na janga kidogo kwenye ufugaji wa Mbuzi nimepatwa na ugonjwa unaitwa Goat Pox, Mbuzi wanapata mafua makali sana na kuvimba vidonda mwili mzima mpaka mdomoni hivyo kupelekea Mnyama kushindwa kula kabisa, ulimi unabadilika kuwa wa bluu, na vidonda vingi. Kwa sasa nimeshapoteza wanyama 15 na wengine 7 bado hali zao sio nzuri. Kwa wafugaji hiki kipindi ni cha huu ugonjwa tuwe na taadhari. Mungu awabariki nyote.

..aisee pole sana.

..tunakuombea upate tiba ya haraka kwa mbuzi wako.
 
Habarini za leo ndugu zangu, nimepatwa na janga kidogo kwenye ufugaji wa Mbuzi nimepatwa na ugonjwa unaitwa Goat Pox, Mbuzi wanapata mafua makali sana na kuvimba vidonda mwili mzima mpaka mdomoni hivyo kupelekea Mnyama kushindwa kula kabisa, ulimi unabadilika kuwa wa bluu, na vidonda vingi. Kwa sasa nimeshapoteza wanyama 15 na wengine 7 bado hali zao sio nzuri. Kwa wafugaji hiki kipindi ni cha huu ugonjwa tuwe na taadhari. Mungu awabariki nyote.

Asante kwa taarifa kiongozi n pole kwa changamoto hii.
 
Amina sana nawashukuruni sana nyote kwa kunipa moyo ktk hili, kuhusu chanjo ya huu ugonjwa hakuna ila kuna program ktk serekali za EA wako ktk utafiti wa chanjo ya huu ugonjwa, kwa sasa natumia PENSTREP,400 na VITAMIN na DEXAKEL0.2,
Na pia huwa nawaosha kwenye vidonda na maji ya dreep na aiodin ya vidonda. Tunapambana kuokoa uhai wa hawa wanyama mpaka nguvu yangu ya mwisho.
Nilikwenda kwa wale watafiti wa magonjwa ya wanyama pale Kibaha mailimoja kwakweli msaada wao ni mdogo sana na niwagharama kubwa sana nimeshindwa kuwaelewa kabisaa na nikitengo cha Serikali.
Walisema wanachukuwa Sampuli kwa MBUZI 1 kwa sh elf 10, na unalipia Vet mmoja kuja kwako elf 50 na wanataka waje vet 2, mimi nina Mbuzi 85 wao wanasema nilazima wachukuwe sampuli kwenye asilima 25 mpaka 30 kwa Mbuzi wote, hapo nikaona gharama ni kubwa sana nimebakia napamabana na matibabu na Vet wangu na hali inakwenda vyema pole pole.
Nawaombeeni siku njema na baraka za Mungu ziwe juu ya kazi zenu.
 
mkuu naweza kuja kujifunza kwa kuona? naomba huu msaada tafadhali
 
Changamoto ni zakawaida kwekweli kikbwa nikuzikabili kuzikubali na kupambana nazo huku ukimtanguliza Mungu mbele daima tutashinda.
 
pole kiongozi kwa changamoto hii kubwa! nina imani utavuka. Swali langu mbuzi wako ni wa aina gani? naweza kuja kuwaona?
 
Back
Top Bottom