Aman Ng'oma
JF-Expert Member
- Nov 8, 2011
- 954
- 510
Lini unatarajia kuanza mafunzo tena?nahisi tarehe zmepita...*ANDAA DAFTARI, ANDAA KALAMU JIUNGE KWENYE GROUP LA WHATSAP LA "PATA ELIMU FUGA KUKU" UONE TOFAUTI*
*Pata Elimu Fuga Kuku* ni kundi jipya la Whatsap lenye lengo la kutoa elimu kabambe na ya aina yake ya namna bora na yenye tija ya kuendesha mradi wa ufugaji wa kuku.
Lengo kuu ni kuhakikisha kuwa mfugaji wa kuku anapata elimu sahihi itakayomsaidia kuendesha mradi wa ufugaji wa kuku kwa faida. Kutokana nafasi niliyonayo ya kuwa kwenye tasnia hii ya kuku kwa muda mrefu kama mtaalamu na mzoefu, nina nambo mengi ya msingi ambayo naamini mfugaji akiyapata yatamsaidia kwa kiwango kikubwa kuongeza ujuzi katika ufugaji wake. Hakuna atakayejuta kwa kushiriki darasa langu.
Natambua katika ufugaji wa kuku kuna changamoto nyingi lakini kubwa ni vifo vya ghafla vya kuku, kutamalaki kwa magonjwa, utagaji usiyoridhisha, chakula kutokidhi viwango na bei yake kuwa juu, tija ndogo katika ufugaji, kukithiri kwa matumizi ya dawa, gharama za uendeshaji wa mradi kuwa juu nk
Mradi wa ufugaji wa kuku si mradi rahisi kama ambavyo watu wengi wanadhani. Naamini waliyowahi na wanaofuga kuku wanalijua hili. Ufugaji wa kuku ni tofauti kidogo na ilivyo ufugaji wa wanyama wengine wenye miguu minne. Kuku anapoumwa anahitaji apate tiba haraka. Na tiba hiyo haiitaji kubahatisha. Lazima ugonjwa ujulikane, ujue pia dawa halisi. Vinginevyo utaishia kulia na kupata hasara kila siku wakati wenzako wakipiga pesa kupitia ufugaji huo huo wa kuku. Asikuambie mtu, kuku wanapokufa inauma sana kama una moyo mwepesi lazima Pressure ikushike hasa kama pesa iliyotumika kuanzishia mradi ulikuwa umeikopa.
Kufugaji kuku bila kuwa na elimu ni sawa na kutaka kujitumbukiza kwenye shimo huku ukijua wazi madhara yake. Kuku wana kawaida ya kubadirika badirika. Unaweza ukawaona leo wazima lakini si ajabu baada ya muda mfupi ukashangaa wakaanza kuumwa na wanapoumwa haichukui muda wanaanza kufa mara moja.
Vifo vinapotokea, mapigo ya moyo yataanza kukupanda, jasho litakutoka na hata usingizi utashindwa kulala. Mawazo mengi yatakujaa. Utawaza hasara unayoipata kwa kuwapoteza kuku wako.
Kwa kuona hili nimeamua kuanzisha mafunzo haya maalumu kwa njia ya whatsap yatakayoendeshwa kwa siku tatu kuanzia tarehe 15/11/2017 hadi 17/11/2017 ili niweze kutoa elimu yangu kwa watanzania wenzangu kwa gharama ndogo kabisa ya shilingi elfu tatu tu ili kuwangozea maarifa wafugaji na wale wote wenye lengo la kutaka kufanya mradi wa ufugaji wa kuku kama kazi.
Kuku wanahitaji uangalifu wa hali ya juu. Wafugaji wengi wanakosea sana. Unakuta anaanzisha mradi wa ufugaji wa kuku, halafu anamwachia mfanyakazi wake auendeshe. Ukimtazama mfanyakazi huyo, unakuta hajawahi kupata mafunzo ya aina yoyote hivyo anakuwa hajua hata zile ABC za ufugaji wa kuku matokeo yake mradi hauwi endelevu.
Kwa msingi huo, kama unamfanyakazi wako anayekusaidia kwenye shughuli za uangalizi wa shamba lako si vibaya naye ukamlipia ada ya shilingi elfu tatu ili aweze kupata mafunzo haya muhimu, mafunzo yatakayo mwongozea maarifa na stadi za kuwahudimia kuku wako. Halikadhalika si vibaya kama utaamua hata mke wako naye ukamlipia ili aweze kushiriki na kunufaika na mafunzo hayo maridhawa.
Maarifa siku zote hayaozi. Tunawahamasisha watumishi mbalimbali na hata wastaafu nao waweze kushiriki katika mafunzo hayo ili kujiongezea maarifa yatakayowawezesha kutekekeza mradi wa ufugaji wa kuku kwa weledi.
Kama utahitaji kujiunga na kundi la *PATA ELIMU FUGA KUKU* tafadhali wasiliana nami kwa njia ya ujumbe mfupi kupitia namba 0767989713 au 0715989713 ili nikupatie namba utakayofanyia malipo yako.
Mara baada ya kukamilisha malipo, nitakuunga rasmi kwenye Group hilo la *PATA ELIMU FUGA KUKU*
Mafunzo haya yataendeshwa na Ndugu Aman Ng'oma aliyebobea na kuwajua vizuri Kuku. Bwana Ng'oma ni Mkurugenzi Mtendaji na Mwanzilishi wa Kampuni ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd. Ndugu Ng'oma kitaaluma yeye ni afisa Mifugo, Mchumi Kilimo na Biashara, na pia Mtu wa Miradi. Ndugu Ng'oma ana Cert. Animal Health and Prod., Dip. Animal Health, BSc Agric.Eco.&Agr and Post Grad. Dip. Project plan.&Mgt.
Wote mnakaribishwe kwenye mafunzo haya muhimu na ya aina yake kuwahi kufanyika.
*Tafadhali saidia kushare*
Acheni uongo jmn hiv mnajua faida ya mil 30?NDUGU SMU, kazi yako iko ndani ya uwezo wetu.Tuna uzoefu na hiyo kazi.Kuna wapo ambao tayari tumekwisha waanzishia mradi kama wako na wamefanikiwa, kwa mfano kuna mteja ambaye tumemwanzishia mradi na kwa sasa,kila mwezi anatoa kuku 5000 na kuwapeleka sokoni.Yeye anatotoresha na kufuga kuku wa kienyeji.Kila kuku anauzwa kwa shs.10,000 kwa bei ya jumla,ebu imagine kuku 5000 ni sh. ngapi anatengeza,ukipiga hesabu hapo utaona kila mwezi anatengeneza milioni 50.Akitoa gharama,let say milioni 20,je kuna kuna kazi gani ambayo unaweza ukaearn milioni 30 kwa mwezi!Kwa hiyo kama utahitaji ufafanuzi zaidi nitumie namba yako kwenye private message nitakutumia yangu.
Hatujafikiria bado ila ukihitaji masomo tuliyoyatoa tunaweza kukutumia kwa ada ya tsh 5000Lini unatarajia kuanza mafunzo tena?nahisi tarehe zmepita...
Uko wapi?Pata kuku wataamu kabisa kujiramba mwanzo mwisho
( *Wakienyeji* ) wakubwa wa kutoshaaa 20, 000tsh @1..
*_oda ya kuanzia Kuku 7 unapata punguzo_ ...*
* _Popote ulip0 dar unaletewa..*_
niko ubungo dar es salaam nichekiUko wapi?
Una mpango wa kuanza na kuku wangapi?Habari zenu wakuu,
Kama title inavyojieleza, nataka kujua ni nini au vitu gani vya kuzingatia kabla na nitakapoanza kufuga kuku wa mayai, KIBIASHARA