Ufugaji Mbuzi wa kienyeji (Asili) kibiashara

Dume mmoja kwa wakati mmoja? S atakua anakojoa upepo
Ndugu inategemena na unamajike wangapi na unataka kupandishaje hapo ni wewe tu mfugaji na malengo yako. Ni rahisi sana kikubwa ni wewe unahitaji kufanyeje na kwa wakati gani maana hata hali ya hewa pia nayo ni yakuangalia sana wakati wa uzalishaji.
 
Umeandika majike 20 au 30 kwa pamoja.. labda utumie uhamilishaj ila kwa njia ya kupanda kwa dume moja ni kitu haiwezekan
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu. naomba niwapongezeni sana nyote ktk kujenga mawazo ya kutaka kuingia ktk miradi kama hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji wa Mbuzi na nina fuga Mbuzi kwa muda mrefu, niwaombeni kitu ufugaji ni mzuri na una faida na changamoto zake, kikubwa ni kukubali kujifunza na kujijengea umakini ktk ukaguzi na usimamizi wa mifugo yako. Kwa aliyepo Dar namkaribisha kwangu aje tujifunze pamoja na tugawene ujuzi kwa pamoja. Kwa anae anaza kufuga nakuomba sana usinunuwe mbegu kwanza kabla hujapita kwetu wafugaji tulio kutangulia ujifunze vitu halafu ndio uingize Mbegu shambani kwako. Karibuni kwa maswali mbali mba;li nipo hapa tutasaidiana kwa kadiri Mungu atakavyo tujaalia.
 
Ndugu inategemena na unamajike wangapi na unataka kupandishaje hapo ni wewe tu mfugaji na malengo yako. Ni rahisi sana kikubwa ni wewe unahitaji kufanyeje na kwa wakati gani maana hata hali ya hewa pia nayo ni yakuangalia sana wakati wa uzalishaji.
Nahitaji nije kujifunza ufugaji wa Mbuzi. Nina heka nne Morogoro nahitaji kufuga. Unapatikana wapi?
 
Nawasalimuni kwa jina la Mungu. naomba niwapongezeni sana nyote ktk kujenga mawazo ya kutaka kuingia ktk miradi kama hii ya ufugaji. Mimi ni mfugaji wa Mbuzi na nina fuga Mbuzi kwa muda mrefu, niwaombeni kitu ufugaji ni mzuri na una faida na changamoto zake, kikubwa ni kukubali kujifunza na kujijengea umakini ktk ukaguzi na usimamizi wa mifugo yako. Kwa aliyepo Dar namkaribisha kwangu aje tujifunze pamoja na tugawene ujuzi kwa pamoja. Kwa anae anaza kufuga nakuomba sana usinunuwe mbegu kwanza kabla hujapita kwetu wafugaji tulio kutangulia ujifunze vitu halafu ndio uingize Mbegu shambani kwako. Karibuni kwa maswali mbali mba;li nipo hapa tutasaidiana kwa kadiri Mungu atakavyo tujaalia.
Naomba no yako ndugu nije kujifunza
 
loader.png
 
Hapa linatakiwa eneo kubwa , alaf unaligawa hata vipande vinane vya ukubwa wa hekari mbili kila kimoja , unazungusha fensi nzito , supply ya maji iwe constant , ataishi kifalme Sana , na mbuzi atawakimbia , Ila hii ya kuwapeleka machungani na kurudi chenga tupu , mbuzi Wana visirani Sana kila mara mchungaji atakuwa anarudi amevunja mgongo mmoja

View attachment 2470846
Mkuu huu sasa uwekezaji wa mabiloni, eka 16 zenye fensi nzito? Huu sio mradi wa wanaojitafuta sasa.
 
Natamani kufahamu experience ya wafugaji wa mbuzi juu ya soko lake lipoje.

Kwa maana uhitaji wake sokoni?
Changamoto zake kwenye soko hasa kwa haya makundi mawili ya mbuzi kwa maana mbuzi wa asili na mbuzi wa kisasa ikoje? (Competition ikoje sokoni)

Vp kuhusu bei ya soko kwa maana nimeona hapa Kuna mchangiaje amesema bei ya mbuzi ya kisasa inafika Hadi 2.5 mil, ni kweli utaweza kuuza kwa bei hiyo kwa mlaji wa mwisho? Inafikirisha kidogo hasa ukiwaza bei ya mbuzi pale vingunguti. Hii imekaaje!!
 
Habari za leo ndugu naomba nikusaidie kidogo kwenye hili swala la ufugaji wa Mbuzi. Kwakaweli sisi TZ bado tuko nyuma sana ktk uzalishaji na kuwa na mbegu bora za kuweza kutufanya tuingie sokoni na kupambana kwaajili ya kufikia malengo ya mahitaji ya soko, kwahiyo ndio sasa tunahimizana kutafuta mbegu zilizo bora ili tuweze kuendana na soko linavyo hitaji.
Kwa soko lilivyoko tunapashwa kutoka kuuza Mbuzi kwa kumwangalia kwa umbo nakumkisia halafu ndio tumpange bei hii inakuwa haina faida kwa mfugaji hata kidogo, ndipo hapo sasa yatupasa kutafuta hizo mbegu za kisasa ili tuweze kupata Mbuzi atakaye tuwezesha kupata Kg za juu na iwe kwa Muda mfupi.
Kuhusu Mbuzi kuuzwa bei ya 2.5 ml hilo naomba lisikusumbue ni kwamba, unapo anaza kuzalisha kumbuka hizo mbegu zinauwezo wa kutoa watoto amabao wakifikisha miezi 6 anaweza kuwa sokoni labda awe kwa mbegu au wa supu au Nyama ktk viwanda vilivyo anzishwa nchini hapa au kusafirirsha nnje. Sasa wewe usitegemee kuuza kwa ml bali wewe utapata faida yako kwa kadiri utakavyo kuwa unazalisha na utakavyo kuwa unauza. Mf ano ukiuza kila uzao kwa sh laki 2 mpaka moja na nusu kwa watoto walao 5 kwa uzao wa kwanza unahasara gani? kikubwa ni kujipanga na tuelewe ufugaji faida yake haiji hapo kwa hapo kama uuzaji wa duka. barikiwa sana. Karibu ktk ufugaji.
 
Asante kwa ufafanuzi ndugu MUBENDE barikiwa sana.
Vp kuhusu soko la wazarishaji wa nyama hapa nchini mfano Hawa frostan limited, nguru hill ranches? Je, Kuna utaratibu wowote wa kuwafikia kuweza kufanyanao biashara? Hakuna urasimu wowote?
Je, kwa wafugaji wa kawaida Kuna kipi kinahitajika ili kupata tija kwa haya makampuni makubwa ya uzalishaji wa nyama hapa nchini?
Tunaomba ufafanuzi kutoka kwako na kwa yoyote anayefahamu utaratibu wa kuwafikia kibiashara. Asante
 
Karibu sana tutasaidiana kwa kadiri iwezekanavyo ili wote tufikie malengo ktk ufugaji
Asante sana mkuu, kwahiyo ukiwapandisha hao mademe wa kigeni kwa hawa majike wa asili wakipatikana watoto wataongia sokoni kama mbuzi wa asili au wa kisasa? Na vipi kwenye soko kunakuwa na uwanja mpana kama hawa wa asili?
 
Hao tunawaita F1 kitaalamu au cross hapo unakuwa umeboresha shamba lako, na ndicho tunachokifanya na ndicho tunatakiwa kukifanya kuboresha mashamba yetu, ila kumbuka kuna kuangalia majike yanayo faa kufanya hiyo program ya cross. Na ndio maana kila mara nasisitiza sana tujitahidi sana kutembelea wafugaji wenzetu ili kujifunza kwanza kabla ya kuanza kununua hizo mbegu kwasababu Mbegu ni gharama sana kuzinunua.
 
Asante mkuu, kwahiyo sokoni hao F1 wanauzwa kwa bei kama ya hawa wa kienyeji?
 
Back
Top Bottom