Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,719
- 114,067
Wanabodi
Mwandishi wa Habari wa ITV, Ufoo Saro, ametoka rasmi hospital na leo amefanya Ibada ya Shukrani katika kanisa la KKKT Kibamba ambapo amemshukuru Mungu kwa yote na kutoa shukrani kwa wote waliosimama na yeye wakati wote wa matatizo wakimfariji na kumsupport kwa hali na mali.
Ibada hii ya shukrani imefuatiwa na chakula cha mchana.
Japo nipo hapa na Ufoo yuko accessible, nina maswali yangu fulani ya dukuduku ningetamani nimuulize, ila nahofia kutonyesha vidonda na kumrudisha kwenye machungu anayojaribu kuyasahau.
Wish afike mahali akiri licha ya kumlilia mama yake aliyeondoshwa na Mushi,anapaswa pia kumlilia Mushi despite all the odds kwa sababu ni mzazi mwenzie na baba wa mtoto wake hivyo amekumbwa na double tragedies!.
Naomba tuungane kwa kumpa Ufoo pole kwa yote ila life has to go on!.
Ufoo, welcome back to the game!.
Pasco.
KITAIFA
Ufoo Saro: Niliokoka kufa kutokana na miujiza ya Mungu, namshukuru
Mwandishi wa habari wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro akisoma somo kwenye biblia wakati wa ibada maalumu ya shukrani kwenye Kanisa la (KKKT ) Usharika wa Kibamba nje kidogo ya Jiji la Dare Salaam jana. Picha na Sanjito Msafiri.
Posted Jumatatu,Novemba18 2013 saa 15:24 PM
KWA UFUPI
Dar es Salaam. Mtangazaji wa Kituo cha Televisheni cha ITV, Ufoo Saro ambaye alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi, amefanya ibada na kusema: "Namshukuru Mungu kwa kumponya."
Ni mara ya kwanza Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu, MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.
Katika ibada hiyo iliyofanyika katika Kanisa la Kilutheli Tanzania (KKKT) Usharika wa Kibamba, Jimbo la Magharibi, Ufoo huku akitokwa na machozi na wakati mwingine kushindwa kuzungumza alisema: "Ni miujiza tu ya Mungu yeye kunifanya mimi kuwa hai leo."
Mtangazaji huyo ambaye alilazwa kwa zaidi ya wiki mbili, aliwashukuru watu wote waliomtia moyo, kumsaidia kipindi chote alichokuwa mgonjwa.
"Sina cha kuwalipa, ninawashukuru sana kwa wema wenu, pia kwa kuniombea. Mungu ni mkubwa na amenipigania, naendelea vizuri kwa sasa," alisema na kuongeza:
"Mungu alinisimamia na nyinyi pia mliniombea, hakika sina budi kushukuru kwa kila jambo. Nitasoma zaburi ya 146 katika Biblia Takatifu ili kumshukuru Mungu kwa kunisaidia."
Ufoo alisema kuwa ameamua kumshukuru Mungu kwa sababu siyo watu wote wanaopata matatizo kama yake wanapona.
Mchungaji aliyeongoza misa hiyo iliyoanza saa 4 asubuhi hadi saa 7 mchana, Joseph Maseghe alisema Mungu hakupanga Ufoo afariki dunia kwa kupigwa risasi.
"Mungu bado anakuhitaji, hakupanga ndiyo maana upo nasi leo. Hautakiwi kulia huu ni mwanzo wa maisha yako mengine, usilie unachotakiwa ni kumshukuru Mungu kwa kila jambo," alisema.
Misa hiyo ilihudhuliwa na watu mbalimbali wakiwamo wafanyakazi wa ITV pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Grace Kihwelu, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), John Heche.
Baada ya kumalizika kwa misa hiyo, ndugu na marafiki wa karibu wa Ufoo walialikwa na mtangazaji huyo katika hafla fupi ya chakula cha mchana.
Akizungumza wakati akiwakaribisha wageni katika chakula cha mchana, alisema: "Nimepata pigo kubwa katika maisha yangu, familia yetu sasa haina baba wala mama, kweli namshukuru Mungu na nawaombea kwa Mungu wote walioniombea na kunitakia mema, sijui nimpe nini Mungu, sijui kwa kweli."
Source: Mwananchi.

- Ni mara ya kwanza Saro kuzungumza tukio hilo tangu aliporuhusiwa kutoka Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu, MOI ya Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.