mkuu uwe na huruma , ingawa na mimi kwa mengi yaliyosemwa humu nilijua kwamba tusingeweza pata muendelezo wake. hapa ninaanza kuyaamini yale ya udaku , inaonekana ni hatari sana huyu mama kuliko hata mchawiNingeshangaa kama angesema.
Mushi alikosea sana kulenga.
Hakuna cha siri, mlimzika fedha na mali zake alizokuwa akituma umjengee nyumba wewe ukajijengea mwenyewe na mama'ko. Na ukamsaliti na kutembea na wengine nae akitegemea u wake pekee.
Umemuumiza moyo. Kuna uwezekano mkubwa ni wewe uliyemuuawa na kisha ukajipiga risasi mwenyewe, hawa polisi wanatakiwa wafanye uchunguzi wa kina. Itakuwaje aliyejiua awe na risasi mbili sehemu tofauti?
Mali uliyomzika huto ila kwa raha, itakutesa maisha yako yote.
Hapa kuna utata! Iwe yeye ndo alie mshoot mzazi mwenzie au mwenzie ndie alie mshoot hakuna wa kutoa ushaidi. Yeye mwenyewe ndio anaejua ukweli manae key suspects wote wako 6 feet down! Hata akisema hakuna wa kubalance story hata majiran hawawez kuchukuliwa na uzito sana manake hawakuwa ndani wakati wakizozana! Walisikia milio ya risasi na hawakuona aliekua anafyatua hizo risasi.
Pia hakuna mwenye ushahidi wa moja kwa moja kwamba alikuwa anatumiwa fedha za kujenga! Nani aliona hizo fedha?zilikuwa sh.ngap? Na zilitumwa kwa njia gan? Makubaliano ya yeye kumjengea mumewe nyumba yako wap? Na hiyo nyumba ingejengwa wap?
Hata akiongea nani wa kubalance na kusema yuko sawa au anaongopa? Ts a f..ng mumbo jambo!
Ningeshangaa kama angesema.
Mushi alikosea sana kulenga.
Ushahidi wa kutumiwa fedha ni rahisi sana kuupata ukitakikana.
Uliona au ulisoma au kusikia wapi mtu anajiua kwa kujipiga risasi mara mbili sehemu tofauti?
Stori:Brighton Masalu na Chande Abdallah
SIKU chache baada ya Mtangazaji wa Runinga ya ITV, Ufoo Saro kuruhusiwa hospitalini alipokuwa amelazwa baada ya kudaiwa kupigwa risasi na mzazi mwenzake, marehemu Anther Mushi, ameibuka na kula kiapo cha siri.
Ufoo ambaye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, katika tukio la yeye kupigwa risasi, alimpoteza mama yake mzazi aitwaye Anastazia Saro aliyedaiwa kuuawa na marehemu Mushi aliyejiua kwa risasi.
Akizungumza na gazeti hili Ufoo alisema, kamwe hawezi kusema kilichokuwa kikiwagombanisha yeye na marehemu Mushi mpaka siku ya mwisho wa uhai wake.
Siwezi kuzungumzia kabisa chanzo wala ugomvi wetu mimi na marehemu Mushi. Hiyo itakuwa siri yangu, alisema Ufoo.
Katika mahojiano na gazeti hili, mtangazaji huyo alipoulizwa kuhusu msimamo wake wa uhusiano baada ya kupona kabisa alisema, hawezi kujiingiza tena kwenye mapenzi kwa sasa.
Sitaki kabisa kusikia juu ya mapenzi, siwezi kuliweka suala hilo akilini tena, alijibu kwa kifupi kwa sauti ya chini lakini yenye mkazo.
GPL