1. Siku zote niko open minded na very positive person, siwezi kuja hapa kila siku na machungu tuu na kulaumu kila mtu mwingine lakini not myself, viongozi walioko kwenye power wamechaguliwa na wananchi, hawakujiweka tu wenyewe, hilo ninaliheshimu sana, na ni kuheshimu demokrasia pia, CCM haikujiweka kwenye power, imechaguliwa na wananchi, sasa ninatakiwa, kwanza kuwa na heshima nao, na pia kuwa na Constructive Criticism, kwa mfano mimi na baadhi ya wananchi hapa tuliilalia macho Richimonduli, mpaka mwisho na kuona Waziri Mkuu na mawaziri wawili tena marafiki wa karibu na rais wakijiuzulu, hata bongo nzima JF tumepata credit kwa hilo kwamba ndiyo chanzo cha the whole saga, sasa hatuwezi kuanza kujishushia heshima yetu hapa kwa kuanza kukurupuka ovyo na attacks bila facts au angalau dataz, mkuu hii JF sasa ni chombo muhimu sana cha haabari za siasa ya nchi yetu, kwa hiyo ni lazima tuwe makini na tunachosema, sio kuropoka ropoka ovyo bila sababu, yes ninaona jinsi tulivyoingiliwa sasa hapa JF, lakini hawatadumu maana the originals tuko macho sana na tunajua kinachoendelea! JF haikufika hapa mkuu kwa kurusha unfounded shutuma kila siku tena nonstop kwa CCM na serikali, no mkuu! Hapa mkuu tunaziangalia ishus kwa makini na kwa undani sana, kwa hiyo hili la kuuzwa kwa nyumba za serikali I am sorry kuwa sikubaliani na hizi shutuma kwa sababu kuna wananchi wengi sana wafanyakazi wa serikali ninaowafahamu wamenufaika nao, na ninajua kua wachache pia walionufaika kwa ujanja, lakini percent yapo ndogo sana kiasi kwamba I am willing to live with it.
2. Uongozi mbaya wa CCM haupo, ila kuna viongozi wachache wasiokuwa na uwezo wa kuongoza ndani ya CCM na serikali, now that has nothing to do na CCM collectivelly, unasema tatizo ni siasa za CCM halafu unasema CRDB inafanya vizuri, sasa inafanyaje vizuri kwenye mazingira ya siasa hizo hizo mbovu za CCM?
CCM collectivelly, ingekuwa na siasa mbovu Lowassa, Karamagi, Msabaha, wasingejiuzulu, taifa letu lisingefikia lilipo leo, jamani hapa bongo sio majuu naona wengi sana tunachanganya hilo, na kufikiri bongo tunatakiwa ku-operate kama majuu, no! hii ni bongo mambo yetu kuanzia uchaguzi wa viongozi mpaka maadili yetu kiuongozi ni ya ki-bongo bongo, kwa hiyo tusitegemee mabadiliko yatatokea kama umeme, hapana inatakiwa sacrifice wakuu na inapaswa kuwa clear kuwa hakuna wa kumfanyia mwingine ila ni sisi wenyewe kujiingiza huko kwenye siasa.
Kwa hiyo mkuu mimi sio mtetezi wa CCM na serikali yake, mimi mwannchi wa bongo mwenye upeo wa kuchanganua na kulinganua siasa ya nchi yangu in a positive way, na with an open mind, na in the process understanding kwamba bongo sio Ulaya, pia kwamba wa-Tanzania baada ya kuwa under one party rule kwa muda mrefu sana na kutojua anything kuhusu uwajibikaji, itachukua muda sana kupata mabadiliko tena kwenye hilo niko very realistic kwamba huenda it will happen kwenye another generation, lakini sio hii yetu, na kwamba sio kila kiongozi wetu ni fisadi, kwamba sio kila maamuzi ya serikali yana walakini wa ufisadi, na kwamba tatizo sio CCM, bali ni kwanza sisi wananchi halafu ndio viongozi wetu,
Na kama huamini kuwa sisi wananchi pia ni tatizo kubwa kwa taifa letu kisiasa, hebu pitia threads zote hapa Jambo Forums uone!
Ahsante Mkuu.