engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,149
- 1,441
Leon Bahati
SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeingia tena katika kashfa ya ufisadi wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma, baada ya kubainika kuuza kinyemela sehemu yenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe Kiwira kwa kampuni ya Tan-Power Resources (TPR).
Uamuzi huo unaelezwa na wachunguzi wa mambo kuwa utaathiri mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kwa kusababisha bei ya nishati itakayozalishwa eneo hilo kuwa ghali na italisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 600 milioni sawa na Sh960 bilioni.
Tuhuma hizo za ufisadi, ziliibuka kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na kuifanya iwaite maofisa wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini kujieleza mbele yao, jana.
Sehemu inayodaiwa kuuzwa ilitajwa kuwa ni mlima Kabulo, ambayo aliielezea kuwa ina utajiri mkubwa zaidi wa makaa ya mawe kuliko eneo jingine la Kiwira.
Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alithibitisha kamati yake kuwaweka 'kitimoto' maofisa waandamizi wa wizara hiyo.
"Tumewaita ili watupe maelezo ya kina kuhusu suala hilo," alisema Zitto akilalamika; "Hili ni tatizo la kuchezea raslimali za nchi,"
Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema tukio hilo limekuja wakati ambao serikali imetakiwa kumiliki hisa zote za mradi huo ili kuhakikisha anapatikana mbia anayeweza kuendesha mradi huo kwa faida.
Alisema mradi huo ambao ulikuwa unamililikiwa kwa pamoja kati ya serikali na kampuni ya Tan-Power Resourses, ulitakiwa kusimamishwa pia wafanyakazi walipwe haki zao.
Lakini mpaka sasa, alisema wafanyakazi hawajalipwa ingawa mradi huo umesimama jambo ambalo linaendelea kuisababishia hasara serikali.
Akizungumzia athari za kuuzwa kwa eneo lenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alisema mradi wa umeme unaotarajia kuanzishwa, gharama yake itakuwa kubwa kutokana na malighafi kuzalishwa na kampuni nyingine.
Ole Sendeka alisema Serikali ilikopa Benki ya Dunia dola za Marekani 600 milioni sawa na Sh960 bilioni kwa ajili ya kuendeleza mradi huo lakini kwa kuuzwa sehemu ya Kiwira, serikali itapata hasara kwa kulipa fedha hizo na riba yake kwa mradi ambao unamilikiwa na kampuni binafsi.
Hadi jana jioni Mwananchi lilipoondoka katika ofisi za Bunge, watendaji wa Wizara walikuwa bado hawajawasilisha maelezo yao mbele ya kamati hiyo.