Ufisadi wa mabilioni tena Nishati na Madini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa mabilioni tena Nishati na Madini

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by engmtolera, Jan 20, 2012.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Leon Bahati
  SERIKALI kupitia Wizara ya Nishati na Madini imeingia tena katika kashfa ya ufisadi wa matumizi mabaya ya rasilimali za umma, baada ya kubainika kuuza kinyemela sehemu yenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe Kiwira kwa kampuni ya Tan-Power Resources (TPR).

  Uamuzi huo unaelezwa na wachunguzi wa mambo kuwa utaathiri mradi wa kuzalisha umeme wa makaa ya mawe kwa kusababisha bei ya nishati itakayozalishwa eneo hilo kuwa ghali na italisababishia serikali hasara ya dola za Marekani 600 milioni sawa na Sh960 bilioni.

  Tuhuma hizo za ufisadi, ziliibuka kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na kuifanya iwaite maofisa wakuu wa Wizara ya Nishati na Madini kujieleza mbele yao, jana.

  Sehemu inayodaiwa kuuzwa ilitajwa kuwa ni mlima Kabulo, ambayo aliielezea kuwa ina utajiri mkubwa zaidi wa makaa ya mawe kuliko eneo jingine la Kiwira.

  Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe alithibitisha kamati yake kuwaweka 'kitimoto' maofisa waandamizi wa wizara hiyo.

  "Tumewaita ili watupe maelezo ya kina kuhusu suala hilo," alisema Zitto akilalamika; "Hili ni tatizo la kuchezea raslimali za nchi,"

  Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisema tukio hilo limekuja wakati ambao serikali imetakiwa kumiliki hisa zote za mradi huo ili kuhakikisha anapatikana mbia anayeweza kuendesha mradi huo kwa faida.

  Alisema mradi huo ambao ulikuwa unamililikiwa kwa pamoja kati ya serikali na kampuni ya Tan-Power Resourses, ulitakiwa kusimamishwa pia wafanyakazi walipwe haki zao.

  Lakini mpaka sasa, alisema wafanyakazi hawajalipwa ingawa mradi huo umesimama jambo ambalo linaendelea kuisababishia hasara serikali.

  Akizungumzia athari za kuuzwa kwa eneo lenye utajiri mkubwa wa makaa ya mawe, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka alisema mradi wa umeme unaotarajia kuanzishwa, gharama yake itakuwa kubwa kutokana na malighafi kuzalishwa na kampuni nyingine.

  Ole Sendeka alisema Serikali ilikopa Benki ya Dunia dola za Marekani 600 milioni sawa na Sh960 bilioni kwa ajili ya kuendeleza mradi huo lakini kwa kuuzwa sehemu ya Kiwira, serikali itapata hasara kwa kulipa fedha hizo na riba yake kwa mradi ambao unamilikiwa na kampuni binafsi.

  Hadi jana jioni Mwananchi lilipoondoka katika ofisi za Bunge, watendaji wa Wizara walikuwa bado hawajawasilisha maelezo yao mbele ya kamati hiyo.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Niliona hii habari jana, hakika serikali yetu inasikitisha, na haina kiongozi!
  Ni nani hao huko wizarani walio untouchables' kiasi hicho?
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  mambo mengine yanatia hasira sana
   
 4. I

  IVETA Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Ufisadi kwa waandishi nao uko kwa mfano, waandishi wa habari kilimanjaro


  1. Mbunge wa rombo joseph selasini, juzi alimfunga paka kengele kwa kuelezea jinsi baadhi ya wanahabari wa mkoa huo wanavyowanyanyasa wadau wao ili wapewe kitu kidogo. Habari hiyo imechelewa sana ila tunamshukuru haswa kwa vile ni mbunge wa jimbo ninalotoka.

  Pamoja na mambo mengine mbunge selasini amefungua mjadala ambao hauna budi kujadiliwa na jamii kwa ujumla kutokana na tasnia ya habari kuwa moja ya sekta muhimu katika jamii.

  Ni kwa sababu hiyo basi ndiyo iliyonifanya mimi na wenzangu kuamua kuzifuatilia tuhuma hizo kwa undani zaidi kwa kuwasiliana na wadau wengine walioko huko mkoa wa kilimanjaro kujua kulikoni na ni ushauri gani tutoe.

  Katika kufuatilia kwanza kabisa tuligundua ya kuwa pamoja na kutokuwataja waandishi hao, sisi tulipata taarifa za majina yao nao ni gift mongi wa majira, venance maleli wa moshi fm na ambae hujitambulisha kuwa ni mwandishi wa gazeti la mwananchi na rodrick mushi wa tanzania daima.


  Taarifa za ziada zinaonyesha ya kuwa mbunge alishalalamika mpaka klabu ya waandishi kilimanjaro bila kupata ufumbuzi wowote hivyo kuamua kumwaga mambo hadharani kwenye kamati ya ushauri ya mkoa hivi karibuni huku akiweka wazi ushahidi alionao kuhusiana na sakata hilo.

  Katika uchunguzi wetu wa ziada ni kuwa hata baadhi ya wahariri walipewa taarifa hizo na ushahidi wake lakini hakuna hatua ambazo zimechukuliwa hadi sasa.

  Hata klabu ya waandishi nayo haijachukuwa hatua zozote hata za kuwahoji watuhumiwa hao. Inasikitisha haswa kwa vile watu wengi wamekuwa wakilalamika kuhusiana na tabia hizi mbaya za waandishi kutishia wadau ili wapewe pesa.

  Tuhuma hizi napenda niziunganishe na zingine ambazo zinawahusu baadhi ya viongozi wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa kilimanjaro, ambao ni makamu mwenyekiti rodrick makundi, katibu msaidizi nakajumo james na mweka hazina msaidizi rodrick mushi, ambae pia anatuhumiwa kwenye lile la kwanza.

  Viongozi hawa wanadaiwa kutumia huruma ya mkuu wa mkoa wa kilimanjaro ya kuwapa upendeleo katika ugawaji wa sukari kwa manufaa yao wenyewe kwa kufanya biashara ya kuuza sukari hiyo kwa kutumia jina la klabu tena kwa wafanya biashara ambao wanaisafirisha nje huku wakishirikiana na baadhi ya waofisa wa chama kikuu cha ushirika kncu.

  Cha kujiuliza hapa ni kama viongozi hawa watakuwa na uwezo kuwajadili wanahabari ambao wanadaiwa kuwanyanyasa wadau wa habari.

  Kwa kweli hapa kunahitajika busara ya hali ya juu ili kuinusuru tasnia ya habari na tuhuma hizi nzito.


  2. Pia kuna tuhuma kuwa maleli alitumiwa na wafanyabiashara kadhaa wa wilaya ya rombo ili kumchafua mkuu wa wilaya hiyo ambapo walichangisha shilingi milioni 3 na kumuita mtangazaji wa itv renatus mtabuzi, ambae alitengeneza kipindi maalum cha kumchafua dc wa rombo ili aonekane mbaya. ukweli ni kwamba hizo zilikuwa ni njama za wanasiasa ambao ni wafanyabiashara za magendo wakiongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya rombo pamoja na wafanyabiashara wengine wa haramu.

  Mutabuzi alipewa shilingi milioni 1.5, ambapo pia alifadhiliwa malazi, chakula na vinywaji na mmoja wa mafisadi hao wakati akiwa wilaya ya rombo kwa kazi hiyo isiyo na nia njema kwa utawala bora. kuna ushahidi wa uhakika. Kuna taarifa pia mutabuzi alipewa tiketi ya ndege kurudi dar es salaam baada ya kudai wakubwa zake wanangojea taarifa yake hiyo kwa hamu kubwa.

  Maleli katika sakata hili amesikika akisema kuwa amepata ushirikiano mkubwa kutoka kwa afisa usalama wa wilaya ya moshi kwa vile ofisa usalama wa wa rombo alimnyima ushirikiano.


  Viongozi hawa watatu wa press klabu hawana budi kuchunguzwa kwa undani zaidi kutokana na wao kunogewa na biashara hiyo ya sukari wanayoifanya kwa kutumia mgongo wa klabu na huruma ya rc kwa wanahabari na ndiyo sababu wanashindwa hata kuwahoji wale wote wanaotuhumiwa kuwatishia wadau wa habari kuwa wana habari zao nyeti ili wapewe fedha wasiziandike.

  TAARIFA ZA MALELI.

  Maleli huyu anatuhuma nyingi ambazo zinamnyima sifa za kuwa miongoni mwa jamii ya waandishi wa habari kwa vile ni mchochezi katika mambo mengi.

  1. kwanza anawagonganisha maofisa usalama wa rombo na moshi kwa kuonyesha kuwa wanaingiliana kazi zao.

  2. ni yeye aliyetoa tuhuma ambazo zinaendelea kuvuja ya kuwa mwenyekiti wa klabu ya waandishi kilimanjaro hilda ana uhusiano wa kimapenzi na mkurugenzi wa utpc karsan na kwamba mkurugenzi huyo anamtayarisha hilda kuwa makamu wa rais wa utpc.

  3. kikubwa zaidi ni pale alipowashawishi wafanyabiashara wa magendo rombo kwa ushirikiano na mwenyekiti wa halmashauri ya rombo tesha kumleta mwandishi wa itv kumchafua dc wa rombo. hii ni aibu kwa vile itv ni chombo kikubwa na cha kuheshimiwa.

  Ni muda muafaka kwa utpc na mct kuingilia kati swala hili kwa vile tasnia ya habari imechafuka.
   
 5. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 426
  Trophy Points: 180
  Hii ni baraa au laana kila kukicha ufisadi mwingine unaibuka na serikali imekaa kimya kama vile hakuna controler, mambo yanakwenda hovyo hovyo, hali hii mpaka lini??????????Tutaishia wapi Watanzania?????????

   
 6. m

  mams JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hii nchi, kama tumelaaniwa vile!
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  ndio hivyo wakuu
  no way out,ndio maisha tuliyojichagulia TZ

  ni wakati sasa wa kusimama na kusema big NO
   
 8. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  MKUU
  ndio maana wanasiasa hawataki kusikia issue ya AZIMIO LA ARUSHA ndilo lilikuwa AZIMIO pekee la kuvunja nguvu za akina untouchables
   
 9. MANI

  MANI Platinum Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,862
  Trophy Points: 280
  Mkuu kuna wakati Johnson Mbwambo aliwahi kusema nchi hii iko kwenye "auto pilot" kwa hiyo tusubiri pilot atakapo kaa kwenye kiti na kuanza kuindesha !
   
Loading...