SOMA RAI !
03.04.2008
Sasa Wizara ya Afya yatetea takataka zake
[FONT=Verdana, Arial, Helvetica, sans-serif]na mwandishi wetu
KATIKA kipindi kisichozidi wiki tatu, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imetoa taarifa mbili, zenye maelezo yanayojipinga yenyewe kwa yenyewe kuhusu ununuzi wa vitendanishi aina ya Capillus na kutuhumiwa kueleza uongo dhidi ya ubora wa mashine ya kupimia chembechembe za CD4 aina ya Cyflow.
Mkanganyiko huo umejitokeza baada ya wizara hiyo kutoa taarifa zinazopingana kuhusu msimamo wake juu ya matumizi ya vitendanishi vya Capillus na matokeo ya tathimini ya mashine ya Cyflow.
Na katika kilichoonekana kama kutaka kujisafisha, wizara hiyo imetumia mamilioni ya shilingi kununua kurasa za magazeti ili kutoa taarifa ya kuweka sawa mambo. Hata hivyo, taarifa hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Wilson Mkama, ina mambo yanaoonekana kupingana na taarifa iliyotolewa na waziri wake, Profesa David Mwakyusa
Taarifa aliyotoa Profesa Mwakyusa wiki mbili zilizopita, ilieleza kwamba Shirika la Afya Duniani (WHO) limeitaarifu wizara yake kwamba mashine hiyo haifai. Hata hivyo, katika tangazo la wizara la wiki hii, wizara inasema WHO haijawahi kuwaambia kuhusu mashine hiyo kwa sababu haijawahi kuifanyia tathmini. Tangazo lilisema kuwa WHO liliwashauri kuwa wafuate vigezo vya nchini ili kutumia au kutoitumia mashine hiyo.
Habari ambazo Rai imezipata kutoka Shirika la Afya Duniani, zinaeleza kuwa chini ya utaratibu wa shirika hilo, ili teknolojia mpya ya kitabibu iweze kutumika katika nchi yoyote, ni lazima iwe imefanyiwa tathimini tatu; kati ya hizo, tathmini moja iwe imefanyika katika nchi husika na mbili katika taasisi nyingine za kimataifa. Hata hivyo, Rai inayo taarifa kwamba mashine aina ya FactsCount iliyochaguliwa, haijawahi kufanyiwa tathmini hapa nchini.
Mbali ya maelekezo ya WHO, pia sheria za Tanzania zinataka hivyo. Kitu kinachowashangaza wengi ni kwamba wakati mashine ya Cyflow ililazimika kupitia katika chekeche mara tano katika kipindi cha miezi 12, mashine iliyopewa baraka (Facs Counter) haijawahi kutathminiwa nchini licha ya sheria kutaka kufanya hivyo.
Kwa mujibu wa sheria ya Bodi ya Maabara za Afya za Umma mwaka 1997, na tangazo la serikali namba 226 kifungu kidogo cha 2.5.2 (1)(v) linalotoa masharti ya matumizi ya kifaa chochote cha tiba, ni lazima kifaa chochote kipate tathmini moja ndani ya nchi, na moja nje ya nchi. Zaidi ya mashine 40 za Facts Count zinazotumika hapa nchini, hakuna hata moja iliyofanyiwa tathmini hapa nchini.
Shirika hilo la Afya duniani, limethibitisha kwamba tayari limekwishanunua mashine 100 aina ya iliyokatazwa Tanzania na kuzisambaza nchi mbali mbali duniani. Hivi sasa, India inaziondoa mashine zote za FactsCount na kuzibadilisha na Cyflow. Thailand ina mashine zipatazo 132 na zinafanya kazi kwa ufanisi mkubwa nchini humo. Katika taarifa yake wiki mbili zilizopita, Waziri wa Afya, alisema kwamba Cyflow, zinatumika katika nchi za Afrika tu.
Kwa upande wa vitendanishi aina ya Capillus,Wizara hiyo inakiri kwamba mwaka 2004, baada ya Serikali kuamua kupeleka huduma za upimaji wa VVU hadi vijijini iliamua kutafuta vitendanishi mbadala ambavyo havihitaji uhifadhi wa baridi, na kutangaza rasmi azma ya kuachana na Capillus mwaka 2006. Wakati akitoa taarifa yake wiki mbili zilizopita, Waziri wa Afya alisema wizara yake itaendelea kuzitumia Capillus kwa sababu imeandaa miundo mbinu ya kutosha. Hata hivyo, tangazo la Jumatano wiki hii katika magazeti mbali mbali, wizara hiyo hiyo imesema kuwa inaviondoa vitendanishi hivyo kwa sababu haina uwezo wa kuvitunza katika jotoridi la nyuzi kati ya mbili hadi nane kwa muda wote.
Katika ununuzi wa vitendanishi hivyo, Wizara ya Afya imeendelea kutoa kisingizio kwamba bado watumishi wake wapo katika mchakato wa mafunzo kuhusu matumizi ya vitendanishi vingine.
Vitendanishi hivyo ambavyo viliingizwa na wizara katika utaratibu mpya wa upimaji wa Virusi vya Ukimwi (New Algorithm) ni Unigold, SD Bioline na Determine. Pia wizara hiyo inaeleza kuwa ingawa mafunzo hayo yalipangwa kufanyika mwaka jana, Wizara hiyo, ilirefusha muda wa utoaji wa mafunzo hayo kwa kisingizio kwamba baada ya kutangazwa kwa kampeni ya kitaifa ya upimaji VVU utaratibu wa utoaji mafunzo pia ulivurugika. Kwa mujibu wa wizara, maelezo hayo ndiyo yaliyotoa mwanya wa kuendelea kutumia vitendanishi hivyo nchini.
Taarifa ya Wizara ya Afya inaeleza kuwa Julai 12 mwaka jana, Bohari Kuu ya dawa nchini (MSD) iliagizwa kununua Kits 21,896 za vitendanishi vya Capillus zenye thamani ya takriban Sh. bilioni nne kwa kufuata taratibu za sheria za ununuzi. Hata hivyo maelezo hayo yamezua mkanganyiko mwingine kwani wizara iliagiza vitendanishi hivyo vinunuliwe wakati vilishaondolewa katika 'Nationa Algorithm'.
Kwa maelezo mengine ni kwamba vitendanishi hivyo vilinunuliwa huku vikiwa havijasajiliwa na Bodi ya Maabara za Umma (PHLB), jambo ambalo ni ukiukwaji mkubwa wa sheria ya ununuzi wa vifaa vya afya.
Mkanganyiko mwingine unaojitokeza ni pale Wizara ya Afya ilipoamua kununua idadi kubwa ya vitendanishi hivyo na kuviingiza nchini kwa awamu saba kwa kisingizio kwamba ilifanyika hivyo ili kulinda ubora na uhai wa vitendanishi hivyo kwa sababu ya hifadhi yake. Pamoja na kwamba jambo hilo ni ukiukwaji wa taratibu za sheria za ununuzi, Rai imekuwa ikipigia kelele suala hili la uwezo wa nchi kutunza vitendanishi hivi ambavyo vinahitaji kutunzwa kwenye nyuzi joto mbili hadi nane kwa wakati wote kwa mujibu wa maelekezo ya Shirika la Afya Duniani aliyotumiwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo mwanzoni mwa kampeni ya kitaifa ya upimaji wa VVU.
Baadhi ya maofisa wa Wizara ya Afya wameliambia Rai kuwa lengo la kununua vitendanishi hivyo na kuviingiza nchini kwa awamu kulitokana na hali halisi ya hapa nchini kwamba hapakuwapo na vifaa vya kutosha vya kutunza vitendanishi hivyo, jambo ambalo limeendelea kuwa tatizo kubwa hadi leo.
Maofisa hao wamesema kwa kuwa hali ya utunzaji wa vitendanishi hivyo ilikuwa ikijulikana tangu awali, hapakuwapo haja ya kusaini mkataba wa kununua Kits nyingi kwa mkupuo kisha ziletwe nchini kwa awamu saba. Baadhi ya vyanzo vyetu vya habari vilieleza kuwa mkataba huo ulikuwa na lengo la kutumia kisingizio cha kampeni ya kitaifa ya upimaji wa VVU kununua idadi kubwa ya vitendanishi hivyo.
Uchunguzi uliofanywa na Rai kwa siku kadhaa umebaini kuwa vitendanishi hivyo vimekuwa vikiagizwa
nchini na kuhifadhiwa kwa muda katika maghala ya MSD kisha kusambazwa mikoani bila kuzingatia
masharti ya kuvihifadhi katika nyuzi joto kati ya mbili hadi nane.
Taarifa ya sasa ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayoeleza kwamba baada ya vitendanishi (capillus) vinavyotarajiwa kuingizwa nchini mwezi huu, Serikali haitanunua vitendanishi vingine vya aina hiyo, inapingana na taarifa iliyotolewa na wizara hiyo hiyo wiki chache zilizopita iliyokuwa ikielezaa kuwa kipimo cha Capillus ni bora. Hivyo vitaendelea kutumika nchini. Taarifa hiyo iliongeza kwamba wizara hiyo ina vifaa vya kutosha vya kutunza vitendanishi hivyo.[/FONT]
tumepata e-mail leo:
"...We must realise that there is a serious problem but this is as far as the people are ignorant. The political leadership is usually misled. Once the information is public,even the president will be forced to perform his constitutional duties.
We had similar situations in Kenya which need a whistle blower.
Yesterday, the meeting between the some four selected journalists ended up not being a press conference!!
The minister wanted to find a way of cover up since the matter is very serious there. He wants to bribe the journalist to 'go slow'. He even wanted to find out the source of original report.You can see he is fully involved in the corrupt deal.
Its important to note that a similar scandal was reported by ThisDay recently but on Financial scandal at the central bank of Tanzania..."
"...Concerning Mr Rajani of Biocare,I understand the man lost his wife a few months ago. The funeral was attended by almost the whole Cabinet including the prime minister. This shows that the man has used his money in many ways than one. We must therefore scare away his seasonal political friends by exposing the matter..."