Ufisadi wa CCM na kampuni ya A1 Outdoor | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa CCM na kampuni ya A1 Outdoor

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by n00b, Aug 24, 2010.

 1. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Wakuu,

  Mnaweza kuwa hamwelewi CCM ina-operate vipi au wengine mnafahamu zaidi yangu lakini sasa naona mwenzenu yamenikera mpaka nimeamua niyaseme.

  Ndiyo, inasikitisha kuona Usalama wa Taifa (wanahusika katika hili) wako kimya wakati siasa zikitumika na kulitumbukiza taifa katika risk kubwa kiwango ambacho nitakielezea chini hapa.

  Kwa mlio jijini Dar es Salaam nadhani mshayaona matangazo ya CCM ambayo aidha yamewekwa katika nguzo zote za barabarani au kwenye mabango makubwa (yote ni ya ZADOK - A1 Autdoor).

  Ukweli ni kuwa haya matangazo CCM wamelipia printing tu, kama kawaida Zadok amejipendekeza kwa CCM ili aendelee kufanya upuuzi wake kushikilia soko la matangazo hasa ya barabarani. Amekuwa akifanya hivi kipindi kirefu na hata ukiangalia design ya matangazo yenyewe iko very poor na kibaya zaidi wametumia picha za JK akiwa kama rais kwenye matangazo na sio akiwa kama mwana CCM, huwezi kumchukua JK akikagua Jeshi la Tanzania kwenye shughuli ya kitaifa kisha ukatengeneza bango ati CCM inaimarisha amani. Ni upuuzi at its best.

  Sasa, kwa ofa hii kwa CCM, wamejisahau kabisa kumfuatilia huyu jamaa ambaye amekuwa beneti nao na kusababisha barabara toka Uwanja wa ndege ikiwa giza, wamefumbwa macho. Fikiria barabara ambayo inawaleta watalii kibao kulitembelea taifa kuanzia Jet mpaka TAZARA ni giza tupu zaidi ya miezi mitatu sasa. Usalama wa Taifa wanalichukulia suala hili kuwa dogo?

  Nguzo zenyewe za taa ni low quality, zinaanguka ovyo, hakuna wa kumsema. Taa nazo zikiwaka huwa zina mwanga mdogo sana kitu ambacho husababisha ajali zisizokuwa za lazima.

  Jamaa hawa wamekuwa na kiburi sana kiasi wanaweka mabango yanayo-distruct mtu unapokuwa una-drive na mabango ambayo wanajua yangetakiwa kuondolewa ndiyo wanaweka picha za CHAGUA JK, CHAGUA CCM. Hapo watawala wanakuwa wamezibwa kabisa masikio na macho. Wanapita wakikenua na kufurahia tu.

  Natambua kuwa Halmashauri zetu hazina uwezo wa kuendesha kila kitu na ndo maana imekuja PPPA, lakini ni lazima iwepo Public Consultation kabla ya kupata partners bomu kama hawa. Ni watu wasiolitakia taifa mema kabisa na wapo kifisadi zaidi.

  Mwanzoni nilikuwa na imani sana na Zadok (wa A1 Outdoor) lakini kwa low quality hii na kwa kujipendekeza kwake kwa chama tawala naanza kukosa imani naye pamoja na Mall yake iliyokwama; najua anatafuta namna ya kujikwamua baada ya mkataba wake na Zaina kubuma.

  Kama Masasi Signs wamewekewa mpinzani katika kazi (si upinzani wa ubaya bali kibiashara), kwanini A1 Outdoor wasiwe na mpinzani? Huwezi kulinganisha mitaa ya ovyo waliyoiweka hawa jamaa na zile za Sam Nujoma hata kidogo.

  Wakuu, nakereka sana kwa siasa kusababisha mambo mengi kukwama, nalazimika kuandika JF nikiamini huenda nikasikika na watawala kuchukua hatua.

  Shukrani
   
 2. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Minguzo yenyewe inaanguka ovyo:

  [​IMG]

  Hawa jamaa wamechangia kwa kiwango kikubwa Dar es Salaam kuwa jiji la giza
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  Ukiangalia tulishajadili juu ya hili nadhani mwaka 2008 (kama sio 2009).

   
 4. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Najiluliza kwa nini ccm wanahangaika kujitangaza kiasi hiki kama kweli wamefanya mazuri. It shows hawajiamini na wanahaha huku wakikumbatiana na makampuni ya namna hii kuendeleza ukiritimba. Enough is enough. It is time to vote them out
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,903
  Likes Received: 1,330
  Trophy Points: 280
  Mimi Pamoja na hayo lakini hili la kufanya hila ya kuwaondoa wagombea walio weka pingamizi zidi ya CCM wao ndio wanaondolewa na TUME na Usalama wa Taifa wamekaa kimya,inauma sana sijui wanataka kitu gani kitokee baada ya 31 tutaona kama kutakuwa na atakaye pona
   
 6. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Ni aibu...popote duniani,serikali mbovumbovu ikishikiliwa na wafanyabiashara lazima ianguke..wafanyabiashara hawana "political interest" rather wana "profitical interest"...ccm bado hawajajua kutofautisha hapo...
   
 7. dkims

  dkims Senior Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sasa ile bil 40 ccm walisema ni kwaajili ya kampeni za raisi wanazitumia wapi????????
   
 8. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aiiiiiiiiiiiiissssse! CCM inaila hiyo kampuni au kampuni inaila kampuni....oh no KUMBE NI WATZ tunaliwa!!!:confused2:
   
 9. G

  GEOMO Senior Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Naomba kujuzwa mmiliki halisi wa hiyo kampuni. Usishangae inamilikiwa na wakuu wako wa nchi huyo unae muona ni mmiliki akawa ni msimamizi tu!!?
   
 10. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,468
  Trophy Points: 280
  tatizo sio matangazo ya mabango..
  tatizo ni coverage ya tv kwa wapinzani....
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Haya mengine tunayatafuta huko yaliko lala yanaishia kutuongezea kushuka kwa presha bila sababu. Kuna mambo yanawezekana bila nguv za hawa wafanyabiashara ambao watataka kurudisha hela zao kwa kufanya sub standard jobs in the future.
   
 12. Bu'yaka

  Bu'yaka JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 80
  Ulosema yana mantiki, lakini kila nikiona nembo yako ya mtu anapiga sarakasi huku anaachia vikimba naona kama na wewe si mtu wa kuchukuliwa seriously. Labda ungeibadilisha.
   
 13. n00b

  n00b JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 952
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 60
  Walau hii leo taa wamezi-fix na zinafanya kazi kadhaa kuanzia Jet mpaka Vingunguti. Kumbe kelele hizi wakati mwingine zinafanyiwa kazi?
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Aug 26, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Kampuni ya matangazo ya outdoor ya jijini Dar es Salaam imefanya uharibifu mkubwa katika barabara ya Morogoro eneo la jangwani.

  Kampuni hiyo ambayo imepewa tenda na ccm/ikulu kuweka mabango ya mgombea uraisi wa ccm, imekata miti mingi iliyokuwa imepandwa kandokando ya barabara ya Morogoro, ili mabango ya ccm yaweze kuonekana kwa umbali mrefu. Miti hiyo ambayo ilipandwa na wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika juhudi yao ya kutunza mazingara na kuweka kivuli kandokando ya barabara hiyo, imehujumiwa vibaya na ccm na outdoor, na huenda uhabifu huu ukaendelea kufanyika katika barabara nyingine nyingi.
   
 15. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #15
  Aug 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Aisee hii haivumiliki. Ina maana huko Dar hakuna vikundi vya kutetea mazingira walau vikaandamana, au kushtaki kabisa?
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Aug 26, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Aiseeee
   
Loading...