Ufisadi Nzito Wa Rais Kibaki's Government

Kenyan-Tanzanian

JF-Expert Member
Nov 7, 2006
302
2
Raila fanya hima utusafishie huu ufisadi ambao Githongo alifichua...

Wakuu, zikiwa zimesalia sikuu tisa tuu tuingie kwenye mabox za kuamua political future ya Kenya, pokeeni hizi ripoti kali on kashfaa nzito ya ufisadi wa serikali ya Rais Mwai Kibaki zilizofichuliwa na Bw. John Githongo. Githongo aliyekuwa mkuu wa idara ya kupambana na ufisadi Kenya, alitorokea UK baada ya maisha yake kuwekwa hatarani pale alipofichua ufisadi nzito ndani ya serikali ya Rais Kibaki unaotekelezwa na mawaziri wa Kibaki. Makandarasi yalitolewa kwa kampuni isiyojulikana wanaoimiliki ya karibu Billioni 20 za Kenya ili eti kununua vifaa zaidi za kivita za kisasa (kwani Kenya inapigana au inapanga kupigana na nani?)

Alipojaribu kuripoti haya kwa Rais, kwa mujibu wake mwenyewe, aliombwa awachane na hayo kwajili "haya yalikuwa mambo ya kawaida". Githongo ni mKikuyu kama Kibaki na Mawaziri fulani wenye usemi mkubwa serekalini wanaogombea viti vyao tena kwa tikiti ya PNU ni wa jamii yake Githongo na Rais na wanamuona kama msaliti aliyeiua serikali "yao" from within badala ya kutumbukiza tumboni mshahara mkubwa ambaye ofisi aliyokuwaakishikilia serekalini ulikuwa unampa kila mwezi.

Lakini kwa maelfu ya wananchi na Upinzani, Githongo ni hero ambaye alionyesha kwa maneno yake mwenyewe kwamba " mwizi ni mwizi hata awe wa kabila yako au ndugu yako." Inapendeza kufahamu kwamba Raila Odinga ametangaza hadharani mbele ya umati wa waKenya wasiopungua elfu hamsini huko Kisumu kwamba Githongo atarudi nyumbani pindi ODM itakaponyakua ushindi azidikusaidia vita dhidi ya Mafisadi wa Kenya.

Ripoti ya Githongo nipo nayo hapa lakini ni kubwa mno na inapita uzito wa attachment unaokubaliwa na JF Admin.

Webpages za information juu ya ripoti yenyewe hizi hapa:

http://216.180.252.4/archives/?PHPSESSID=21d00565e0a0db9838cfd14aeaa2b106&dmy=16%2F12/2007

http://216.180.252.4/archives/?mnu=details&id=1143978974&catid=4


http://politics.nationmedia.com/inner.asp?sid=1060

http://kumekucha.blogspot.com/2007/10/john-githongo-i-knew-too-much.html
 
Back
Top Bottom