Ufisadi na rushwa zinaanza kurudi taratibu katika ofisi za serikali kwa speed hi hali inatisha

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
790
1,264
Leo nilienda katika ofisi za manispaa Fulani hapa Dar kufuatilia leseni ya biashara

Yani jamaa hata aogopi ananiambia ukilipia leseni hiyo elfu 81 haupati hadi ulipe na service levy elfu 50 ila ukinipa 30 au 20 nitakufanyia mpango upate leseni yako

Nikamuangalia moyoni nikasema ni bora nisipate hiyo leseni kuliko kukupa elfu 30 uitie mfukoni kwako

Baadae katika mizungoko yangu mulemule manispaa nikakutana na jamaa ameshika hizo lisiti kibao mkononi ambazo huzipati hadi ulipe hiyo kodi ya service levy

Nikasikitika sana moyoni mwangu nikaona yani hapa kodi ya serikali imeshapigwa na raia pia wameshapigwa

Ukweli ni kwamba hi kodi ya service levy kuwekwa sehemu ya kuchukulia leseni ya biashara yani ukishalipia leseni haupati hadi ulipe hi kodi ni kuwatengenezea watumishi mianya ya kuchukua rushuwa
 
Ila watanzania tuna SHIDA na MATATIZO makubwa mnooo.

Wengi wetu ni WEZI, WADHULUMAJI, MAFISADI ( wengine hatujapewa nafasi tu ) na tumejaa WIVU mkubwa.

Siku zote kazi yetu Ni kuombeana MABAYA na KUFURAHIA mabaya ya watu.

Na saikolojia hii, Magufuli aliijua vizuri "ukitaka KUWAFURAHISHA Watanzania wawe pambana na Wenye nacho na kuwashambulia hadharani.

Anza na Watumishi na MATAJIRI.

Ukifanya hivyo, hutakuwa na haja ya kutafuta watu was kukushangilia watakuwa wanakuja wenyewe.

=======

Anyway, wewe umeenda Manispaa kutafuta Leseni. Kwa utaratibu Ni kwamba inakubidi upewe form ili uipeleke kwa wahusika katika eneo ambalo biashara yako itakuwa kuanzia VEO, Ardhi, Afisa Afya n.k ).

Baada ya ukaguzi ndio wata recommend upewe Leseni au Lah. Lakini wabongo wengi wanapenda shortcut, kupewa Leseni juu kwa juu.

Pili, kulingana na aina ya biashara yako inaweza kuwa unatakiwa kulipa Leseni ya 300,000 ( ambayo kwa kawaida itaathiri mpaka TRA).

Nani hajui kuwa huwa mna-negotiate na watu wa Leseni kiujanja na kulipa pesa ndogo. Mtu ana bakery lakini kakata Leseni ya Tea room.

Tatizo wabongo kila mtu mjanja mjanja na kila mtu analaumu mwenzie lakini HAKUNA MSAFI.

Screenshot_2022-04-01-18-43-11-425_com.adobe.reader.png
 
Waswahili wanasema, ukisusa wenzio twala. Mkuu ni haki yako kuwa mzalendo, lakini kaa ukijua uzalendo hauleti chakula mezani. Kaa kwanza hapo nje upigwe jua kidogo, baadae utatoa tu.
Pole lakini
 
Leo nilienda katika ofisi za manispaa Fulani hapa Dar kufuatilia leseni ya biashara

Yani jamaa hata aogopi ananiambia ukilipia leseni hiyo elfu 81 haupati hadi ulipe na service levy elfu 50 ila ukinipa 30 au 20 nitakufanyia mpango upate leseni yako

Nikamuangalia moyoni nikasema ni bora nisipate hiyo leseni kuliko kukupa elfu 30 uitie mfukoni kwako

Baadae katika mizungoko yangu mulemule manispaa nikakutana na jamaa ameshika hizo lisiti kibao mkononi ambazo huzipati hadi ulipe hiyo kodi ya service levy

Nikasikitika sana moyoni mwangu nikaona yani hapa kodi ya serikali imeshapigwa na raia pia wameshapigwa

Ukweli ni kwamba hi kodi ya service levy kuwekwa sehemu ya kuchukulia leseni ya biashara yani ukishalipia leseni haupati hadi ulipe hi kodi ni kuwatengenezea watumishi mianya ya kuchukua rushuwa
Hilo neno RUSHUWA kama mbadala wa rushwa nimelisikia kitambo sana.
 
Nnachojua mimi service levy inapigwa percent kadhaa toka kwenye mauzo ghafi. Sasa wewe unaenda kutafta leseni si ndo kwanza unafungua biashara ama? Hiyo levy watapiga kwenye mapato yepi?
 
Kama service levy ndio ipo hivyo basi tunaibiwa

Niliwauliza hi biashara ni mpya sasa ni huduma zipi mlizonipa hadi mnidai service levy jibu lao lilikuwa ni lilelile kuwa haupati Leseni yako hadi ulipe service levy

Na naamini hiyo sheria ya service levy hata wao wanaijua ila wanatengeneza mazingira ya kupewa rushuwa
 
Ila watanzania tuna SHIDA na MATATIZO makubwa mnooo.

Wengi wetu ni WEZI, WADHULUMAJI, MAFISADI ( wengine hatujapewa nafasi tu ) na tumejaa WIVU mkubwa.

Siku zote kazi yetu Ni kuombeana MABAYA na KUFURAHIA mabaya ya watu.

Na saikolojia hii, Magufuli aliijua vizuri "ukitaka KUWAFURAHISHA Watanzania wawe pambana na Wenye nacho na kuwashambulia hadharani.

Anza na Watumishi na MATAJIRI.

Ukifanya hivyo, hutakuwa na haja ya kutafuta watu was kukushangilia watakuwa wanakuja wenyewe.

=======

Anyway, wewe umeenda Manispaa kutafuta Leseni. Kwa utaratibu Ni kwamba inakubidi upewe form ili uipeleke kwa wahusika katika eneo ambalo biashara yako itakuwa kuanzia VEO, Ardhi, Afisa Afya n.k ).

Baada ya ukaguzi ndio wata recommend upewe Leseni au Lah. Lakini wabongo wengi wanapenda shortcut, kupewa Leseni juu kwa juu.

Pili, kulingana na aina ya biashara yako inaweza kuwa unatakiwa kulipa Leseni ya 300,000 ( ambayo kwa kawaida itaathiri mpaka TRA).

Nani hajui kuwa huwa mna-negotiate na watu wa Leseni kiujanja na kulipa pesa ndogo. Mtu ana bakery lakini kakata Leseni ya Tea room.

Tatizo wabongo kila mtu mjanja mjanja na kila mtu analaumu mwenzie lakini HAKUNA MSAFI.
Umeongea mengi ila hayana msingi wowote Mimi nimezungumzia wafanya biashara wa kawaida viduka vya mitaani ndio wanao kutana na hizo kadhia

Mimi leseni nilienda kumchukula wife amefungua kibiashara cha kawaida tu mtaani hata ukienda manispaa wafanya biashara utakao kutana nao ni hawa hawa wa mitaani wenye viferemu vya kuuza maji ,juice ya viduka vya kawaida tu

Hata hiyo kuwambia walipe elfu 81 kisha walipe elfu 50 ya service levy ni kuwakandamiza tu na ndio maana wengi wanaona ni bora atoe rushuwa ya elfu 20 achukue hiyo leseni
 
Leo nilienda katika ofisi za manispaa Fulani hapa Dar kufuatilia leseni ya biashara

Yani jamaa hata aogopi ananiambia ukilipia leseni hiyo elfu 81 haupati hadi ulipe na service levy elfu 50 ila ukinipa 30 au 20 nitakufanyia mpango upate leseni yako

Nikamuangalia moyoni nikasema ni bora nisipate hiyo leseni kuliko kukupa elfu 30 uitie mfukoni kwako

Baadae katika mizungoko yangu mulemule manispaa nikakutana na jamaa ameshika hizo lisiti kibao mkononi ambazo huzipati hadi ulipe hiyo kodi ya service levy

Nikasikitika sana moyoni mwangu nikaona yani hapa kodi ya serikali imeshapigwa na raia pia wameshapigwa

Ukweli ni kwamba hi kodi ya service levy kuwekwa sehemu ya kuchukulia leseni ya biashara yani ukishalipia leseni haupati hadi ulipe hi kodi ni kuwatengenezea watumishi mianya ya kuchukua rushuwa
Kwamba unapeenda kulipa.. bora uumpe huyo mwamba apeleke nyumban watoto wapate mlo wa siku.. kuliko kwendaa kuipeleka hazina halaf zikagawaanwa na wenye nchi yao.. kwamba naniliu imerud kwa wenyew.. hahah..
 
Acha urudi..mana hao viongozi wa juu hayo madili wanayoyapiga ungejua bora ungehama nchi tu..hakuna mzalendo nchi ishauzwa hii..wanasiasa ndio wameiharibu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mi ninachojua kama lesen yako imeisha ukienda ku re new ndio wanataka ulipe hiyo service levy, mi niliambiwa ni elf 36 kwa mwaka, akasema nadaiwa miaka mitatu hivyo aniandikie mmoja nimtoe kidogo, nikamwambia aniandikie hiyo miaka mitatu nalipa, akanipa control namba nikalipia nikachukua lesen yangu nikasepa! Watanzania wengi tunakosa nafas za kuiba ndio maana uzi za hivi kulalamika haziishi! Hivi ukiambiwa service levy sh flan ukilipa na kusepa huyu atapata wapi hiyo rushwa? Tatizo ni kupenda njia za mkato
 
Bado kidogo tuuondoe mfumo wa control number, tulipie huduma kwa akaunti za kila taasisi…. watu wamalizie mijengo yao.
Nilienda Tanesco mkuranga, nikapewa control number imeandikwa kwa mkono. Mpaka nilishtuka mno,
 
Back
Top Bottom