Hi kodi ya manispaa inayoitwa service levy haipo sawa irekebishwe

Wazolee

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
4,127
Reaction score
4,825
Leo nimegundua kwa nini watanzania wengi wanakimbia kulipa kodi
Kuna mambo mengi hayapo sawa na wajasilia mali wengine wanaamini ukijifanya mzalendo wa kulipa kodi basi hako kabiashara kako utakafunga

Wiki mbili tatu nilianzia TRA katika michakato yangu ya kufungua biashara nikakadiriwa kodi 150000 kwa mwaka
Tatizo likaanzia hapo baada ya kuambiwa hadi ukifika mwezi December niwe nimelipa kodi yate wakati mimi biashara nimeanza mwezi wa 9 kwa nini nilipe kodi yote kana kwamba nimeanza biashara January badala ya kulipia robo ya mwisho tu
TRA wakaniambia huo ndio utaratibu wa nchi yetu haijalishi biashara umeanza link

Leo nimeenda manispa kufuatilia leseni ya hiyo biashara yangu walipo maliza kukagua documents zangu nikandikiwa nikalipie leseni tshs 81000
Nilipo maliza kulipia nikapeleka slip ya benk sehemu husika ili nipewe lisiti ya manispaa niende chumba cha kuchukua leseni
Nikaambiwa huwezi kupata leseni hadi ulipe SERVICE LEVY tshs elfu 50 kwa kweli hichi kitendo kilinikera sana

Nikauliza sasa mbona hamkuniambia tangu mwanzo kuhusu hi kodi ya service levy mnakuja kuniambia wakati nimeshamaliza michakato yote ya leseni nilaambiwa ndi hivyo lipia elfu 50 ya service levy tukupe leseni yako

Nikagundua hi nchi ukijifanya wewe ni mzalendo na wao wanakukomoa ili ukome na uzalendo wako

Hongera zenu Temeke manispaa kwa kuwawekea mazingira magumu wajasilia mali wazalendo wanao penda kulipa kodi
 
Mzee baba huo ndio ulimwengu wa biashara na ndio maana sio kila mtu anaweza kufanya biashara.

Ina mateso ya kutosha,kukosa usingizi usiku kucha,kuwaza namna ya kutoboa(washindani/strategy),kodi etc.

So ukiingia kwny biz umeingia vitani rasmi,welcome to the world.
 
hii service levy ingewekwa wazi tujue! zaidi ya hapo tutahesabu SERIKALI ndio WANAWAIBIA wanyonge
 
Leo nimegundua kwa nini watanzania wengi wanakimbia kulipa kodi
Kuna mambo mengi hayapo sawa na wajasilia mali wengine wanaamini ukijifanya mzalendo wa kulipa kodi basi hako kabiashara kako utakafunga
Wiki mbili tatu nilianzia TRA katika michakato yangu ya kufungua biashara nikakadiriwa kodi 150000 kwa mwaka
Tatizo likaanzia hapo baada ya kuambiwa hadi ukifika mwezi December niwe nimelipa kodi yate wakati mimi biashara nimeanza mwezi wa 9 kwa nini nilipe kodi yote kana kwamba nimeanza biashara January badala ya kulipia robo ya mwisho tu
TRA wakaniambia huo ndio utaratibu wa nchi yetu haijalishi biashara umeanza link
Leo nimeenda manispa kufuatilia leseni ya hiyo biashara yangu walipo maliza kukagua documents zangu nikandikiwa nikalipie leseni tshs 81000
Nilipo maliza kulipia nikapeleka slip ya benk sehemu husika ili nipewe lisiti ya manispaa niende chumba cha kuchukua leseni
Nikaambiwa huwezi kupata leseni hadi ulipe SERVICE LEVY tshs elfu 50 kwa kweli hichi kitendo kilinikera sana
Nikauliza sasa mbona hamkuniambia tangu mwanzo kuhusu hi kodi ya service levy mnakuja kuniambia wakati nimeshamaliza michakato yote ya leseni nilaambiwa ndi hivyo lipia elfu 50 ya service levy tukupe leseni yako
Nikagundua hi nchi ukijifanya wewe ni mzalendo na wao wanakukomoa ili ukome na uzalendo wako
Hongera zenu Temeke manispaa kwa kuwawekea mazingira magumu wajasilia mali wazalendo wanao penda kulipa kodi
[/QUOTE serekali itoe elimu kwa wale wanao taka kufungua biashara iorodheshe njia zote za kulipia Kodi mpaka kupata leseni ya biashara.Bila elimu tata lia wengi tuta umizwa na virushwa vya kutenge neza.
 
Makadirio ya kodi yangawanywa awamu nne hivyo 150000 gawanya kwa nne Ni 37500 ndicho kiasi unachotakiwa kulipa kitu kingine unachopaswa kujua makadirio unajikadiria mwenyewe na sio kukadiriwa na tra ndio maàna wanakupa fomu ujaze Kama ukijaza vibaya makadirio yatakuwa juu Kama umelipia leseni kafungue biashara wakija kukagua leseni waonyeshe risiti za biashara uliyolipia service levy na leseni Ni vitu viwili tofauti
 
kufanya biashara nchi hii ni ngumu sana, wafanya biashara wote! kila mmoja ana mbinu zake za kukwepa kodi
 
TRA na manispaa wanafanya mambo muhimu anayotakiwa ajue mwananchi katika kufanya biashara kama siri, hakuna uwazi kabisa wa mtu kujua anatakiwa alipe nini ili aanze biashara, na ukianza biashara kila mwaka unakadiriwa kodi mpya wao wana amini kuwa kila mwaka unatengeneza faida kubwa zaidi ya iliyo pita, wamekaa maofisini kukadiria tu mapato hawazunguki kwa wafanya biashara kuona uhalisia. Ndio maana wengi wamfeunga biashara zao au wanaendesha kiujanja tu.
 
Yani hawa manispaa wana mambo ovyo sana.kiukweli nimelipia leseni toka febr,adi leo sijapata na kira nikienda saound.hua najiuri kwa nini hawatoa lesen badara yake unatumia risit pekee?hayo hozo tozo ndo usisema.utakuta ana kigori)kidogo rakina utakuta TRA,MANISPAA,ZIMA MOTO,TAKATAKA,SEVC REVI CJUI,NK yaani serikari kwenya kodi badi mpo juu mno.UNATUBANI WANANCHI WENU.au mnataka bado tuwe machinga kumwaga bidhaa chini?
 
Sidhani Kama Ni sahihi kukatwa hiyo Kodi kabla ya huduma kutolewa....
 
Makadirio ya kodi yangawanywa awamu nne hivyo 150000 gawanya kwa nne Ni 37500 ndicho kiasi unachotakiwa kulipa kitu kingine unachopaswa kujua makadirio unajikadiria mwenyewe na sio kukadiriwa na tra ndio maàna wanakupa fomu ujaze Kama ukijaza vibaya makadirio yatakuwa juu Kama umelipia leseni kafungue biashara wakija kukagua leseni waonyeshe risiti za biashara uliyolipia service levy na leseni Ni vitu viwili tofauti
Hi ishu naijua na ndio maana nilibishana sana na yule Dada kwamba haiwezekani ni lipe kodi yote ya mwaka wakati biashara imeanza mwezi wa 9 ambayo ni robo ya mwisho katika mwaka
Akaniambia system ya TRA ndio imesetiwa hivyo haijalishi biashara umeanza lini unatakiwa ulipe kodi yote ya mwaka
Lakini kwa kuwa document yao ninayo na inaonyesha biashara nimeanza lini nitaenda kwa meneja wao kutoa malalamiko yangu
 
kuna kituo cha malalmiko kimefunguliwa kipo samora baada ya jengo la extelcom kuna watu vilaza hakuna system iliyosetiwa hivyo au mwone meneja wake au wamepata kazi kwa kushikwa mkono ndio maana kila kitu anakaririr
 
Makadirio ya kodi yangawanywa awamu nne hivyo 150000 gawanya kwa nne Ni 37500 ndicho kiasi unachotakiwa kulipa kitu kingine unachopaswa kujua makadirio unajikadiria mwenyewe na sio kukadiriwa na tra ndio maàna wanakupa fomu ujaze Kama ukijaza vibaya makadirio yatakuwa juu Kama umelipia leseni kafungue biashara wakija kukagua leseni waonyeshe risiti za biashara uliyolipia service levy na leseni Ni vitu viwili tofauti
Acha kupotosha mkuu, kiwango cha mwisho cha kodi kwa tra ni 150,000 tena kwa mfanya biashara mdogo kabisa,kama kiduka, sehemu za kunyorea, wanakupa fomu ujaze? Pale atakuuliza aina ya biashara, kiwango cha mtaji ulichonacho, na makisio ya mauzo, halafu hata uende leo bado miezi miwili mwaka kuisha wao wanakadilia tu hesabu ya mwaka, laki na 50,na kufikia dec 31,lazima uwe umeilipa yote, na January uende tena kwa makadilio mapya, Ndio maana ukianzisha biashara miezi hii lazima ukubali tu kuumia, au uanze tu bila TIN, wala leseni then, january ndio uanze upya!!! Sana sana leseni ndio wanaweza kukusumbua miezi hii, ila wakikukuta wanakupiga faini tu,. Ukisha kuwa na risiti ya kulipia leseni tu umemaliza
 
Hiyo service levy nilikutana nayo nilipo enda kuchukua leseni TMK nikaambiwa ni kodi ya huduma
Wale wanao jua jamani watufafanulie hi huduma anayo pewa mfanya biashara baada ya kulipa hi kodi ni huduma gani?

Maana yawezekana ukishalipa unaweza ukajikuta unahudumiwa kwa kuletewa juice na maziwa ya kopo kila mwezi
 
Hi ishu naijua na ndio maana nilibishana sana na yule Dada kwamba haiwezekani ni lipe kodi yote ya mwaka wakati biashara imeanza mwezi wa 9 ambayo ni robo ya mwisho katika mwaka
Akaniambia system ya TRA ndio imesetiwa hivyo haijalishi biashara umeanza lini unatakiwa ulipe kodi yote ya mwaka
Lakini kwa kuwa document yao ninayo na inaonyesha biashara nimeanza lini nitaenda kwa meneja wao kutoa malalamiko yangu
Mkuu hata uende kwa kamishina hawezi kukusaidia hilo kwani ndio mfumo wao wa kodi umepangwa hivyo!! Wewe chakufanya kama umeshapata TIN namba, na leseni fungua tu biashara yako, January ndio uwaibukie, kuwa nimekuja ndio nataka kufungua biashara, watu ndio hufanya hivyo, kufungua biashara mwishoni mwa mwaka kodi lazima ikuumize
 
Acha kupotosha mkuu, kiwango cha mwisho cha kodi kwa tra ni 150,000 tena kwa mfanya biashara mdogo kabisa,kama kiduka, sehemu za kunyorea, wanakupa fomu ujaze? Pale atakuuliza aina ya biashara, kiwango cha mtaji ulichonacho, na makisio ya mauzo, halafu hata uende leo bado miezi miwili mwaka kuisha wao wanakadilia tu hesabu ya mwaka, laki na 50,na kufikia dec 31,lazima uwe umeilipa yote, na January uende tena kwa makadilio mapya, Ndio maana ukianzisha biashara miezi hii lazima ukubali tu kuumia, au uanze tu bila TIN, wala leseni then, january ndio uanze upya!!! Sana sana leseni ndio wanaweza kukusumbua miezi hii, ila wakikukuta wanakupiga faini tu,. Ukisha kuwa na risiti ya kulipia leseni tu umemaliza
sidhani hata kama una biashara mi nafanya biashara na ninapambana nao kila siku labda wewe umezoea kupotoshwa
 
Leo nimegundua kwa nini watanzania wengi wanakimbia kulipa kodi
Kuna mambo mengi hayapo sawa na wajasilia mali wengine wanaamini ukijifanya mzalendo wa kulipa kodi basi hako kabiashara kako utakafunga

Wiki mbili tatu nilianzia TRA katika michakato yangu ya kufungua biashara nikakadiriwa kodi 150000 kwa mwaka
Tatizo likaanzia hapo baada ya kuambiwa hadi ukifika mwezi December niwe nimelipa kodi yate wakati mimi biashara nimeanza mwezi wa 9 kwa nini nilipe kodi yote kana kwamba nimeanza biashara January badala ya kulipia robo ya mwisho tu
TRA wakaniambia huo ndio utaratibu wa nchi yetu haijalishi biashara umeanza link

Leo nimeenda manispa kufuatilia leseni ya hiyo biashara yangu walipo maliza kukagua documents zangu nikandikiwa nikalipie leseni tshs 81000
Nilipo maliza kulipia nikapeleka slip ya benk sehemu husika ili nipewe lisiti ya manispaa niende chumba cha kuchukua leseni
Nikaambiwa huwezi kupata leseni hadi ulipe SERVICE LEVY tshs elfu 50 kwa kweli hichi kitendo kilinikera sana

Nikauliza sasa mbona hamkuniambia tangu mwanzo kuhusu hi kodi ya service levy mnakuja kuniambia wakati nimeshamaliza michakato yote ya leseni nilaambiwa ndi hivyo lipia elfu 50 ya service levy tukupe leseni yako

Nikagundua hi nchi ukijifanya wewe ni mzalendo na wao wanakukomoa ili ukome na uzalendo wako

Hongera zenu Temeke manispaa kwa kuwawekea mazingira magumu wajasilia mali wazalendo wanao penda kulipa kodi
Mimi tatizo la "service levy" ni pale pamoja na kulipia service levy wanakuja wakusanya taka nao wanataka uwalipe; sasa napashinda huduma iliyolipiwa na hiyo "service levy" si ni pamoja na kuuweka mji safi?
 
sidhani hata kama una biashara mi nafanya biashara na ninapambana nao kila siku labda wewe umezoea kupotoshwa
Hili sio suala la kubishana,lipo kisheria kiwango cha chini cha kodi ni 150,000,na kodi inalipwa kwa awamu nne,march, june, Sept na dec, hata uende November, kuwa unataka kufungua biashara hawawezi kukukadiria labda 37,500!!ya installment ya mwisho(dec) lazima ukadiliwe 150,000 wa kikusaidia sana watakushauri usifungue muda huo, njoo january!! Kwani kwenye system hawezi kufanya tofauti na hivyo!!! Hayo mawazo yako mpe huyo mdau aende hata kwa waziri uone kama kuna msaada atapewa!! Hapa tupo kuelimishana kitu ambacho mtu unakuwa na uhakika nacho, na unakifanya kila siku, kwani ni sheria, kwenye siasa na mapenzi ndio kila mtu anaweza toa maoni yake, kumshauri mhusika, lakini sio kwenye fani za watu.
 
Back
Top Bottom