Ufisadi mkubwa Wizara ya Maji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi mkubwa Wizara ya Maji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bishop Hiluka, Aug 19, 2011.

 1. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #1
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  * Wakaguzi wabaini ufujaji pesa za miradi

  * Mabilioni ya pesa za walipa kodi yayeyuka
  * Kashfa kwenye ununuzi wa mashangingi 68
  * Wafadhili watishia kuzuia misaada yao

  WIZARA ya Maji na Umwagiliaji imekumbwa na kashfa kubwa baada ya ukaguzi maalumu
  uliofanywa kwenye miradi ya maji nchi nzima kubaini tuhuma za ufisadi, uzembe wa maofisa
  na matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi kwenye wizara hiyo.


  Ukaguzi maalumu (special audit) uliofanywa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
  za Serikali (CAG) kwenye programu ya maendeleo ya sekta ya maji (2007-2010) umebaini
  malipo mengi ya utata kwenye miradi ya maji nchini na matumizi mabaya ya pesa za umma.


  Katika moja ya tuhuma hizo za ufisadi, Wizara ya Maji na Umwagiliaji imebainika kutumia zaidi
  ya dola za Marekani milioni 39 (takribani shilingi bilioni 63) kwenye mazingira ya utata bila
  kuzingatia miradi iliyopo kwenye mpango kazi wa mwaka wa wizara hiyo.


  "Shughuli za manunuzi ndani ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji hazifanywi kuendana na mpango
  wa manunuzi wa kila mwaka," imesema sehemu hiyo ya ripoti mpya ya CAG kutokana na ukaguzi
  uliofanywa Septemba mwaka jana.


  Pia ukaguzi huo umebaini kashfa kwenye ununuzi wa mashangingi (Toyota Land Cruiser) yapatayo 68
  uliofanyika mwaka 2009 kwa Yen za Japan milioni 235.4 (zaidi ya shilingi bilioni 5) kinyume na utaratibu
  rasmi wa manunuzi ndani ya serikali.


  Kwa mujibu wa wakaguzi wa ofisi ya CAG, ununuzi huo wa mashangingi bila kufuata taratibu za serikali
  umeisababishia wizara hasara ya zaidi ya shilingi milioni 218 kutokana na tofauti ya viwango vya
  ubadilishaji wa pesa za kigeni.


  Wizara hiyo imebainika kutokuwa na ufuatiliaji wa karibu wa pesa za miradi ya maji zinazopelekwa
  nchi nzima kwenye mamlaka za serikali za mitaa na hivyo basi kutojua kama pesa hizo zimetumiwa
  kwenye matumizi sahihi ama la.


  Wizara hiyo pia imekumbwa na kashfa ya matumizi makubwa ya pesa kwenye miradi mbalimbali ya
  maji kuliko gharama halisi za awali zilizokubaliwa kwenye miradi hiyo.


  Mifano hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Bwawa la Matwiga ambapo wakati mkataba wa awali
  ulisema kuwa mradi utagharimu dola za Marekani 284,693, wizara hiyo iliongeza malipo ya ziada
  kwenye mradi huo ya dola 80,615 (wastani wa shilingi milioni 129).


  Kwenye mradi wa Mpwapwa na Utete, wizara ilitumia dola za Marekani 32,250 zaidi ya gharama
  halisi ya mradi huo kwenye mkataba wa ujenzi ambayo ilikuwa ni $39,600.


  Mamlaka ya Maji Safi na Taka ya Moshi nayo ilitumia $947,757.53 (shilingi bilioni 1.5) kuilipa
  kampuni ya Seureca Consulting Egineers ya Ufaransa kushirikiana na NETWAS Tanzania Ltd
  wakati mkataba na kampuni hiyo ulikuwa ni wa malipo ya $303,375.04 (shilingi milioni 485 tu).
  Malipo hayo ya ziada ni sawa na asilimia 212 ya gharama zilikubaliwa awali za mkataba huo.


  Wakaguzi wamebaini ukiukwaji mkubwa wa taratibu rasmi za manunuzi, utunzaji wa kumbukumbu
  za fedha na ufuatiliaji kwenye miradi mbalimbali ya maji. Hii ni pamoja na kutokuwepo kwa nyaraka
  muhimu za malipo, malipo ya pesa nyingi zaidi kuliko zilizokubaliwa kwenye mikataba ya miradi ya maji,
  matumizi mabaya ya pesa na kutokuwepo kwa wakaguzi wa ndani.


  Baadhi ya matumizi kwenye miradi ya maji nchini inayoratibiwa na wizara hiyo yameonekana kuwa ni
  zaidi ya pesa zilizotengwa kwenye bajeti, huku pesa nyingine zikitumiwa kwenye miradi ambayo
  haikulengwa kutekelezwa.


  "Wizara ya Maji na Umwagiliaji inatakiwa kutengeneza utaratibu mzuri wa kufuatilia na kuweka rekodi
  ya pesa zote zinazotumwa kwenye mamlaka za serikali za mitaa," ilisema sehemu ya ripoti hiyo ambayo
  KuliKoni imepata nakala yake.


  Ofisi ya CAG imetoa maagizo kwa wizara hiyo kuhakikisha kuwa manunuzi yote yanafanywa kulingana
  na pesa na miradi iliyowekwa kwenye mipango rasmi ya manunuzi.


  Maafisa wa serikali wameiambia Kulikoni kuwa baadhi ya nchi na mashirika ya kimataifa ambayo
  yamekuwa yakitoa misaada na mikopo kwenye sekta ya maji hapa nchini yamesitisha misaada yake
  kwa Tanzania, huku na mengine yakitishia kuzuia misaada kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa pesa
  kwenye miradi ya maji.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Here we go again. Hivi Waziri wa hii wizara si ndiyo yule Mgonjwa yuko Nje ya nchi?

  Huyu anajulikana sana ingawa madudu mengi kayakuta. Ukitaka kupata habari yake, waulize TTCL jinsi alivyowaliza.

  Mtoto wake akaenda kutesa South Africa....... very poor mind. Unauza nchi kwa shanga na kioo?
   
 3. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Yote haya ni kukosekana kwa uzalendo...
   
 4. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Haponi mpaka Bajeti ya wiraza yake ipe ndio atapona amekimbia kijanja huyo
   
 5. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Teh teh, ina maana kila siku anapiga simu kuulizia?
   
 6. m

  massamu Member

  #6
  Aug 19, 2011
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  '' freedom is never voluntary given by the oppressor; it must be demanded by the oppressed ''
   
 7. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #7
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  So, what should be the solution?
   
 8. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  tutaona mengi sana juu ya hii serikali yetu legelege....................................!
   
 9. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #9
  Aug 19, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  \
  Kuna kiongozi mmoja alisemaga kwamba hakuna msafi ndani ya CCM. Nafikiri mtu akifanya research ya ufisadi kuanzi juu mpaka chini kwa mwenyekiti wa serekali za mitaa, anaweza kupata PhD kabisa.
   
 10. GHOST RYDER

  GHOST RYDER JF-Expert Member

  #10
  Aug 19, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 1,025
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Sijui Wizara Ipi salama, jana tunaambiwa ati baada ya Majibu mazuri ya Mama Tibaiuka wabunge wakaamua kuipitisha Bajeti yake. Hatutaki majibu mazuri uwajibikaji ndio hasa muhimu. Wanaobainika na kutuhumiwa kama hawa sheria madhubuti zichukue Mkondo na si drama za akina Zombe
   
 11. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #11
  Aug 19, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Alikuwa Sofia Simba (mbunge na waziri)
   
Loading...