Ufisadi mkubwa chuo kikuu cha Nelson Mandela - Arusha

Chiluba

Member
Nov 8, 2007
51
7
Huku kukiwa na takribani miezi miwili tuuu tokea Rais J.Kikwete kukizindua Rasmi Chuo cha Nelson Mandela maarufu kama Nelson Mandela African Institute of Science and Technology, kashfa nzito, na ufisadi wa kutisha umebainika kufanywa na Naibu wa Makamu mkuu wa chuo hicho (Deputy Vice Chancellor – Planning, Finance and Administration).

Ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka umebainika katika zoezi la ukaguzi “audit” ambalo bado linaendelea kufanyika chuoni hapo, imebainika kuwa mengi ya matatizo hayo yamekuwa yakilalamikiwa na wafanyakazi bila kufanyiwa kazi na uongozi wa chuo hicho kwa mda mrefu…
Haya ni baadhi tuu ya mambo machafu yaliyobainika na yanayosemekana kufanywa na Profesa huyo bila aibu yeyote.

1. Kwa mwaka wa fedha 2011/12 Ametumia takribani Tsh 50m (Milioni Hamsini) kwa safari za ndani tuu, ambazo nyingi ni zake binafsi kwenda Dsm ilipo familia yake. Siku za safari zikiwa ni kuondoka Alhamisi na kurudi J3 takriban kila wiki. (Inasemekana anajenga ghorofa mjini DSM kwa hyo anakwenda kusimamia nk).Gharama zote za safari zimelipwa na Chuo yeye akiwa ndio muhidhinishaji wa malipo yote.

2. Imebainika kwamba Safari zote wanazotakiwa kwenda wafanyakazi waliopo chini yake anakwenda yeye. Mf. masuala yote ya Budget, Mipango, Mishahara na watumishi, yanayotakiwa kufuatiliwa na wataalamu wa kada hizo amekuwa akienda yeye bila kushirikisha wataalam hao. Pia amekuwa akijilipa safari zake zote anazosafiri huku wafanyakazi wengine wakishindwa kusafiri safari za kikazi au wakisafiri bila kulipwa kwa kisingizio cha kutokuwepo kwa fedha.

3. Imebainika kwamba Manunuzi yote ya Taasisi amekuwa akifanya yeye kwa kusaidiana na rafiki yake wa Karibu ambaye ni ESTATE Manager, bila kuhusisha kitengo cha manunuzi ambacho kipo, hivyo kikiuka taratibu zote za manunuzi, na pia kununua vifaa vingi visivyohitajika ama vyenye ubora hafifu sana na kwa bei ghali sanaaa! Mf. Huku Taasisi ikihitaji kununua “printers 6 zenye kutumia smart cards”… bila kuhusisha wataalam yeye na mwenzake wakajikuta wamenunua “printers 6 za kuprint Identity cards” ambazo zimelipiwa na hazifanyi kazi kabisa wala haziwezi kutumika… Vile vile amebainika kununua magenerator mawili tokea Zanzibar alipokuwa akifanya kazi na yote mawili hayafanyi kazi, pamoja na kununuliwa kwa gharama kubwa tuuu.

4. Imebainika kwamba Huku akilimbikiza madeni ya wafanyakazi (wafanyakazi wapya wamekuwa wakichukua hadi miezi 6 kulipwa malipo yao ya kuamisha familia nk) amekuwa akiwalipa watoa huduma mbalimbali bila kufuata taratibu zozote na kwa muda muafaka.
5. Matumizi mabaya ya rasilimali, imebainika kwamba hata gari la taasisi analotumia yeye hataki litumiwe na afisa mwingine yeyote Yule na anaposafiri huwa linapaki nyumbani kwake hadi arudi.

6. Kuna tuhuma ambazo zimekwisha fika kwa Mkuu wa Mkoa na Makamu mkuu wa chuo, huku kukiwa na ushaidi kuwa amekuwa akitoa ajira kwa akina dada na hasa “masekretari wake” kwa rushwa ya Ngono! Hili limefika TAKUKURU na linafanyiwa kazi kwa kuwahusisha baadhi ya masekretari aliowafukuza ama walioamua kuacha kazi kwa sababu yake.

7. Kutokana na malalamiko mengi ya wafanyakazi, Prof huyu amekuwa akikwepa ziara zote za viongozi mbalimbali wanaotembelea taasisi ya Nelson Mandela, Hakuwepo ktk ziara ya Katibu Mkuu wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Technologia (Chuo kipo chini ya wizara hii), ziara ya waziri wa Mawasiliano, sayasi na technologia, ziara ya waziri Mkuu, na hata ziara ya Mkuu wa Chuo Mh. Makamu wa rais, hii yote inasemekana ni kuogopa kushtakiwa na wafanyakazi
 
Mtaje jina yawezekana watu wakamjua historia yake na kutiririsha ukweli.
 
Mtaje jina yawezekana watu wakamjua historia yake na kutiririsha ukweli.

Huyo bwana anaitwa prof. Alfonce Dubi, kabla ya kuteuliwa kuwa hapo Mandela inasemekana alikuwa UDSM (MARINE) ZANZIBAR ambako inasemekana wafanyakazi wa kule walifikia kutaka kuchoma nyumba aliyokuwa akiishi.
 
Huyo bwana anaitwa prof. Alfonce Dubi, kabla ya kuteuliwa kuwa hapo Mandela inasemekana alikuwa UDSM (MARINE) ZANZIBAR ambako inasemekana wafanyakazi wa kule walifikia kutaka kuchoma nyumba aliyokuwa akiishi.

Namjua huyu mzee ana mtoto wake mmoja anaitwa Irene mkali kinoma alishawahi kuwa miss COET (UDSM) enzi hizo ila kwa sasa ameolewa nadhani.
 
Je ule mgogoro baina ya uongozi wa wanafunzi juu ya kukatwa au kucheleweshewa fedha za tafiti umeishia wapi?
Huyo ameamua ajichotee mapema. Kweli biashara asubuhi, jioni mahesabu.
 
Ukifuatilia kwa makini utakuta majina ya watu wale wale walioiba pesa za ujenzi wa UDOM sasa wapo Nelson Mandela! Ni mtandao wa watumishi wa serikali na washirika wao wa nje!
 
Gaza and Israel;

Hebu pitia hapa Kamanda wangu!


Acha mambo hiyo kabisa mkuu. Tanzania Sayansi ni Siasa. Kila kitu wakubwa wanajua kuliko wadogo hata kama wanakosea.

Taarifa za ndani zinaonyesha kuwepo kwa matumizi mabaya ya fedha zinaelezwa na wafanyakazi na pamoja na wanafunzi wa Chuo hiki. Hii imesababisha wanafunzi kushindwa kuingia katika tafiti zao mpaka sasa. Wengi wamepata hela za kujikimu kidu8chu huku wakiwa hawajapata materials ambayo jamaa huyu anasema vitakuwa vinaagizwa na chuo badala ya wanafunzi. Hili ni tatizo na uroho wa pesa. Mtu wa PhD anajua anachofanya haitaji kuongozwa.

Kila mahali sahizi ukikutana na wanafunzi wa chuo hiki wamekuwa wamekufa moyo hasa kwa mambo yanavyoendeshwa kisiasa.

Kisa cha matumizi mabaya ya madara na ufujaji pesa, umeanza kujulikana baada ya wafanyakazi kuongezeka na kuanza kuhoji. Lakini hata hivyo watawala wamekuwa wagumu kutambua nini lengo la kuanzisha chuo hiki.

Thanks,
 
serikali huwa inazembea kufuatilia mambo,serikali makini huwa inapopata tetesi inafutilia,ili kujulisha uma ukweli,serikali huwa inamtindo wa kuzembea kufuatili mambo,ambayo baadaye yanaleta tafrani kubwa,serikali ifuatilie hili swala,kwasababu huu ni ufisadi.
 
Naona kama mleta mada hana ushahidi na anayoongea. Mbona mambo hapo chuoni nasikia ni mazuri sana? Tunaomba atuwekee ushahidi zaidi.
 
jamani sasa tutaenda wapi?? hamna chuo nlikua napenda kuja kusoma kama hiki!!! duh.....kweli hii ni tz......ila poa taratibu tutafika!!!!
 
Back
Top Bottom