Ufisadi miaka 50 ya uhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi miaka 50 ya uhuru

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiroroma, Dec 7, 2011.

 1. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2011
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Yapo mambo ya kusimuliwa yako mambo ya kuona kuhusu miaka hamsini ya UHURU wa Tanganyika. Mbwembwe za kila aina zimesheheni ufisadi wa hali ya juu.Kweli kweli ukishangaa ya Musa basi Farao ni cha mtoto.
  Katika kusherehekea miaka hiyo hamsini.Taifa limejiingiza katika ufisadi mwingine kwa style tofauti kwani safari hii una kibali cha serikali Kuu,Ikulu,Luhanjo na timu yake.
  Kila unachokiona katika mlolongo wa maadhimisho haya kimepatikana kwa gharama mara kumi hata na zaidi. Mathalani T shirt walizovaa watumishi wa Wizara ya Fedha zimenunuliwa Mariedo kwa bei ya T shirt mmoja na kofia Tshs.75,000/=,Huduma za chakula kwa wafanyakazi wa wizara ya Ardhi mtu mmoja anapata lunch ya shs.25,000/= achilia mbali out pocket Allowance ya Tshs.50,000/=,Magari ndo usiombe mafuta yanajazwa pasipo rekodi.Kwa ujumla kuna ufujaji mkubwa sana wa fedha za serikali katika kipindi hiki cha miaka 50 ya Uhuru.Nimejionea mengi mengi sana muda hautoshi ningeweka data za kushangaza hapa.
   
 2. shizukan

  shizukan JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii ndio serikali tulioipa dhamana na kuisapoti kila viongozi wanapoongea 'dust bin contents'. Kununua T-shirt 75,000 lazima cha juu kimeandikwa tu. Na hata tukirudi nyuma, tujiulize ni mangapi muhimu kuliko T-shirt hayajafanyika badala yake tuko bize na sherehe ambayo ktk uhalisia wake haina maana kwani Watanzania hawako huru.

  Jana tumeona kwenye habari jinsi njaa inavyokamata vijiji kila kona ya nchi, badala ya kuliona hili hebu angalia msururu wa vituko:
  1. Mkuu wa wilaya anakanusha kuwa si kweli wananchi wa wilaya yake wanaishi kwa kula kumbikumbi na nyasi (kesho yake tu ikadhihirika ni kweli)
  2. Katibu wa bunge (kwa kuona aibu) anakanusha kuwa wabunge wameongezewa posho (kesho yake tu inadhihirika ni kweli zimeongezwa). Wabunge wameongezewa kwa kuwa maisha magumu, walimu wanajiandaa kuandamana.
  3. Maalim Seif Shariff Hamad ambaye si muda mrefu uliopita alikuwa critic mkubwa wa serikali dumafu ya CCM anatamka hadharani kuwa VIJANA WANATAKIWA WAPEWE ELIMU YA KUTAMBUA MAFANIKIO YA NCHI NA SIO KUONA MAPUNGUFU TU. (huu ni unafiki)

  Kama CDM na WANAHARAKATI wameonekana wanaleta tu fujo walipodai KATIBA inatungwa kwa manufaa ya CCM, sasa umefikia wakati kila mtu ajionee mwenyewe.
  1.Hakuna fedha za kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu na Wastaafu wa EAC, za kulipa EPA zipo.
  2.Serikali imeona kuwa 'maisha ni magumu', lkn inaonesha ni magumu kwa wabunge tu na sio walimu
  3.Sheria iliyoruhusu kupandishwa kwa posho za wabunge inampa mamlaka Rais kufanya hivyo (ndiyo huu hasa ugomvi wa wanaharakati juu ya muswada wa katiba) Mtu mmoja kuwa na madaraka ambayo anaweza kuyatumia kama ilivyotumika hapa kwa maslahi ya kundi linalomhusu.

  TUMEYATAKA WENYEWE kwa KURA ZETU
   
 3. kimatire

  kimatire JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2011
  Joined: Nov 27, 2008
  Messages: 365
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Haya ni matunda au ni mazao ya miaka 50 ya Uhuru? Kuna jambo la kujifunza kwamba hatusongi mbele bali tumethubutu kuchagua njia isiyo ndani ya miaka 50.


   
Loading...