Ufisadi Juu Ya Magari Ya Abiria!!!

Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,324
41
Wakuu wa JF, kuna taarifa ya kuwa Serikali imetoa waraka kuwa Gari za Abiria zitakazoingia Tanzania ziwe mwisho 2005(by next Month), yaani gari itakayoingizwa iwe 5yrs back kutoka mwaka unaonunua hio gari.

Hii ni tofauti na ile walotangulia inayosema gari iwe ya miaka 10, zaid ya hapo itabidi iwe inalipiwa gharama za Mali CHOVU.

Hofu yangu ni kuwa watu wa kima cha chini wanaoingiza hiace au Mini buses...hawatoweza kuafford hili, na kuna uwezekano mkubwa kuna wajanja wachache wanataka kuingiza gari zao, na ili zilipe basi wanaweka vizingit wengine wasiweze kuagiza magari yao. Na Hapa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa wahusika wakalambishwa chochote juu ya Hili.

Naomba Tujadili na kama kuna mtu ananyeti zaid..basi atumwagie..
 
kuna uwezekano mkubwa kuna wajanja wachache wanataka kuingiza gari zao, na ili zilipe basi wanaweka vizingit wengine wasiweze kuagiza magari yao. Na Hapa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa wahusika wakalambishwa chochote juu ya Hili.

Kwa maoni yako unadhani kweli hiyo ndiyo sababu ya msingi ya serikali kupiga marufuku uingizaji wa magari ya abiria yaliyozidi miaka 5?
 
Wakuu wa JF, kuna taarifa ya kuwa Serikali imetoa waraka kuwa Gari za Abiria zitakazoingia Tanzania ziwe mwisho 2005(by next Month), yaani gari itakayoingizwa iwe 5yrs back kutoka mwaka unaonunua hio gari.

Hii ni tofauti na ile walotangulia inayosema gari iwe ya miaka 10, zaid ya hapo itabidi iwe inalipiwa gharama za Mali CHOVU.

Hofu yangu ni kuwa watu wa kima cha chini wanaoingiza hiace au Mini buses...hawatoweza kuafford hili, na kuna uwezekano mkubwa kuna wajanja wachache wanataka kuingiza gari zao, na ili zilipe basi wanaweka vizingit wengine wasiweze kuagiza magari yao. Na Hapa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa wahusika wakalambishwa chochote juu ya Hili.

Naomba Tujadili na kama kuna mtu ananyeti zaid..basi atumwagie..
Kuna hoja mbili zinatumika, na zimepigiwa kelele pia Bungeni.

1) Magari chakavu na hasa ambayo hayafuati specification ndiyo sababu kubwa ya ajali nyingi ambazo zimechukua maisha ya Watanzania wenzetu wengi.
2) Tanzania imefanywa kuwa dumping ground ya magari machovu.

Sijawahi kuona utafiti wa kisayansi, sina hakika kama sababu hizi zinaweza kuwa msingi wa kutosheleza wa Waraka huo, na kama kweli ajali nyingi zinatokana na sababu hiyo!
 
Naona na wewe Dr. Slaa, hoja hapa swala sio magari ya miaka mingi tatizo ni ukaguzi mbaya wa magari na udhibiti mbovu wa mwenendo wa madereva wanayoondesha hayo magari. Kwani kwenye nchi za wenzetu yanayotoka hayo magari tunaona magari hayohayo miaka mingi yakibeba abiria na bila kupata ajali. Ninachoona hapa watu wanakwepa majukumu na kutafuta masilahi yao humo humo. Tatizo hapa ni rushwa katika ukaguzi wa magari.
Asante.
 
Hapa ndipo penye tatizo,sioni sababu ya kufanyia ukaguzi magari yanayoingizwa nchini wakati ndani ya nchi kuna magari machakavu kupita kiasi.Tatizo la serikali yetu inakimbia majukumu na hasa watendaji wanaubinafsi usiokuwa na tija.kwa nini tusifuate utaratibu wa nchi za wenzetu wa kukagua magari kwa kutumia vifaa vya kisasa na gari ambalo halifai litolewe njiani.
Lakini huu mchezo wa kupeleka sh 2000/= pale trafiki kisha unapewa stika et gari limekaguliwa hautufikishi popote.
 
Kuna hoja mbili zinatumika, na zimepigiwa kelele pia Bungeni.

1) Magari chakavu na hasa ambayo hayafuati specification ndiyo sababu kubwa ya ajali nyingi ambazo zimechukua maisha ya Watanzania wenzetu wengi.
2) Tanzania imefanywa kuwa dumping ground ya magari machovu.

Sijawahi kuona utafiti wa kisayansi, sina hakika kama sababu hizi zinaweza kuwa msingi wa kutosheleza wa Waraka huo, na kama kweli ajali nyingi zinatokana na sababu hiyo!

Hawa wanaosema magari chakavi ndio tatizo la ajali barabarani ni waongo wakubwa wanaotaka kuudanganya umma wa WaTanzania,hebu walete stastic ya magari yanayopata ajali,mbona mara tunasikia madereva ni wazembe ,wanaendesha magari mbio ,si bora wakaruhusu yaliochakaa ,hayaendi mbio.

Walikurupuka na hoja ya kufunga luku kwenye magari,hawa jamaa wameishiwa ,na sasa wanataka kuuzidisha umasikini wa Mtanzania zaidi ya hapa ulipo,hebu watafute gari iliyotumika miaka mitano,ni kiasi gani na Mtanzania anapokea mshahara kiasi gani ,je maisha bora kwa kila mtanzania ya kumiliki angalau kijigari kidogo cha kupeleka wanawe shule yatafanikiwa ?
 
Tatizo la magari mengi na hasa yenye kutumia diseli na petroli yanachangia sana katika kuchafua mazingira, na ni kupitia katika moshi wa magari hayo ambao huwa na No na CO... Mchanganyiko huu hutoa vilatile organic compound (VOC) ambayo uharibu ozone layer.

Kwa binadamu moshi wa magari sio mzuri kwa afya, zaidi ni mbaya sana kwa watoto, wazee na watu ambao wanasumbuliwa na asthma, bronchus inflammation na ugonjwa wa moyo.

Nchini China, tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 7 ya watoto katika nchi hiyo tayali wameathirika na moshi wa magari, Ni ni baada ya damu zao kuwa na viwango vikubwa vya lead kuliko inavyotakiwa na viwango wa nchi yao.

Dunia ya leo na hasa katika nchi zilizoendelea kuna ukaguzi mkubwa wa magari na hasa kwenye utoaji wa CO, kiwango cha iyali kwa nchi za EU za moshi wa magari ni 140g/km, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa magari mengi yanatoa 160g/km. Haya ni magari yenye umri wa 0 hadi miaka mitano.

Kwa mtazamo wangu upo umuhimu wa kuzuia magari ambayo yameshatumika zaidi ya miaka mitano ili kuweza kulinda mazingira ya nchi yetu. Kuanzia mwaka 2012 nchi za ulaya zitakuwa na sheria kali katika magari mapya na yale ya zamani, na ninategemea magari machakavu mengi yataingizwa kwa wingi barani Afrika na Tanzania ikiwa mojawapo.
 
Wakuu wa JF, kuna taarifa ya kuwa Serikali imetoa waraka kuwa Gari za Abiria zitakazoingia Tanzania ziwe mwisho 2005(by next Month), yaani gari itakayoingizwa iwe 5yrs back kutoka mwaka unaonunua hio gari.

Hii ni tofauti na ile walotangulia inayosema gari iwe ya miaka 10, zaid ya hapo itabidi iwe inalipiwa gharama za Mali CHOVU.

Hofu yangu ni kuwa watu wa kima cha chini wanaoingiza hiace au Mini buses...hawatoweza kuafford hili, na kuna uwezekano mkubwa kuna wajanja wachache wanataka kuingiza gari zao, na ili zilipe basi wanaweka vizingit wengine wasiweze kuagiza magari yao. Na Hapa kuna uwezekano mkubwa wa kuwa wahusika wakalambishwa chochote juu ya Hili.

Naomba Tujadili na kama kuna mtu ananyeti zaid..basi atumwagie..

Mkuu heshima mbele.

Habari hii umeinyaka wapi na ni nani aliyetoa agizo hilo?
 
Kuna hoja mbili zinatumika, na zimepigiwa kelele pia Bungeni. i) Magari chakavu na hasa ambayo hayafuati specification ndiyo sababu kubwa ya ajali nyingi ambazo zimechukua maisha ya Watanzania wenzetu wengi. 2) Tanzania imefanywa kuwa dumping ground ya magari machovu. Sijawahi kuona utafiti wa kisayansi, sina hakika kama sababu hizi zinaweza kuwa msingi wa kutosheleza wa Waraka huo, na kama kweli ajali nyingi zinatokana na sababu hiyo!

sipingi wala siungi mkono hivyo vi hoja vyenu vya kitoto.

hizo hoja ulizozitoa zinaweza kuwa ni hoja za tatu na kuendelea ila kwa mwenye akili na jinsi ufisadi unavyofanya kazi nchi hii, hoja kubwa na muhimu ni kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaobangaiza na kuwaweza hao wenye nazo (viongozi) ndio wawe wafanyabiashara ya usafirishaji. wao wanafahamu kabisa kuwa biashara hii ina faida nzuri tu ndio maana wanasisitiza magari yanayotakiwa yawe na viwango vikubwa ambavyo ni wao tu ndio wanaoweza kuvimudu!
 
Tatizo la magari mengi na hasa yenye kutumia diseli na petroli yanachangia sana katika kuchafua mazingira, na ni kupitia katika moshi wa magari hayo ambao huwa na No na CO... Mchanganyiko huu hutoa vilatile organic compound (VOC) ambayo uharibu ozone layer.

Kwa binadamu moshi wa magari sio mzuri kwa afya, zaidi ni mbaya sana kwa watoto, wazee na watu ambao wanasumbuliwa na asthma, bronchus inflammation na ugonjwa wa moyo.

Nchini China, tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 7 ya watoto katika nchi hiyo tayali wameathirika na moshi wa magari, Ni ni baada ya damu zao kuwa na viwango vikubwa vya lead kuliko inavyotakiwa na viwango wa nchi yao.

Dunia ya leo na hasa katika nchi zilizoendelea kuna ukaguzi mkubwa wa magari na hasa kwenye utoaji wa CO, kiwango cha iyali kwa nchi za EU za moshi wa magari ni 140g/km, lakini uchunguzi unaonyesha kuwa magari mengi yanatoa 160g/km. Haya ni magari yenye umri wa 0 hadi miaka mitano.

Kwa mtazamo wangu upo umuhimu wa kuzuia magari ambayo yameshatumika zaidi ya miaka mitano ili kuweza kulinda mazingira ya nchi yetu. Kuanzia mwaka 2012 nchi za ulaya zitakuwa na sheria kali katika magari mapya na yale ya zamani, na ninategemea magari machakavu mengi yataingizwa kwa wingi barani Afrika na Tanzania ikiwa mojawapo.

Hii ya hali ya hela si kweli kwamba ndilo lengo lao! Hawa ni lengo la kuzia tu wanyonge ili fedha ambazo mafisadi wamekusanya waweze kununua magari mapya watese! Je ni ajari ngapi za barabari zinazoenyesha kuwa magari yanayoangua ni yale yenye umri umri mkubwa! any research au data! huku ni kushidwa tu kwa usalama wa raia barabarani na serikali yake kutafuta sababu za kweli na njia sahihi ya kupunguza ajali barabarani!

Taifa hili halitafika mbali kama sababu za msingi zinajulikana lakini walio juu wanatafuta zao kwa maslahi yao!

Kama suala ni uchafuzi wa hali ya hewa je MBONA NIMESIKIA SERIKALI INATAKA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA MAKAA YA MAWE!!!? JE SI HAYA MAKAA YA MAWE YALISABABISHA UCHAFUZI MWINGI WA HALIA YA HEWA HUKO CHINA!?
 
Kuna hoja mbili zinatumika, na zimepigiwa kelele pia Bungeni.

1) Magari chakavu na hasa ambayo hayafuati specification ndiyo sababu kubwa ya ajali nyingi ambazo zimechukua maisha ya Watanzania wenzetu wengi.
2) Tanzania imefanywa kuwa dumping ground ya magari machovu.

Sijawahi kuona utafiti wa kisayansi, sina hakika kama sababu hizi zinaweza kuwa msingi wa kutosheleza wa Waraka huo, na kama kweli ajali nyingi zinatokana na sababu hiyo!

......hizo ni baadhi ya sababu....trust me Mh. Dr. Slaa.........soma pia maelezo mazuri ya Mkuu Kibunango..........regardless ya kwamba.....eti kuna watu wanataka wanyonge wasifanaye biashara ili wenye uwezo peke yao ndio wafanye........hapa watu wanajaribu kukimbia hoja.............hutuhitaji gymnastics za kisayansi kuona hizo sababu ni za msingi Mh. Dr. Slaa..........

.....hiki kilio cha Afrika kuwa dumping ground nadhani sio kigeni kwako na Tanzania ni nchi moja iliyoathirika na hilo (....yeah ndio umasikini wenyewe)..............

tumeshuhudia pia malori ya aina mbali mbali yakifanyiwa modifications kuwa mabasi ya abiria

Ni muhimu kuwe na standard za magari ya abiria..........pia napenda kusema kama ni ajali.........hili suala huchangiwa na vitu vingi ZAIDI ya hivyo hapo juu...........masuala kubwa ya ku-abide nayo ni kama ifuatavyo

1.Engineering - i.e. standard specifications are met
2.Education i.e. both to the public and to the using driving the machine
3.Enforcement i.e. law enforcers to make sure 1 & 2 are adhered

hayo mambo matatu hapo juu yanaenda pamoja................ukiacha moja tu .........ndio utaishia ktk mijadala isiyokwisha
 
.........Kama suala ni uchafuzi wa hali ya hewa je MBONA NIMESIKIA SERIKALI INATAKA KUZALISHA UMEME KWA KUTUMIA MAKAA YA MAWE!!!? JE SI HAYA MAKAA YA MAWE YALISABABISHA UCHAFUZI MWINGI WA HALIA YA HEWA HUKO CHINA!?

......Duhh........kaazi kweli kweli
 
Kuna ubaya gani kutaka kuleta magari bora zaidi? Hivi mnataka tuendelee kupanda magari mikweche? Hata kama ni njia ya kuwafukunza nje ya biashara wasio na uwezo, ni bora iwe hivyo ilimradi tu tuwe na uhakika tunasafiri na magari imara yanayostahili kubeba binadamu. Kuna haja gani ya kutafuta vitu vya bei rahisi ambavyo vitatuangamiza?
 
Hao ni wazushi tu, hata yakiletwa brand new kwa barabara za kwetu yatakuwa chakavu kwa kipindi kifupi sana. watuonyeshe takwimu kwamba mabasi hasa hizi dala dala zetu zilivyosababisha ajali kwa ajili ya uchakavu.

TANZANIA YENYE NEEMA HIYOOOO YAJA
 
Hapa naona kuna mafisadi walijaribu na sasa wameshapenya ndani ya bunge, faida itakayopatikana ni kwa wale wanaoagiza bulk of cars na kuziweka kwenye maduka ya kuuzia magari. Hawa wanataka kuwaua kiuchumi wale wanaopata vijisenti vya papo kwa papo ambao hufunga safari kwenda Japan au Dubai kununua kigari kimoja au viwili na kurudi kuviuza au kuvitumia kisha kuviuza na kurudi kwenda kununua nyengine.

Ni aina ya biashara kwa baadhi ya ndugu zetu na hujipatia riziki zao kihalali. Madhara ya kuifunga sector hii ambayo hao wanaoitumia huwa hawana uwezo wa kununua gari iliyotumika miaka mitatu au mitano na ,uwezo wa kununua ni kwenye modeli 90ies .

Nina wasiwasi hawa wanaotunga sheria hapa Bongo wanadhani au labda wanaamini kuwa gari ikiwa ni ya model 90 huwa imeshachakaa kabisa na imezeeka kwa shughuli za kubeba abiria. Nadhani hawafahamu kuwa hata huko Japan kuna magari yanawekwa showroom na hayapati mnunuzi na kwa hali ya kwao ikishapita miaka miwili gari hiyo huwa haiuziki tena au haipati mnunuzi na hapo hupelekwa kwenye soko la mnada na bei yake huwa inapungua kila mwaka.

Kuna gari huwa zimebondeka tu na pengine ilitengenezwa miaka kumi iliyopita na ndio hivyo hivyo kwa zingine zinakuwa zimeathirika katika handling na huwa zinauzwa kama zilivyo. Lakini gari ni mpya kwa Mtanzania tu inamtosha kabisa.

Ila hawa mafisadi wanajaribu sasa kuhamia katika mambo ya biashara na wanataka kuziua biashara ili zibaki za kwao. Sasa mtu kama Chenge ana uwezo wa kuleta gari kama mia model 2008, mtu huyu akiliteka bunge na kupitisha hoja ya kukataza yasiletwe magari yaliyotengenezwa chini ya 2007, natumai mmeiona picha inayotaka kuchezeshwa bungeni na mafisadi wetu wachanga wachanga.
 
Kuna hoja mbili zinatumika, na zimepigiwa kelele pia Bungeni.

1) Magari chakavu na hasa ambayo hayafuati specification ndiyo sababu kubwa ya ajali nyingi ambazo zimechukua maisha ya Watanzania wenzetu wengi.
2) Tanzania imefanywa kuwa dumping ground ya magari machovu.

Sijawahi kuona utafiti wa kisayansi, sina hakika kama sababu hizi zinaweza kuwa msingi wa kutosheleza wa Waraka huo, na kama kweli ajali nyingi zinatokana na sababu hiyo!

Hapo napingana na wewe kwa kuwa asilimia kubwa ya ajali barabarani husababishwa siyo na uchakavu wa magari, bali uzembe wa maderava pamoja na njaa inayowakabili maaskari wa usalama barabarani. Utakuta trafki anamkamata dereva kwa kuendesha gari kwa mwendo kasi au kwa kutofuata ipasavyo sheria za barabarani na badala ya kumpeleka kituoni kumchukilia hatua za kinidhamu, anazunguka naye nyuma ya gari kisha anachukua kilicho chake na safari inaendelea.

Jambo jingine linasababishwa na utolewaji wa holela wa leseni manake mfano mzuri ni rafiki yangu mmoja ambaye alikuwa na leseni ya Class 'C' halafu ndiyo kwanza alikuwa anafanya mpango wa kwenda kusomea udereva. Ukimuuliza imekuwaje una leseni wakati hata kuendesha gari hujui, jibu lake ni rahisi tu, kuna mjomba wake alimfanyia mpango wa kuipata ile leseni kwa sababu yeye alikuwa anastaafu hivyo ingekuja kumuwia ngumu kijana kuja kupata leseni pale atakapokuja kuihitaji wakati mjomba keshastaafu.
 
Haya ndiyo maelekezo ya Serikali kuzuia mabasi yaliyotumika chini ya miaka 5

Huu ni ufisadi kikweli kweli; kuna nchi nyingi tena zilizoendelea kuliko yetu ambao hawajachukua uamuzi wa kipuuzi kama huu. Watanzania wangapi wenye uwezo wa kuagiza gari la abiria (basi) chini ya miaka 5?. NA hao waliopo wanaweza kuingiza mabasi ya aina hiyo kutosheleza mahitaji ya nchi nzima? Hapo kuna mkono wa kifisadi.

Nimeambatanisha kivuli cha barua ambayo TBS waliwaandiki JAAI
View attachment 2002
 
Jee, hii sheria inayodhibiti uagizaji magari yasiyozidi miaka 5 inahusu magari ya abiria pekee, au? Hebu anaye fahamu anieleweshe tafadhali. Thx
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom