Ufisadi: Jitegemee Trading Company, mmiliki nani?

Ufisadi: Jitegemee Trading Company, mmiliki nani?

Kampuni hii imepewa tenda katika mazingira tatanishi ya "Development of Lorry, Container and Motor Vehicle parking facility and logistics centre outside Dar Port" ambapo project hii ina thamani ya TZS 10,000,000,000.

Wadadisi wanadokeza kuwa ina mkono wa CCM na kuhisi kuwa ni katika kukusanya 'mapato' towards 2015.

Nyaraka nitawasilisha kwa wakuu wanisaidie kuziweka zikiwa hazina footprints. Kama kuna mwana JF anaijua vema hii kampuni atusaidie tuweze kufahamu vema juu ya kampuni hii.

Doc 1:
attachment.php

Doc 2

attachment.php

UPDATE 1:

sasa kwa nini wamemwamisha Mwakwembe??
 
Mkuu Makene, wasiomjua Mwakyembe ndio wanaosikitishwa kuhamishiwa wizara ya A.Mashariki, lakini hawajui kwamba Mwakyembe sio msafi kama anavyojipambambanua lakini pia kuonekana kwenye vyombo vya habari kwa kila tukio hata kama ni la kawaida nako kumesaidia kuwapofusha baadhi ya wananchi kuonekana kama ni mchapakazi.

Hata hivyo ukweli wa mambo umeonekana kwenye panguapangua ya baraza la mawaziri, maana angekuwa mchapakazi kweli basi system ingemlinda kwa ama kubaki kwenye wizara nyeti aliyokuwa anaisimamia ama angehamishiwa kwenye wizara nyeti zaidi kama ya nishati na madini ili kuendeleza uchapakazi wake
 
makene ni kanjanja.....mwakyembe ni best minister anayetajwa kwenye urais so makene anahangaika ku turnish image yake

Naomba nikusamehe. Nikuache. Hujui mantiki ya mjadala huu. Uraisphobia unawasumbua CCM. Ndiyo maana mnaishia kuwa na 'wataka' urais badala ya wagombea.

Kama umesema kwenye uzi huu kuwa anatajwa kwenye urais, basi umesaidia moja ya inferences nzuri za kufikia hitimisho kimantiki juu hasa ya kilichokuwa nyuma ya ufisadi huo wa SUKITA ambao malengo yake yanaelezewa kuwa ilikuwa ni kutafuta fedha za urais, kusaidia kundi na chama hicho. Kama EPA.

Nina wasiwasi na uelewa wa mwanzilishi wa bandiko hili. Anaandika uzi kama standard four. You need to improve you writting skill my bro...
 
Hivi CHADEMA mmeshindwa kabisa kujifunza namna ya kufanya siasa safi?
 
Mkuu Makene, wasiomjua Mwakyembe ndio wanaosikitishwa kuhamishiwa wizara ya A.Mashariki, lakini hawajui kwamba Mwakyembe sio msafi kama anavyojipambambanua lakini pia kuonekana kwenye vyombo vya habari kwa kila tukio hata kama ni la kawaida nako kumesaidia kuwapofusha baadhi ya wananchi kuonekana kama ni mchapakazi.

Hata hivyo ukweli wa mambo umeonekana kwenye panguapangua ya baraza la mawaziri, maana angekuwa mchapakazi kweli basi system ingemlinda kwa ama kubaki kwenye wizara nyeti aliyokuwa anaisimamia ama angehamishiwa kwenye wizara nyeti zaidi kama ya nishati na madini ili kuendeleza uchapakazi wake

Sistimu ni nani, ina uadilifu kiasi gani? hakuwa mzuri kiutendaji kama waziri yupi ndani ya CCM?
 
Bado Mimi nitabaki na Mwakyembe kama ndiye waziri mchapakazi na mwenye kiwango cha uadilifu kuwazidi wengine katika CCM ya sasa.
 
Ukweli utaendelea kuwa Ukweli hata watu wakipambana kuzuia usijadiliwe
 
Huyo ndio mkurugenzi wa habari Chadema. akili kama mtoto wa chekechea

Kwa nafasi yake anapokuwa analeta mada hapa ni vema akaipitia kwanza na kuwa na uhakika na uandishi ili kujenga na kulinda heshima ya nafasi yake kwenye chama kinachotegemewa na Watanzania wanyonge.
 
Kwa nafasi yake anapokuwa analeta mada hapa ni vema akaipitia kwanza na kuwa na uhakika na uandishi ili kujenga na kulinda heshima ya nafasi yake kwenye chama kinachotegemewa na Watanzania wanyonge.
Makene ameeleza kwa kina na kuweka viambatanisho kujustify alichokiwasilisha. Wewe unataka uhakika gani zaidi?
 
Sistimu ni nani, ina uadilifu kiasi gani? hakuwa mzuri kiutendaji kama waziri yupi ndani ya CCM?
Sistimu ni serikali ya ccm, uadilifu ni ule wa kutojihusisha na kashfa yoyote ya kifisadi na hakuwa mzuri kiutendaji kama wa wale mawaziri mizigo waliowahi tajwa tena hadharani na viongozi wa ccm. Swali lingineee...!!!
 
Hivi CHADEMA mmeshindwa kabisa kujifunza namna ya kufanya siasa safi?
unamaanisha nini? yaani kuibua na kukemea ufisadi kwa maslahi ya watanzania wote unaona ni siasa chafu, hebu tuambie kwa mfano mmoja tu, siasa safi ni ipi hasa?
 
Wale wanaojua mizigo ina circulate vipi bandarini wanasema kuwa TPA mizigo haishushwi siku hizi bali yote inapelekwa kwenye ICDs (bandari kavu) ambazo nyingi ukichunguza ni za walewale (vigogo).
Tukumbuke kuwa wazo la bandari kavu lilikuwa zuri na ilikuwa ni kwa ajili ya kuisaidia bandari pale inapokuwa imeelemewa, lakini ndio nasikia hata ikiwa haina mizigo ICD zinapewa upendeleo.
 
Makene ameeleza kwa kina na kuweka viambatanisho kujustify alichokiwasilisha. Wewe unataka uhakika gani zaidi?
Kuna post ya mwanzo ilikuwa inaelea elea ( haikuwa imekamilika), nadhani hii imefanyiwa usahihi ndio maana inasomeka vizuri kwa sasa.
 
Back
Top Bottom