Ufisadi Halmashauri Ya Wilaya Karagwe -jembe La Mkono Km 30 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi Halmashauri Ya Wilaya Karagwe -jembe La Mkono Km 30

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamakabuzi, May 5, 2008.

 1. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Juzi juzi nilikuwa matembezini katika wilaya ya Karagwe. Kilichonishangaza ni kukuta barabara kati ya makao makuu ya wilaya na tarafa moja ya nyabionza, umbali wa zaidi ya km 30, inatengenezwa kwa jembe la mkono. Hivi kweli uhalali uko wapi. Je ina maana fedha zilizotolewa hazitoshi kutumia catepillar?

  Kioja hicho kinazidi unapokuta watengenezaji wanalima nyasi za pembeni mwa barabara na kuzifukia kwenye mashimo yaliyo katikati ya barabara. Matokeo yake yakipita magari mawili, shimo linarudi palepale, lakini mhusika ameshatengeneza!
  Pia utakuta halitengenezwi tuta la barabara kiasi cha kuwezesha maji ya mvua yatiririke kwenda pemebeni, hivyo mvua ikinyesha maji huzoa tena hata huo udongo kidogo waliouweka kwa jembe la mkono, mfano mzuri ni sehemu inayoitwa Bigoro.

  Kuna siku wananchi waliona gari la Tanroads mkoa wa Kagera, wakajisemea moyoni kuwa sasa huyu mkandarasi atakoma maana wenye barabara wameona upuuzi anaoufanya - lakini wapi - anaendelea vilevile.

  Naendelea kutafuta kiasi cha fedha kilichotengwa kwa barabara hiyo, ila kwa vile nilikuwa nimeenda kutembea huko, inakuwa vigumu. Wana JF kama kuna anayeweza kukipata kwa haraka, atujulishe.
   
 2. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mambo mengine hata yanatia uchungu kuyasoma jamani...
   
Loading...