Hahaaa mmeshupaza shingo sasa zimevunjika , mnara mlioujenga Mungu kaamua kuuvunja huyu anasema leta tofali anapewa ndoo mwingine anaomba nondo anapewa mchanga hakika ukiujua ukweli nayo kweli itakuweka huru na ukae ukijua Mungu hamfichi mnafiki na kila kitu na na wakati wake , kuna wakati wa kulia ,
Wakati wa kucheka , wakati wa usiku na wakati wa mchana hakuna siri chini ya Mbingu na malipo ni hapa hapa Duniani aliye msafi ndani ya ccm na awe wa kwanza kumpiga jiwe lowassa
Siku zote Mungu huwa hujitenga na unafiki,umbeya, chuki, uzandiki, unyanganyi, dhuluma, rushwa, na mambo mengine yafananayo na hayo msimamizi wa haya ni shetani
Mungu huyu tunaemwamini muumba wa Mbingu na Dunia na vyote vilivyomo anapenda Amani, Upendo, Haki, Furaha na vyote vifananavyo nayo Tulianza na Mungu tutamaliza na Mungu.