Ufaulu wa wanafunzi kuendelea na daraja zero (0)

Ufaulu wa wanafunzi kuendelea na daraja zero (0)

mapinduzi daima

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
1,724
Reaction score
2,704
Waungwana,

Naibu Waziri Mr. Mulugo amewasilisha Taarifa Maalumu ya Wizara ya Elimu hivi punde bungeni Dodoma.

Kwa kifupi, daraja la SIFURI litaendelea kuwepo, na SI daraja la TANO kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu.

Kwa hiyo wale wote watakaoshidwa kupata daraja la I-V, watapata daraja la O, na wataendelea kutopatiwa VYETI.

Nawasilisha.
 
Huyo atakayepata div. 0 atakuwa amepata daraja gani kwa kila somo? Maana hata akiwa na F 7 mara 6 ni 42 ambayo bado ni div. Four nzuri tu.
 
Ningekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo ningejiuzulu. Hivi ni nani zaidi katika utendaji wa wizara kati ya katibu mkuu na naibu waziri? Mbona mulugo anamharibia sana huyu prof wa tcu? Prof usikubali kuburuzwa na wanasiasa vihiyo, ondoka!
 
Kwanza napenda kuungana na mwana jf aliyetangulia aliyetoa wito/ushauri kwa katibu mkuu wa wizara husika kuachia ngazi kutokana na mkanganyiko uliotuchanganya wananchi juu ya madaraja ya ufaulu nchini. Jambo hili limezidi kudhihirisha madudu yaliopo ndani ya serikali yetu. Jambo linaloniumiza kichwa ni pale kiongozi anapojua wazi amevurunda lakini bado anabaki madarakani. Inamaana Tanzania hakuna utamaduni wa kuwajibika? Hii ni aibu kubwa kuendesha serikali ya kidemokrasia namna hii. AMKA TANZANIA!
 
Waungwana,

Naibu Waziri Mr. Mulugo amewasilisha Taarifa Maalumu ya Wizara ya Elimu hivi punde bungeni Dodoma.

Kwa kifupi, daraja la SIFURI litaendelea kuwepo, na SI daraja la TANO kama ilivyotangazwa na Katibu Mkuu.

Kwa hiyo wale wote watakaoshidwa kupata daraja la I-V, watapata daraja la O, na wataendelea kutopatiwa VYETI.

Nawasilisha.

hakuna atakaepata 0, maana hata ukipata 5% kila somo overall unakuwa na V, fu ck u Mligo
 
Kinachoshangaza wengi ni kwamba, watendaji wakuu wa wizara ( waziri, Naibu na Katibu mkuu) wametoa matamko yanayokinzana. nijuavyo mimi na ilivyo kiutendaji, Waziri, Naibu waziri na katibu mkuu Wa wizara husika huxa na wazo moja kwenye maswala yenye tija kama haya. Labda wanataka kuwaambia watanzania ya kwamba wizara ile kila mtu ana maamuzi yake?,
 
hii wizara kuna shetani anapita kama haishi humo ndani, hivi ina maana katibu mkuu aliamka na kusema bila hawa jamaa "mawaziri" hawakuwa informed before? ama wakati wanapanga hayo madaraja - hawakushirikisha wadau wengine e.g. NECTA, Vyuo vikuu, walimu,etc? aibu sana
 
Huyo atakayepata div. 0 atakuwa amepata daraja gani kwa kila somo? Maana hata akiwa na F 7 mara 6 ni 42 ambayo bado ni div. Four nzuri tu.

Kwa wenye akili TUMESHAJUA MIPANGO YAO MIOVU JUU YA ELIMU YA TANZANIA.

Ni kuwa DARAJA LA SIFURI (0) limefutwa RASMI. K/Mkuu na N/Waziri wanawahadaa Watanzania.

Kuanzia sasa, HAKUNA Mwanafunzi atakeyapata DARAJA O. Hivyo watadai UFAULU wa wanafunzi umeongezeka,

Pambaaaaffffff kweli hii mijitu iliyosoma kwa kodi za Watanzania na kuendelea kula kodi za Maskini.

aaaaahhhahahhahaahah!!!!!!!!
 
hakuna atakaepata 0, maana hata ukipata 5% kila somo overall unakuwa na V, fu ck u Mligo

Haki ya MUNGU nimekogongea like kutoka kumoyo, kwa mana natumia haka "kamobiteli"
 
Enyi wenye fikra pevu na mnaofikiri kwa bongo na mioyo yenu humu hebu nisaidieni hapa, "hivi unaamini kuwa Rais wetu kaliona la tembo kwisha na mkorogano wa East Africa tu hili la elimu ya watoto wetu (wapiga kura watarajiwa) halioni wala kusikia"?. Na migongano ya watendaji wake je? Au labda anawasubiri kuwashtaki kwa matumizi mabaya ya ofisi hawa kina Mulugo?
 
Back
Top Bottom