UFARANSA: Polisi "amfufua mwanamke" aliyedaiwa kufa

UFARANSA: Polisi "amfufua mwanamke" aliyedaiwa kufa

proskaeur

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2017
Posts
1,594
Reaction score
4,972
Habarini ndugu wana JF,

Mwanamke mmoja Ufaransa "amefufuliwa" na Afisa mmoja wa polisi ambaye alimfanyia matibabu ya dharura kwa jina CPR saa moja baada ya Maafisa wa Afya kusema amefariki.

Mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina, alikua akiugua ukosefu wa hamu ya kula , alipatikan akiwa amezirai akiwa na mwanae wa miaka 18 baada ya kukabiliwa na kiharusi.

Maafisa wa Afya walifika nyumbani kwake mjini PARIS lakini walshindwa kumsaidia mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 49. Lakini Maafisa wa polisi walioitwa ili kuandika ripoti walihisi uhai ndani ya tumbo lake.

Taarifa ya gazeti la Le Parisien imesema kamba Maafisa hao wa Afya walikua wamesema kuwa amefariki na kutia saini cheti chake cha kifo.

Lakini Maafisa hao wa Polisi walihisi uhai ndani ya tumbo lake baada ya kumfunua nguo aliyokua amefunikiwa nayo.

Wakati Afisa mmoja wa polisi alipoangalia mishipa yake, walihisi Moyo wake ulikua bado ukipiga.

Huku Afisa mmoja akimshika mkono mmoja na kuzungumza naye, Afisa mwingine alipiga simu idara ya zimamoto ili kuchukua maelezo kwa ajili ya kumfufua. Baada ya dakika 30 za kumfufua, mwanamke huyo aliedhaniwa kufa alianza tena kupumua.

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom