Ufanye nini baada ya kuvunja ndoa?

Ufanye nini baada ya kuvunja ndoa?

NAWAONYA MATEPELI WA JF, AMBAO HAMNA ROHO YA UTU

KWENU NYINYI KAMA LAKI MOJA YA MNYONGE MNATAKA KUIPIGA.


SASA MNAPOMFUATA PM. NA KUJARIBU KUA NA HURUMA. KUMBE MNAWAZIA 2M ZA BIDADA, NI USHENZI NA UKOSEFU MKUBWA WA AKILI.


BIDADA, HUMU JF WOTE NI MATAJIRI, WANA MAKAMPUNI, WANAUWEZO WA KUKUAJIRI, WANA UWEZO WA KUKUPA KAZI, WANAUWEZO WA KUKUUNGA KABISA.

HUMU UNAEZA KUAMBIWA "KUNA JAMAA ANATAKA MILION 1 ILI AKUINGIZE KWENYR AJIRA ".


KUNA MWINGINE ATAKUJA KARIBU NAWEWEZ AKUPETIPETI NA KUKUPA POLE,WAKAT HUO ANAULIZIA " UMEBAKI NA NGAPI SASA???"




KWAHIYO KUA MAKINI... WEE ONDOKA NA USHAURI , WAKUKUSADIA, AKUSAIDIE BILA KUKUOMBA HELA YOYOTE.


NASEMA HAYO KWA SABABU BINADAM WASASA NI MNYAMA, HANA HISIA, WALA HURUMA, UKIWA MNYONGE NDO UNAPIGWA ZAIDI.
 
Pole sana hata hivyo hujaweka wazi namna mlivovunja hiyo ndoa!

Kwamba ni wewe umechukua tu uamuzi wa kuondoka kwake au ni yeye kaleta vurugu na kukufukuza nyumbani? Vipi mmeshashirikisha ndugu kujaribu kuwaweka sawa? Kama hamkuachana kwa kuvunjia ndoa mahakamani, huyo bado ni mumeo na vilevile ukumbuke mkiachana kiholela kwa kukimbiana au kufuzana tu hapo ni rahisi wewe na watoto kuzikosa haki zenu!

Kama mtaachana kwa kuvunja ndoa mahakamani hapo lazima mambo yafuatayo yafanyike:-

1. Mahakama lazima izigawe mali zote mlizochuma pamoja ktk maisha ya ndoa yenu, hapo utagawiwa 30% au 50%, ratio itategemea ulichangia vipi. Kwa hizo nyingine unazosema ni za kwako mwenyewe itatemea na namna utakavyoweza kuithibitishia mahakama kwa kutumia ama risit au mikataba ya manunuzi, ukiwa navyo hivyo mali zako utapewa zote, plus mgao wa zile mlizochuma pamoja.

2. Kama watoto wote ni wa kwake atawajibika kutoa pesa ya matunzo na gharama za masomo wala huna haja ya kumuhamishia mtoto shule za kawaida labda tu kama unahamia mkoa mwingine au mbali na shule yake.

Aidha, nakushauri ujipe muda wa kufikiri kwa utulivu lakini pia ukitafakari shughuli ya kufanya maana hiyo pesa mkononi ukikaa muda mrefu kwa gharama za sasa za maisha utabaki na vichele tu!
 
Pole Sana Kwa Unayoyapitia
Tuliza Mawazo Halafu Ndiyo Utakuwa Sawa Sawa
Watoto Unamtoa English Medium Wakati Huu Ama Ada Shi

Pole sana hata hivyo hujaweka wazi namna mlivovunja hiyo ndoa!
Kwamba ni wewe umechukua tu uamuzi wa kuondoka kwake au ni yeye kaleta vurugu na kukufukuza nyumbani? Vipi mmeshashirikisha ndugu kujaribu kuwaweka sawa? Kama hamkuachana kwa kuvunjia ndoa mahakamani, huyo bado ni mumeo na vilevile ukumbuke mkiachana kiholela kwa kukimbiana au kufuzana tu hapo ni rahisi wewe na watoto kuzikosa haki zenu!
Kama mtaachana kwa kuvunja ndoa mahakamani hapo lazima mambo yafuatayo yafanyike-
1.Mahakama lazima izigawe mali zote mlizochuma pamoja ktk maisha ya ndoa yenu, hapo utagawiwa 30% au 50%, ratio itategemea ulichangia vipi. Kwa hizo nyingine unazosema ni za kwako mwenyewe itatemea na namna utakavyoweza kuithibitishia mahakama kwa kutumia ama risit au mikataba ya manunuzi, ukiwa navyo hivyo mali zako utapewa zote, plus mgao wa zile mlizochuma pamoja.
2.Kama watoto wote ni wa kwake atawajibika kutoa pesa ya matunzo na gharama za masomo wala huna haja ya kumuhamishia mtoto shule za kawaida labda tu kama unahamia mkoa mwingine au mbali na shule yake.
Aidha nakushauri ujipe muda wa kufikiri kwa utulivu lakini pia ukitafakari shughuli ya kufanya maana hiyo pesa mkononi ukikaa muda mrefu kwa gharama za sasa za maisha utabaki na vichele tu!
Ndoa hatukufunga tulikua tunaishi tu...poa mimi ndio nimechoka na matendo yake nikaamua kuondoka tu nawatoto
 
Kama una laini za uwakala anza na hilo kwanza. Milioni 2 zinatosha kuanzia na anzia nyumbani usiende kupanga. Tatizo litakuwa ni location ya kufanyia uwakala na kodi au kama vipi nunua kibanda cha chuma, kipya kinatengengezwa kwa laki tano hivi, used kizuri cha laki nne hivi unapata.

Uwakala ni mgumu una changamoto zake kama huna uzoefu ila hakuna kitu rahisi. Ungesema uko eneo gani upewe idea nyingine
 
Usifanye kitu kwanza, jibane Sana Kwa mwezi mmoja, tulia tu ukifikiri cha kufanya! Ukikurupuka na Biashara Za kushauriwa jamii forum Kwisha Habari yako!
 
Cha msingi na Hakika nenda ustawi wa jamii kwanza wakupe tafsiri ya seke seke lote. Kama mlikua na ndoa na mmetofautiana jamaa atatakiwa ahudumie watoto, kama mlijenga nyumba ni ya watoto
Nyie mnaoshupalia aende ustawi wa jamii mna uhakika gani kama hao watoto ni wa huyo mwanaume?
Kama alimkuta ni single mother mwenye watoto wawili?
Mwambie kwanza huyu bidada anyooshe maelezo yenye kueleweka.
Kichwa cha habari anauliza afanye nini baada ya kuvunja ndoa.
Kwenye comments anasema hakuolewa alikua anaishi tu na Jamaa.
Kikubwa hio 2m yake anitafute tukapige ishu za madini, fasta tu anakua bilionea.
 
Kweli kabisa mkuu, sema wivu wengine wanashindwa kuvumilia hasa kama yeye anaenzi uaminifu!
Mleta mada nakushauri punguza wivu rudi mkalee watoto u-single mother mgumu heshima yako inapungua swala la jamaa kutowajibika kitandani dawa unayo mwenyewe usirudie kupekua simu yake nae hatashika simu yako.
 
Mleta mada nakushauri rudi kwa mme wako uku mtaani vijana watakuchakaza sana na kamwe hutaolewa hakuna mtu mkamilifu punguza jabza rudi kwa mmeo utakuja kunishukuru nakuambia
 
Kama amesema hawezi kulea watoto ambao hawapo mikononi mwake ina maanisha anataka kukaa na watoto, ushauri wangu huyo wa miaka 7 ungemuacha akae na baba yake aendelee kusoma, usimuharibie mtoto maisha kwa magomvi yenu, muache mtoto apate elimu anayostahili,
Huyo mdogo ishi nae nyumbani, usipange kwa sasa

Lakini kama hakupigi wala kukunyanyasa kijinsia nakushauri mngeyaongea yakaisha, ukawa mbali na simu zake, mpe sharti la kufunga ndoa, miaka 7 bila ndoa jamaniii , lakini ukiona hayasameheki basi fata ushauri hapo juu.
 
Wanawamke wa siku hizi tatizo mnajifanya mnajua sana, hapo ukute wewe ndo chanzo, wala sio mshikaji.
 
Dah nilikifirkia kuhsu life kweli niwe na watoto wananipa furaha na mke anayeniheshinu then nichepuke kitoto duh
 
Mleta mada nakushauri rudi kwa mme wako uku mtaani vijana watakuchakaza sana na kamwe hutaolewa hakuna mtu mkamilifu punguza jabza rudi kwa mmeo utakuja kunishukuru nakuambia
Ushauri wa hivi haujengi umekaa ki kukata tamaa kabisa, amani ya moyo ni muhimu hivi huwa mnawaza hao watu wakiuana mnapata raha gani? Acheni basi dah!! Kuzaliwa mwanamke ktk hili bara yahitaji ushupavu sana
 
Back
Top Bottom