UFALA HUU

UFALA HUU

Joined
Jan 13, 2018
Posts
38
Reaction score
50
Katika uzi huu mang’amuzi ya kisayansi yametumiwa kutilia shaka maudhui yanayoonekana kwa juu juu katika andiko la ikulu la kutofurahishwa na mjadala wa kuongeza muda wa urais. Badala yake, uzi huu unajikita katika maudhui yaliyojificha. Natumia mang’amuzi ya sayansi kwa sababu sayansi inatabia ya kutilia shaka na kudadisi; haichukulii kitu chochote hivihivi tu. Msingi huu huitwa organized skepticism. Japo andiko la ikulu kuhusu kutofurahishwa na mjadala wa kujiongezea siyo la kisayansi, lakini ni kazi ya sayansi kufunua na kuanika yaliyojificha. Sayansi hutumika kuelezea na ku-predict mambo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo jamii, uchumi, serikali n.k. Angalia hapa: Uchambuzi yakinifu wa kisayansi kuelezea wanaohamia CCM kumuunga mkono Rais

Kwa juu juu, barua ya ikulu inasikitika na kutofurahishwa na mjadala unaosemekana kuendelea. Kwa undani, yaani kwa kufunua yaliyojificha, barua hii inaweka kumbukumbu kuwa kumekuwepo hitaji la “watu” kutaka muda wa rais kutawala uongezwe. Inawaandaa wananchi kisaikolojia. Ni rejea inayoweza kutumika siku zijazo kwamba siyo matakwa ya rais kujiongezea muda bali “watu wametaka”; kwa lugha ya kawaida “nimeombwa”.

Sambamba na barua ya ikulu, ni mwitikio wa Juma Nkamia wa kumpinga rais BBC. Si jambo la kawaida rais kupigwa waziwazi na mbunge kutoka chama chake tena kwenye vyombo vya nje. Uamuzi wa Nkamia kuongea na BBC pia unaweka kumbukumbu na kuitayarisha jumuia ya kimataifa kuhusu kuongezewa muda kama hitaji la “wananchi” siyo yeye rais. Uamuzi wa Nkamia unaweza kutafsiriwa kama hofu yake ya kukosa ubunge ikiwa atakuja rais mwingine atakaye ruhusu demokrasia kufanya kazi. Maana katika mazingira ya sasa, CCM ndiyo wamepewa furasa ya kufanya siasa na kuhakikishiwa ushindi, uwe halali ya kwa bao la mkono. Angalia hapa: Uchambuzi yakinifu wa kisayansi kuelezea wanaohamia CCM kumuunga mkono Rais

Kwamba mjadala haujawahi kufanywa katika kikao chochote cha chama na ni kinyume na katiba ni maelekezo ya kuonyesha njia ya kutumia kuongeza muda wa kutawala. “Wanaohitaji” muda wa rais uongezwe wapeleke kwanza hoja hiyo ifanyiwe kazi katika vikao vya chama vya CCM. Baada ya hapo ndipo hatua ya kubadili katiba ifuate. Tayari Nkamia alishasema atapeleka hoja katika bunge ili muda wa rais uongezwe hadi miaka saba. Kutokuwepo na mpango wowote wa rais na kutotarajia kwake kuongeza muda wa urais kama inavyoelezwa kwenye barua kunapunguzwa nguvu na hoja iliyotangulia. Kupeleka suala hilo katika vikao vya chama na baadaye Nkamia kupeleka pendekezo la kubadili katiba bungeni. Angalia hapa: Come on CHADEMA you have missed a point, tatizo ni utawala wa sheria, ushindi mahakamani

Tumefikaje hapa tulipo? Mambo mengi yamechangia, na kwa hakika hisoria itawahukumu akina Mwanakijiji, Nyaningabo (ambaye ni mfuasi mwaminifu wa Mwanakijiji), Waberoya and the likes. Watu hawa walitegemewa kuwa wahenga haka jukwaani kwa kutetea demokrasia badala yake wamegeuka na kushadadia ukandamizaji na kuonekana kuingizwa katika biashara ya manunuzi ya wanasiasa angalia hapa:

Nyingine ya kufungia mwaka: Mzee Mwanakijiji awaombe msamaha wananchi

Tunapinga na kulaani mawazo ya Waberoya kurahisisha mauaji ya ‘akina Bashe ‘

Nini kifanyike? Uchambuzi wa hapo juu unaonyesha uwezekano wa hoja hiyo kuibuka huko mbeleni kwa kuwa kumbukumbu za “hitaji” la “watu” kuongezewa muda zimeshawekwa. Hivyo, wanademokrasia msilale usingizi wa pono. Endeleaji kufanyia kazi namna ya kuzima mikakati ya kuongeza muda wa kuongeza urais.

cc: Ole Sendeka, Mwanakijiji, Nyani ngabu, Waberoya, wote
 
yaani kila nikisikia habari za kuongezewa miaka roho inanikereketa nachafukwa tatizo sijui ni nini ,Nahisi giza li mbele ya nchi yangu , niliyoyaona kwenye nchi jirani,na nchi nyingine machafuko yaliyotokea come on viongozi mbona mpo kimya kukemea hili,

wacha tu niishie hapa maana nitaanza kuandika visivyohitajika 😡 😡 😡 😡
 
leo unaanza kwa kuingiza kidole then kesho utaingiza nanilh,lengo langu sio kutukana ila ni kuonyesha kuwa hili suala linakuja kwa style ya mawimbi yaani leo mnaambiwa leo hivi kesho vile,repeat a lie several times,eventually it will asert itself to be a truth,kama unavyosema mkuu hapa tunaandaliwa kisaikolojia ili kesho tutakapoambiwa wangapi mnataka raisi aongezewe muda wake,tayari kama ilivyo kawaida wazee wa zidumu fikra za mwenyekiti watapata kura nyingi tayari ndio tusha liwa
Kwa akili ya kawaida,inawezekanaje Raisi amekemea kwa kufunga mjadala juu ya yeye kuongezewa muda,then wanaibuka eti watu wanaipinga kauli ya raisi yeye kupinga hili,hivi inaingia akilini kweli kama sio kutuzuga?
Mbele giza............
 
Uchambuzi yakinifu wa kisayansi..
 
Back
Top Bottom