Ufahamu mmea unaokula nyama

Ufahamu mmea unaokula nyama

Thewildlife_tz

Senior Member
Joined
Apr 23, 2019
Posts
127
Reaction score
85
UNAFAHAMU MMEA UNAOKULA NYAMA??

Huu mmea unaitwa VENUS FLYTRAP na kisayansi unaitwa Dionaea muscipula
upo katika kingdom plantae na
Order: Caryophyllale
Ni mmea unaopatikana katika bara la Amerca kaskazini western calorina

Huu mmea ni mdogo na unamatawi ambayo yana urefu wa cm 20
kila tawi lina majani yapatayo saba na kila jani limegawanyika katikati katika pande mbili zinazofanana na ukubwa wa jani ni cm 8-15

pembezoni mwa kila jani kuna structure kama nywele ndogo ndogo sana ambavyo hvi huwa ni senser kwaajili ya kugundua kama prey atagusa

katikati ya kila jani kuna rangi nyekundu hii rangi hutumika kuvutia chakula ambapo prey lazima atavutiwa na ile rangi nyekundu

Tabia kuu ya huu mmea ni kula nyama tu yaani ni CARNIVORES

Chura na reptilia na wadudu wanaliwa sana huu mmea na mara nyingi huwa unakua umechanua tayari kwa kualika prey

structure ya nje huwavutia sana prey kwenda kujificha au kwenda kupumzika
mara zote unakua na rangi anga'avu hasa muda wa mchana

Hvyo prey akishaingia katikati akaenea vizuri kwenye angle 45-60' basi hujifunga haraka sanaaa na hii inakua ni chini ya sekund 1 ila inategemea na aina ya prey

Sasa kwa kawaida huchukua prey wawili hadi watatu kama watakua wadogo ndio hujifunga ila akiwa mkubwa akagusa pande zote hujifunga

Kwa kawaida digestion huchukua siku 10 na ule wekundu unaoonekana ile ni special grand kwaajili ya kudigest chakula
na baada ya siku hzo hujifungua tena pakiwa pakavu na mng'ao ule ule

Huu mmea ni rahisi sana kukua ila ukiwa mdogo hushambuliwa sana na wadudu ukikua hata ukiukata utaota tena na kuendelea kukua labda uondoe shina..

VIDEO
DAAH!! chura katoka kwenye mishe mishe kachooka akaona ngoja akapumzike kwenye ua jekundu kumbe ndio israel anamsubiri, hapo ndio habari yake imeshaisha hata atune vipi

Huu mmea uko katika mfumo wa pingu yani ukibana prey akiforce kujitanuaa au kujizuia wenyewe ndio unabana zaidi na akilitulia unamdigest taratibu

Baada ya siku kumi hata mfupa hutaona..

Ukiangalia kushoto umeshajifunga hapo uko kwenye digestion tayari
follow instagram Thewildlife_tz
 

Attachments

  • thewildlife_tz-20190424-0001.mp4
    223.2 KB
Asee we dhehebu gani mmh..?


Wapi Mungu aliruhusu ulaji wa nyama mpaka unatamka hilo neno?.
Ulaji wa nyama ni kutokana na uroho wa mwanadamu tu...
Kasome Mambo ya Walawi 11 utaelewa
 
Asante kwa somo zuri,kumbe kuna baadhi ya watu wanapotea maporini inawezekana iko mimea mikubwa inayokula watu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom