Ufahamu mkasa wa kifo cha utata cha mwanamke wa Isdal ulioishangaza dunia (sehemu ya 1)

4G LTE

JF-Expert Member
Aug 4, 2015
6,777
10,533
IMG_20190719_215643.jpg


IMG_20190719_180654.jpg

Bonde la Isdalen karibu na jiji la Bergen, Norway linajulikana kama bonde la kifo/umauti "death valley" kwa wakazi wa eneo hilo si kwa sababu watembezi/watalii hupotelea kwenye mlima wa bonde hili mara kwa mara, ila kwa sababu kipindi cha nyuma kwenye miteremko ya mlima huo watu walikuwa wanajiua.

IMG_20190719_181123.jpg



IMG_20190719_181239.jpg

Lakini kwenye kesi ya mwanamke huyu hakuonekana kama mtembezi/mtalii. Tuanze kwa kuangalia namna ya mwili wa mwanamke huyu ulivyookotwa. Ulikuwa mchana wa Novemba 29,1970 ambapo familia moja ambayo ilikuwa na baba na binti wawili wenye asili ya Norway walikuwa wakienda kutalii katika mlima Ulriken upatikanao katika jiji la Bergen, watalii wengi hupenda kupanda mlima huo uliojaa barafu na nchi ya Norway ni nchi ya baridi kali na barafu. Kabla ya kuanza kupanda mlima huu kuna bonde kubwa ambalo upande mmoja una barafu na upande mwingine hauna barafu nalo ni kivutio cha utalii.

Familia hii ilipita upande wa bonde usiokuwa na barafu ambapo kumejaa mawe makubwa na miamba na wakiwa wakimalizia bonde hili, mmoja wa watoto wa mzee huyu akaona saa kwenye moja ya jiwe kubwa. Yule mtoto akakimbilia kwenye lile jiwe aliloona saa huku familia yake ikimshangaa anaelekea wapi na kuanza kumuita kwasababu huko alikokuwa anaelekea kulikuwa na mawe ambayo yametengeneza maficho ya kutisha ambayo ni hatari pia.

Mtoto huyo alipokaribia saa, akaona kitu kilichomshtua na kumfanya apige ukelele na kuifanya familia yake kushtuka na kumkimbilia kule alikokuwa kujua sababu ya ukelele huo ni nini, na kama nilivyoelezea hapo alikuwa eneo hatarishi. Wakakutana na mwili wa mwanamke ambao umeungua na kuharibika sana hata kutambulika ni vigumu, hapo hapo baba wa familia hiyo akatoa taarifa polisi. Mtaa karibia na bonde hilo kulikuwa na polisi mwanasheria ambae ndiye wa kwanza taarifa hizi kumfikia ambaye aliitwa Carl Halvor Aas, ambapo aliuona mwili wa mwanamke huyu ukiwa umeungua sana huku amelala chali huku mikono yake ikiwa imeelekea juu na kutengeneza utata flani kuwa labda alikuwa anajitetea au ndio pozi la kukata roho.

Afande huyu hisia zake za haraka zikamuongoza kuwa ni tukio la kujitoa roho na ukizingazia historia ya bonde hili "death valley"....maiti ya mwanamke huyu ilikuwa imezungukwa na vitu vinavyoaminika ni vya kwake, hata walipoenda kupima DNA walikuta ni vya kwake. Juu ya jiwe mojawapo kulikuwa na saa ya kike nzuri, bangili na hereni za kuvutia.

IMG_20190719_181407.jpg


Chini pembeni ya mwanamke huyu kulikuwa na mwavuli uliovunjika, galoni la mafuta, chupa mbili za vinywaji zilizotupu, nguo nzito na hapa ni kwasababu ni nchi ya baridi na kingine kilichokutwa na viatu.

IMG_20190719_182018.jpg


IMG_20190719_181623.jpg


IMG_20190719_181749.jpg


Wapelelezi wakaanza kuvikagua hivi vitu, huku wakivikusanya kwa ajili ya ushahidi na uchnguzi zaidi na kilichowashangaza zaidi nguo na chupa zimeondolewa label zake za utambuzi na kuzidi kuwachanganya wapelelzi hao na jinsi vitu hivyo vilivyosambazwa kama alivivua na kuviweka hapo. Wakaendelea na kuchunguza mwili ukiwa hapo eneo la tukio na wakiwa na mfuko wa kubebea maiti.

Lakini ghafla wakiwa kwenye harakati za kuubeba mwili huo, walishtushwa walipokuwa wanataka kuubeba na kukuta hajaungua sehemu ya nyuma kabisa kwani ni hali isiyo ya kawaida mwili uungue sana eneo la mbele tu. Shingoni pia walikuta mikwaruzo/michubuko na maswali mengi yakazuka na kuzidi kuchachua hisia zao za awali kuwa kama alijichoma moto mwenyewe iweje asiungue sehemu ya nyuma?

Wapelelezi wakaondoka na mwili na vitu vyote walivyovikuta eneo la tukio kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kitabibu na baadhi ya wapelelezi wakabakia eneo la tukio kuchunguza kama wataona kiashiria kingine chochote. Wakati wakiendelea kuangalia huku na huko wakagundua sehemu familia ile ilipougundua mwili huo si njia ya kupanda mlimani na familia ile ilijieleza kuwa ilikuwa na safari ya kupanda mlima hata afande Carl alithibitisha kwa mizigo na mavazi yao yalikuwa yanadhihirisha walikuwa wanapanda mlima. Wapelelezi wakaamua kuwaweka kiporo maana hakukuwa na ushahidi wa kutosha kuhusika na tukio hili, na si kuwa njia hii haifikishi watu mlimani bali si njia rasmi maana ilifungwa baada ya kusababisha maafa kwa watu waliokuwa wanapanda mlimani ambapo miaka ya 1960 kundi flani lilianguka na kupoteza maisha lote, hivyo serikali ya Norway ikafunga njia hiyo.

Hospitalini madaktari wakafanya uchunguzi na majibu yakatoka na yakazidi kuwavuruga wapelelezi hao, kwani tumboni walikuta takribani vidonge 70 vya usingizi ambavyo havijayeyuka na kuingia kwenye mishipa ya damu ili viweze kuleta matokeo pia mapafu yake yalikuwa na moshi na hitimisho likawa mwanamke huyo alichomwa/alijichoma moto mwenyewe.

Vichwa vikazidi kupata moto, kwamba ni nini kilichotokea kwa huyu mwanamke maana dawa ukishameza zinayeyuka mwilini na kwa ripoti hii inamaana alikata roho kabla dawa hazijaanza kufanya kazi na ukichanganya upatikanaji wa moshi kwenye mapafu inahitimisha kuwa kilichomuua ni moto huo. Wapelelezi wakapata picha kuwa mwanamke huyu alikufa kifo cha mateso na kikatili sana cha kuchomwa moto akiwa hai. Swali la kwanini hakuungua maeneo ya mgongoni, wapelelezi na madaktari kwa muda huo wakashindwa kung'amua kwani mtu akichomwa moto akiwa hai maanake angejiviringisha na hata moto kusambaa maeneo mengine mwilini ikiwamo mgongoni.

Taarifa za mwanamke huyu zilisambaa kote Norway ili kama kuna ndugu, jamaa au rafiki aliepotelewa na mtu wake aweze kuripoti polisi, hakuna yeyote aliejitokeza na hakuna taarifa yoyote polisi kuhusiana na mwanamke mwenye sifa hizo.

Siku ya nne wapelelezi wakiendelea kukuna vichwa vyao, akajitokeza jamaa mmoja na kuanza kuongea na wapelelezi kuhusu mwanamke huyo ambae bado hajajulikana.
Huyu mtu alikuwa muuzaji wa duka kubwa la nguo na viatu jijini Bergen na alikuwa shahidi wa kwanza kusema anamfahamu huyo mwanamke kwani alishakuja dukani kwake kununua viatu hivyo ambavyo vilitangazwa kwenye vyombo vya habari.

Viatu alivyokutwa navyo mwanamke huyu kwa wakati huo vilijukikana kama "Celebrity boots", ambavyo bei yake ilikuwa juu sana kioindi hicho, hivyo vilivaliwa na wachache sana.

IMG_20190719_232518.jpg


Wapelelezi wakataka picha ya mwanamke huyo inafananaje maana uso na nyweke zake zilikuwa zimeungua kiasi cha kutofahamika na ndipo muuza duka huyo akaanza kuwaelezea anavyofanana na ndipo sasa wapelelezi wakafanikiwa kuchora taswira yake kwa maelezo ya muuza duka huyo.

Kwa picha hiyo, bado hakuna aliejitokeza kuwa anamfahamu na ndipo wapelelezi wakambatiza jina la Isdal huku wakiendelea na uchunguzi wao, wakati mambo haya yakiendelea polisi jijini Bergen wakapata taarifa kutoka kwenye station ya treni jijini apo kuwa kuna mizigo iliachwa hapo kwa muda mrefu na haijulikani ni ya nani! Polisi wakaelekeza ipelekwe kituoni kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Mizigo yenyewe ilikuwa masanduku na briefcase kubwa mbili, moja ya rangi nyeusi na nyingine rangi ya fedha.

IMG_20190719_182053.jpg


Baada ya kufikishwa kituoni, mizigo ikakaguliwa na kifaa maalumu cha kukagulia mabomu na vilipukizi ili isije kuwa ni mtego wa bomu maana miaka hiyo ilikuwa ndio kipindi cha vita baridi na Norway ilikuwa imetoka kujaribisha kombora lake la masafa marefu, hivyo kuwa tishio kwa nchi nyingine. Kifaa kikaonesha kuwa masanduku hayo hayana shida yoyote, ikabidi sasa kuyafungua na kuanza kutoa vilivyomo, katika masunduku hayo kulikutwa na vitu kama nguo za ndani za kike, mawigi, fedha za kigeni za Ujerumani, Norway na sarafu za kigeni za Uingereza na Uswizi, chanuo na brush, manukato, vijiko vya chai, cream, mfuko wa Oscar Rortvedt's Foot wear store ambapo ni duka la viatu huko Stavanger, miwani, paspoti za nchi 8,diary na business cards.

Polisi wakaingiwa na wasiwasi baada ya kukuta vitu hivyo na kilichowapa waswasi sana ni mfuko huo wa Oscar Rortvedt's na kuamua kuyapeleka mbele masanduko hayo kwa wapelelezi maana huo mfuko ni wa lile duka kubwa la nguo na viatu la yule jamaa ambae alisaidia kupatikana kwa taswira ya mwanamke huyu wa Isdal...

ITAENDELEA......
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom