Ufahamu mji wa Tarshishi(Lebanoni)

Jackwillpower

JF-Expert Member
Oct 4, 2017
2,301
3,411
Mji wa Tarshishi ni mji ambao ulikuwa mahali panapoitwa Tiro.. ambapo kwa sasa ni nchi ya Lebanoni… Nchi ya Lebanoni ni nchi iliyopo kaskazini mwa Israeli, kama vile Kenya ilivyo kaskazini mwa Tanzania (Na mpaka leo hiyo nchi inaitwa hivyo hivyo Lebanoni haijabadilika, inakaliwa na Waarabu sasahivi, lakini haina tena utajiri/ushupavu uliokuwa nao wakati ule)..

Sasa wakati wa vipindi vya wafalme wa Israeli nchi hii ya Tiro (Lebanoni) ambao mji wake mkuu ni Tarshishi ndio ulikuwa ni mji wa kibiashara mkubwa kuliko miji mingine yote. Ulikuwa unasifika kwa kuwa na MERIKEBU NYINGI ZA KIBIASHARA kuliko miji mingine yote. Na ulikuwa ni mji wenye uzoefu wa ki-biashara

Biblia inasema katika kitabu cha Ezekieli…

Ezekieli 27:12 “Tarshishi alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa utajiri wa kila aina; kwa fedha, na chuma, na bati, na risasi, walifanya biashara, wapate vitu vyako vilivyouzwa”
Yeremia 10: 9 “Iko fedha iliyofuliwa ikawa mabamba, iliyoletwa kutoka Tarshishi, na dhahabu kutoka Ufazi,….”.
Unaona? Vilevile Miti ya Mierezi ambayo ilitumika katika ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani, ilitoka huko Lebanoni, kulikuwa hakuna mahali pengine ambapo miti hiyo ilikuwa inapatikana, na njia ya usafirishaji iliyokuwa inatumika kusafirishia miti hiyo ni bahari (Njia ya Maji). Kwa ufupi sehemu kubwa ya malighafi za ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani zilitoka huko Tiro, ambao mji wake mkuu ni Tarshishi. Hata Dhahabu Sulemani alizozitumia kutengenezea vyombo vyake zilitoka huko Lebanoni..Sulemani alinunua dhahabu nyingi kutoka huko Lebanoni mpaka kufikia kiwango cha kuwa tajiri sana hata kuona kutumia madini ya fedha(silver) kutengenezea vito vyake ni kama kujishushia heshima..

1Wafalme 10: 21 “Na vyombo vyote vya kunywea vya mfalme Sulemani vilikuwa vya dhahabu, na vyombo vyote vya nyumba ya mwitu wa Lebanoni vilikuwa vya dhahabu iliyosafika; hakuna vya fedha, fedha haikuhesabiwa kuwa kitu siku za Sulemani.
22 Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.
23 Basi mfalme Sulemani akawapita wafalme wote wa duniani kwa mali, na kwa hekima.”
Huko Tarshishi walikuwepo pia manahodha waliobobea sana, na pia kulikuwa na watu wenye elimu ya ujenzi kubwa sana..baadhi ya wajenzi wa hekalu lile la mfalme Sulemani aliwatolea huko huko Lebanoni.

Hivyo ipo mistari mingi sana katika biblia inayoelezea ushupavu wa Tarshishi…ipo mingi sana unaweza kuipitia kwa muda wako upatapo nafasi…Kasome (Ezekieli 27: 25-27, Ezekieli 38:13, 1Wafalme 22: 48, ).

Sasa kwa kuielewa sifa ya Huu mji wa wa Tarshishi tunaweza kujua ni kwanini Yona alikimbilia huko…Na kwanini alipanda merikebu…Kumbuka kutoka Israeli mpaka Tarshishi(huko Lebanoni) kulikuwepo na njia ya nchi kavu nzuri tu..lakini yeye alikwenda kupanda merikebu. Ni sawa leo mtu atake kwenda Tanga..aache kupanda basi achague kutumia ferry/meli pale bandarini Dar es salaam aende Tanga. Ni lazima anayo sababu ya kufanya hivyo..

Na ni wazi kuwa sababu yenyewe si nyingine Zaidi ya biashara…Yona pengine alikuwa na mizigo yake anakwenda kufanya biashara.. Tarshishi haukuwa mji wa kitalii..ulikuwa ni mji wa kibiashara..hivyo alipoisikia sauti ya Mungu ikimwambia aende Ninawi kuhubiri yeye akaona njia pekee ya kuipotezea hiyo sauti ni kuzama kwenye biashara zake…wala hakuchagua kukimbilia miji mingine kama Misri, au Moabu ambayo angepata pumziko..yeye alikuwa na sababu ya kwenda Tarshishi.. Angalau apate riziki kidogo.
1648299879256.png

1648299904282.png

1648299961235.png
 
Mji wa Tarshishi ni mji ambao ulikuwa mahali panapoitwa Tiro..ambapo kwa sasa ni nchi ya Lebanoni…Nchi ya Lebanoni ni nchi iliyopo kaskazini mwa Israeli, kama vile Kenya ilivyo kaskazini mwa Tanzania (Na mpaka leo hiyo nchi inaitwa hivyo hivyo Lebanoni haijabadilika, inakaliwa na Waarabu sasahivi, lakini haina tena utajiri/ushupavu uliokuwa nao wakati ule)..

Sasa wakati wa vipindi vya wafalme wa Israeli nchi hii ya Tiro (Lebanoni) ambao mji wake mkuu ni Tarshishi ndio ulikuwa ni mji wa kibiashara mkubwa kuliko miji mingine yote. Ulikuwa unasifika kwa kuwa na MERIKEBU NYINGI ZA KIBIASHARA kuliko miji mingine yote. Na ulikuwa ni mji wenye uzoefu wa ki-biashara

Biblia inasema katika kitabu cha Ezekieli…

Unaona? Vilevile Miti ya Mierezi ambayo ilitumika katika ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani, ilitoka huko Lebanoni, kulikuwa hakuna mahali pengine ambapo miti hiyo ilikuwa inapatikana, na njia ya usafirishaji iliyokuwa inatumika kusafirishia miti hiyo ni bahari (Njia ya Maji). Kwa ufupi sehemu kubwa ya malighafi za ujenzi wa hekalu la kwanza la Sulemani zilitoka huko Tiro, ambao mji wake mkuu ni Tarshishi. Hata Dhahabu Sulemani alizozitumia kutengenezea vyombo vyake zilitoka huko Lebanoni..Sulemani alinunua dhahabu nyingi kutoka huko Lebanoni mpaka kufikia kiwango cha kuwa tajiri sana hata kuona kutumia madini ya fedha(silver) kutengenezea vito vyake ni kama kujishushia heshima..

Huko Tarshishi walikuwepo pia manahodha waliobobea sana, na pia kulikuwa na watu wenye elimu ya ujenzi kubwa sana..baadhi ya wajenzi wa hekalu lile la mfalme Sulemani aliwatolea huko huko Lebanoni.

Hivyo ipo mistari mingi sana katika biblia inayoelezea ushupavu wa Tarshishi…ipo mingi sana unaweza kuipitia kwa muda wako upatapo nafasi…Kasome (Ezekieli 27: 25-27, Ezekieli 38:13, 1Wafalme 22: 48, ).

Sasa kwa kuielewa sifa ya Huu mji wa wa Tarshishi tunaweza kujua ni kwanini Yona alikimbilia huko…Na kwanini alipanda merikebu…Kumbuka kutoka Israeli mpaka Tarshishi(huko Lebanoni) kulikuwepo na njia ya nchi kavu nzuri tu..lakini yeye alikwenda kupanda merikebu. Ni sawa leo mtu atake kwenda Tanga..aache kupanda basi achague kutumia ferry/meli pale bandarini Dar es salaam aende Tanga. Ni lazima anayo sababu ya kufanya hivyo..

Na ni wazi kuwa sababu yenyewe si nyingine Zaidi ya biashara…Yona pengine alikuwa na mizigo yake anakwenda kufanya biashara.. Tarshishi haukuwa mji wa kitalii..ulikuwa ni mji wa kibiashara..hivyo alipoisikia sauti ya Mungu ikimwambia aende Ninawi kuhubiri yeye akaona njia pekee ya kuipotezea hiyo sauti ni kuzama kwenye biashara zake…wala hakuchagua kukimbilia miji mingine kama Misri, au Moabu ambayo angepata pumziko..yeye alikuwa na sababu ya kwenda Tarshishi.. Angalau apate riziki kidogo.
View attachment 2165104
View attachment 2165105
View attachment 2165106
Nimebahatika kufika eneo hili la Baalbek, lililopo katika mji Tyre nchini Lebanon, sehemu hii ndio inasadikika Samson mtu aliyekuwa na nguvu kama Simba alivunja nguzo zilizokuwa zimeshikilia jengo, na kusababisha jengo hilo kuporomoka.
 
Kwa nyongeza tu Lebanon ndo alipotoka mwanamke katili Jezebel mke wa Ahab kwenye Biblia.

Mwanama huyu aliogopwa kwa Ukatili na alileta miungu yake ya Baal Israel. Alimpelekesha sana Nabii Elijah.

Alitokea mji wa Sidon kusin mwa Lebanon sasa hivi ngome kuu ya Hezbollah.

Lebanese walijulikana zamani kama Phoenician wafanyabiashara wakubwa sana long distance traders.

Kivutio cha Lebanon ni miti aina ya Cedar. Hii miti ni mingi sana Lebanon enzi na enzi na ni nembo yao ya taifa hata kwenye benders yao ipo.
lebanon-flag.jpg
lippu-libanon.png
 
View attachment 2165134View attachment 2165135
Na pia Lebanon ndipo alipotoka mwanamke mrembo aitwaye Delilah, aliyesababisha Samson kunyolewa nywele, kitendo kilichopelekea kuishiwa nguvu na hatimaye kukamatwa na Wafilisti.
 
Kwa nyongeza tu Lebanon ndo alipotoka mwanamke katili Jezebel mke wa Ahab kwenye Biblia.

Mwanama huyu aliogopwa kwa Ukatili na alileta miungu yake ya Baal Israel. Alimpelekesha sana Nabii Elijah.

Alitokea mji wa Sidon kusin mwa Lebanon sasa hivi ngome kuu ya Hezbollah.

Lebanese walijulikana zamani kama Phoenician wafanyabiashara wakubwa sana long distance traders.

Kivutio cha Lebanon ni miti aina ya Cedar. Hii miti ni mingi sana Lebanon enzi na enzi na ni nembo yao ya taifa hata kwenye benders yao ipo.
View attachment 2165134View attachment 2165135
ubarikiwe sana mkuu
 
hii miti huitwa mierezi,
 
Delilah alitokea the valley of Sorek Gazza. Na ndie mwanamke pekee wa Samson aliotembea nao ametajwa jina lake. Wengine wote hawajatajwa majina yao.

She was a Phillistine from Sorek valley Gazza strip.
upo sahihi mkuu,ubarikiwe
 
Asante ufafanuzi mzuri.

Nasikia hakuna anayejua lilipojengwa hekalu la Solomon.
Dada Hekalu la Sulemani si lilikuwepo hapo uliopo msikiti wa Al Aqsa au Dome of Rock kwenye mlima Moria maana lilibomolewa na Nebukadineza ila lilikuja simamishwa mara ya pili na akina Zerubabeli na Yoshua Kuhani ambalo Yesu alilikuta kisha kuja kuharibiwa na Warumi au mimi sijakuelewa?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom