Ufahamu kuhusu kuandikishiana viwanja

bobtony

Member
Jun 28, 2015
44
37
Wadau habari zenu humu ndani!
Rejea kichwa cha habari, naombeni maelekezo kwa mwenye uelewa zaidi juu ya namna ya kuandikishana katika uuzaji wa kiwanja.

Nimenunua kiwanja eneo la kijiji ambalo ni shamba kama ekari 6, mwenye shamba kaniuzia ekari moja, utata naoupata ni pesa halisi za kuwalipa hawa viongozi wa serikali ya kijiji, maana kila ninaemuuliza maeneo tofauti natajiwa ni kama elfu 70, Mara wengine asilimia 10 ni ya kijiji, naombeni mwenye ufahamu zaidi anisaidie juu ya hili.

Mungu awabariki!
 
Inatakiwa itoke asilimia 10 kwa ajili ya kijiji that means ww utatoa 5% na muuzaji atatoa 5% zaidi ya hapo jiandae mizinga ya mashahidi na wapimaji...
 
Mkuu Moe junior nimekuelewa vyema na hii kazi Mungu akipenda naenda kuifanya kesho, mashaidi tayari nimeshawaandaa, ila hii pesa halisi ndo nataka kuijua, maana sehemu yenyewe ilipo hiyo plot kwa baadae najua itakua ni potential na haipo mbali na barabara, nataka kujua ili nijue naenda na pesa kiasi gani ili nikamilishe taratibu.
 
Malipo hufanywa kulingana na mapatano, ila 10% ya kijiji ni lazima. Mashahidi utawalipa sawa na patano lenu, wanakamati wa serikali ya kijiji inabidi mpatane kwanza ili washiriki katika mauzo husika.

Kuna vijiji ambavyo, kamati ya ardhi ya kijiji ndiyo yenye nguvu na ndio inayochukua posho na wote wanasaini kwenye document yako, sasa kama wakija lundo ( pwani wanapenda mtindo huu) ndio utalijua jiji. Mtindo huu naupenda sababu unashirikisha wadau wa ardhi wa kijiji wakiwa wengi, ila sasa mfuko unatoboka. Na VEO/Mtendaji anapewa taarifa za kilichofanyika na kukupa hati.

Ukiona mnauziana bila mjumbe wa kamati ya ardhi, jua hilo famba, na kama ardhi ni ya familia, omba upate kopi ya mhitasari wa kikao cha familia husika. Watu siku hizi ni vimeo. Kama ardhi mali ya kijiji, kama sio lazima sana bora usinunue, zinasumbua ile mbaya, kama ni lazima, hakikisha mkutano wa kijiji umefanyika na upate kopi ya maandishi.
 
Ofisi ya kijiji huwa wanakula 10% na kuna ingine kidogo kwa ajili ya baraza la ardhi na mashahidi wako siku hiyo wengi hujiandaa kwa kula nyma choma ni 10, 10 mfukoni....Ningekushauri usihurumie pesa sana kwenye kitu chako unachotegemea kuwa nacho mda mrefu..Kikubwa we hakikisha njia zote stahiki unapitia hata wakikuambia lete laki kama upo nayo we toa....Na ukimliza na kijiji mkataba uandikishwe kwa mwanasheria anaetambulika kabisa na si wale wanaoitwa msajili wa umma....Kupitia kuwa karibu na baraza la ardhi la mahali fulan na viongozi wote wa kijiji kuwapiga vipesa kidogo walikuja kuwa msaada mkubwa sana pale aliponiuzia eneo langu alipotakaga kunipora ili auze tena...Na akawa na courage hadi ya kupeleka kesi mahakamani...Kisa anasema yeye ni mwisho kwao na kaka ake mmoja amesema hajakubali eneo hilo liuzwe kwa hiyo yupo tayar kurudisha the same amount niliyonunulia na ishapita miezi 6....Ila nilishinda ile kesi nikapiga ukuta eneo lote baada ya muda nikaliuza na mimi kwa super profit....So tengeneza mazingira mazuri leo kwani hujui kesho mkuu.
 
Shukrani wakuu manuu na malila, sehemu yenyewe ni huku Arusha aisee asanteni sana kwa mawazo yenu, naamini nimepata mwanga wa kwenda kufanya Kesho.Mungu awabariki sana!!
 
Back
Top Bottom