Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,973
- 30,154
Hii web mbona haifunguki??Mkuu kama bado hujapata majibu tembelea www.kilimo.go.tz kuna pdf ya kilimo cha pilipili mtama.
Au kwako Mkuu Tiba inafunguka??
Hii web mbona haifunguki??Mkuu kama bado hujapata majibu tembelea www.kilimo.go.tz kuna pdf ya kilimo cha pilipili mtama.
Ni kweli nimejaribu haifunguki mkuu. Nadhani wataalam IT wa wizara wapo usingizini.Hii web mbona haifunguki??
Au kwako Mkuu Tiba inafunguka??
Hii hapa kama kule wizarani kuna mizenguo....Asante ngoja ni google.
Tiba
Ahsante Mkuu.Hii hapa kama kule wizarani kuna mizenguo....
KILIMO BORA CHA PILIPILI MANGA
Utangulizi
Jina la kiingereza ni Black pepper. Zao hili asili yake ni Mashariki ya Mbali, na linalimwa zaidi katika mkoa wa Tanga na Zanzibar.
Matumizi
Pilipili nyeusi na nyeupe zote hutumika kwa mapishi ya nyama, samaki na kwa mapishi mengine mbalimbali. Nchi za magharibi zina matumizi makubwa ya viungo hivi. Aidha pilipili mtama nyeusi ndiyo huzalishwa zaidi hapa nchini.
Uzalishaji
• Hali ya hewa na udongo
Viungo vingi humea katika maeneo yenye joto la wastani kati ya nyuzi joto 24-26 na huzalishwa maeneo ya mwambao. Udongo wenye rutuba na unaopitisha maji na wenye uchachu wa kiasi cha pH 6.5. Mahitaji ya mvua ni mililita 1500-2000 kwa mwaka.
• Uchaguzi wa mbegu
Uchaguzi huzingatia mambo yafuatayo:-
a) Urefu wa pingili na ukubwa wa majani
b) Ufupi wa pingili unaoambatana na majani madogo.
Tofauti iko hadi kwenye umbile la matunda. Majani ya mche mama sehemu kinapokatwa kipando huondolewa wiki mbili kabla ya kukata. Vipando vyenye macho (nodes) 3-4 humika. Macho mawili huzikwa kwenye udongo na kipando kiwekewe kivuli. Inashauriwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa kupanda.
• Nafasi ya upandaji
Nafasi ya kupanda ni mita 2-3 kati ya mmea na mmea endapo miche imepandwa na miti inayotakiwa kupogolewa mara kwa mara.
• Mahitaji ya mbolea
Matumizi ya mbolea hapa Tanzania si makubwa katika kilimo cha viungo. Ingawa kiasi cha kilo 0.4 cha Urea, kilo 0.3 cha Superphosphate na kilo 0.3 cha Potash ya Muriate kinaweza kutumika kwa miche mikubwa.
• Miti ya kusimikia miche
Miche hupandwa kwa kusimikiwa nguzo ili ikue kwa kujizungusha kwenye miti kama mijenga ua, n.k. Mti huo wa kusimikia nao pia hupaswa kupunguziwa majani ili kupunguza giza. Kila kabla ya msimu miti hiyo hupaswa kupunguziwa matawi (pruning).
Kupogolea miche ya pilipili mtama
Mche ukifikia miezi 18 inapaswa kupogolea kwa kukata sehemu ya juu ya mche ili kufanya matawi mengine yachipue chini ya mche. Inashauriwa mche kuwa na urefu wa mita 3-3.5.
Uvunaji
Maua ya kwanza hutoka baada ya miaka miwili. Matunda hukomaa miezi tisa (9) hadi kumi (10).
Uvunaji ni mizunguko 5 hadi 6 kwa mwaka. Pilipili mtama inaweza kuvunwa kwa misimu miwili. Mavuno ni kati ya tani 0.35-3.75 kwa hekta.
Kuhifadhi
Pilipili mtama inaweza ikawekwa kwenye chombo kisichopitisha hewa na kudumu kwa miaka 20 bila kuharibika.
Mashambulizi ya wadudu na magonjwa
Hapa nchini hakuna matatizo makubwa ya wadudu na magonjwa.
Masoko
Soko la pilipili matama linapatikana ndani ya nchi na nje pia. Bei ya ndani ni kati ya Sh1,0000-1,5000.
Wadau,
Nimetonywa na mtu kwamba zao la pilipili manga lina soko na kwa bei nzuri kwenye nchi za kiarabu. Nilitaka kujaribu kulima ili zao. Je kuna anayejua kilimo hiki kinaendeshwaje? Nataka kujua kama unapanda mbegu kwenye matuta au ni plain land, je ni zao linalostahimili ukame au mvua nyingi ni lazima? Na kwa hapa Tanzania hili zao linalimwa wapi?
Msaada tafadhali. Ili zao linaweza kunitoa kwenye umasikini.
Tiba
Asante Dada Faiza Foxy.= hili
= hili
Hiyo miche ya Karafuu sio pilipili MangaGharama za kilimo zikoje kwa heka moja??
Mie mkuu nipo kibiti.Kama humu ndani kuna mtu ni mkulima wa pilipili(sio hoho)
Naomba uje PM natafuta wakulima wa pilipili
Njoo PM mkuuMie mkuu nipo kibiti.
original seeds sealed utavuna miaka mtano straight mpaka unatoka nduki...sio mimbegu ya kariakoo full kuchakachuliwa...Hizo ndio mbegu bora za pili pili mbuzi....carribean red habanero
Unauza mkuu?Hizo ndio mbegu bora za pili pili mbuzi....carribean red habanero
Mkuu bei ya pilipili mbuzi aina hiyo sokoni inaendaje? Kiroba kwa sasa?original seeds sealed utavuna miaka mtano straight mpaka unatoka nduki...sio mimbegu ya kariakoo full kuchakachuliwa...
Bei inabadilika badilika sana. Kwa sasa roba moja ni sh elfu 30-40.Mkuu bei ya pilipili mbuzi aina hiyo sokoni inaendaje? Kiroba kwa sasa?