Ufahamu juu ya kilimo cha pilipili mbuzi

masandare

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2014
Posts
671
Reaction score
584
Habar jf
Nahitaji kulima zao la pilipili mbuzi, lakini tatizo langu sina elimu ya kutosha kuhusiana na ulimaji pamoja na soko lake
Naomba yeyote mwenye ufahamu japo kidogo anijuze.

NAWASILISHA
 
Wadau,

Nimetonywa na mtu kwamba zao la pilipili manga lina soko na kwa bei nzuri kwenye nchi za kiarabu. Nilitaka kujaribu kulima ili zao. Je kuna anayejua kilimo hiki kinaendeshwaje? Nataka kujua kama unapanda mbegu kwenye matuta au ni plain land, je ni zao linalostahimili ukame au mvua nyingi ni lazima? Na kwa hapa Tanzania hili zao linalimwa wapi?

Msaada tafadhali. Ili zao linaweza kunitoa kwenye umasikini.

Tiba
 
Bull Dog kanichomekea mchana kweupe !!!!!!

Kuna wakati nilitaka kwenda Morogoro kuona kilimo cha pilipili Mtama kule milimani, nikakosa usafiri. Asante kwa homework, ngoja niingie chaka nikaone kilichoko, nami nikipata nitarusha hadharani.

Si uongo Bulldog kachapia kumbe? UKipata chochote tutupie hapa. Natanguliza shukrani.

Inaitwa Black pepper kwa lugha za watu wa Uk, kwa wingi inalimwa India, na hapa Tz inalimwa Unguja na Pemba. Kwa leo niishie hapa. Ingia kwa google, andika black pepper farming, kitu kinakuja kiulaini.
 
Asante ngoja ni google.

Tiba
 
Wadau,

Nimetonywa na mtu kwamba zao la pilipili manga lina soko na kwa bei nzuri kwenye nchi za kiarabu. Nilitaka kujaribu kulima ili zao. Je kuna anayejua kilimo hiki kinaendeshwaje? Nataka kujua kama unapanda mbegu kwenye matuta au ni plain land, je ni zao linalostahimili ukame au mvua nyingi ni lazima? Na kwa hapa Tanzania hili zao linalimwa wapi?

Msaada tafadhali. Ili zao linaweza kunitoa kwenye umasikini.

Tiba

IMG_27771-300x225.jpg

Pilipili manga zinastawi na kulimwa sana maeneo ya Amani Muheza Tanga (Usambara Mashariki). Pilipili manga zinapandwa kama vile unavyopanda matunda ya mipensheni. Shamba lako ni lazima liwe na idadi kubwa ya miti, miche ya pipili manga huoteshwa chini ya mti na kutambaa na mti hadi kileleni (tazama picha hapo juu). Kama shamba lako lina vyanzo vizuri vya maji na ukawa unamwagilia kila wakati ndiyo pilipili manga inavyochanua maua na kupata vikonyo vingi vya mbegu kama vinavyoonekana hapa chini.

Pilipili manga haina msimu jinsi inavyopata maji ndiyo huchanua mwaka mzima na inadumu zaidi ya miaka mitano, mazao yakianza kuwa hafifu unang'oa na kupanda pilipili mpya.

1364590123-farm-workers-pick-black-peppers-in-india_1918638.jpg
 
Kama utahitaji mbegu na ushauri, funga safari hadi Muheza Tanga, kutoka Muheza panda daladala zinazoenda Amani, muombe kondakita akushushe kiwanda cha pilipili au Jumuiya ya Wakulima wa Kilimo Hai Usambara Mashariki (JUWAKIHUMA) ni safari ya nusu saa kutoka muheza mjini.

Wanavyo vitalu na mbegu za kutosha.

P1020187.JPG
 
Asante mkuu kwa ushauri wa kitaalamu. Kwa ujuzi wako wa ili zao, linaweza kutoa mazao mazuri upande huu wa Bagamoyo?

Sina hakika sana kwa huu ukanda wa pwani kama inawezekana, lakini pilipili manga pia inastawi vizuri sana kisiwani Pemba. Kama hali ya hewa Bagamoyo ni sawa au zinakaribiana na Pemba jaribu kupanda miche michache. Kama hali ya hewa ni ya joto sana itastawi lakini itadondosha maua na hutapata vikonyo nyenye mbegu.
 
Black pepper tolerates temperature between 10°C and 40°C.
 
Kama utahitaji mbegu na ushauri, funga safari hadi Muheza Tanga, kutoka Muheza panda daladala zinazoenda Amani, muombe kondakita akushushe kiwanda cha pilipili au Jumuiya ya Wakulima wa Kilimo Hai Usambara Mashariki (JUWAKIHUMA) ni safari ya nusu saa kutoka muheza mjini.

Wanavyo vitalu na mbegu za kutosha.

P1020187.JPG
Gharama za kilimo zikoje kwa heka moja??
 
Wadau,

Nimetonywa na mtu kwamba zao la pilipili manga lina soko na kwa bei nzuri kwenye nchi za kiarabu. Nilitaka kujaribu kulima ili zao. Je kuna anayejua kilimo hiki kinaendeshwaje? Nataka kujua kama unapanda mbegu kwenye matuta au ni plain land, je ni zao linalostahimili ukame au mvua nyingi ni lazima? Na kwa hapa Tanzania hili zao linalimwa wapi?

Msaada tafadhali. Ili zao linaweza kunitoa kwenye umasikini.

Tiba
Mkuu kama bado hujapata majibu tembelea www.kilimo.go.tz kuna pdf ya kilimo cha pilipili mtama.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom