Hii simu yangu ina internal storage ya 256MB lakini nikihesabu application zote jumla yake ni 109.44MB nashindwa kuelewa MB nyingine zimeenda wapi maana inaonesha nafasi iliyobaki ni 23.23 MB,kwa anaefaham anifafanulie
Hapo ni ku clear cache. Au uliweka memory card then uka install App halafu memory ikatolewa nenda setting kwenye application angalia ile list ya app je ndizo zinazo display ktk screen, ukiona kuna jina la app yenye maandishi ya kufifia lkn kweny screen huwa huioni clear hiyo app. Nb angalia kama ni built in itakataa kufutika.
Kuna baadhi ya apps zinachofanya nikuclear tu baadhi ya cache ndomana mtu anawezafanya yote hayo na bado akaona space bado ndogo.
Unaezatumia es explorer kufanya analysing ya storage zako ili ujue file lipi limekula space na ukifungua file kama DCIM, file lapicha utakuta vifile kama .thumbnails lina MB zaidi ata ya 60, unachofanya nikufuta tu.
Na baadhi ya apps huwa zinaeka online automatic downloads plugins zisizo na maana, hasa apps zakuedit picha, huwa zinakuwa ktk database ya app kwahiyo ata utumie app mlizoeka hapa huwez futa.
Na vile vile unaweza extract file la app uliyoinstall tayari kwakutumia ES app manager
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.