RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kupitia akaunti yake ya Facebook amesema kuwa hajapiga marufuku matumizi ya vilainishi bali amepiga marufuku mashirika yasiyo ya Kiserikali kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Kauli yake nimekuwekea hapa chini;
Sijapiga marufuku matumizi ya Vilainishi nchini.
Ukweli: Nimepiga marufuku mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) kununua na kuzambaza vilainishi kwa Wanaume wanaojihusisha na mapenzi na Wanaume Wenzao. Sababu nimeshazieleza.
Hivyo, nafurahi kuwajulisha kuwa tayari baadhi ya Mashirika hayo yameanza kutekeleza agizo hili kwa kuanza kuondoa vilainishi kwenye miradi yao. NAYAPONGEZA SANA. Na niendelee kuyataka mashirika mengine kutii agizo hili ambalo tutalisimamia kikamilifu.
Hatutasita kuchukua hatua ikiwemo kuyafutia usajili mashirika yanayoendelea na miradi ya kusambaza vilainishi kwa wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Tupambane na UKIMWI kwa kujikita kwenye afua nyingine zinazozingatia sheria za nchi sambamba na mila na desturi zetu watanzania.