Ufafanuzi wa Meja, Padri, Dr Henry Rimisho

Inside10

JF-Expert Member
May 20, 2011
26,060
23,941
Padri alivyopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba, Kenya

Jambo kubwa lililopamba mahafali ya 15 ya Chuo Kikuu Ardhi (ARU) yaliyofanyika juzi, ni uwepo wa mhitimu wa Shahada ya Uzamivu, ambaye ni padri aliyepitia pia mafunzo ya kijeshi.

Padri huyo, Dk Henry Rimisho wa Shirika la Mitume wa Yesu la Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, amevuta hisia za Watanzania wengi baada ya picha yake kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuibua maswali mbalimbali, hasa baada ya kutajwa mitandaoni kwa namna mbalimbali, ikiwemo kwamba ni komandoo, jambo ambalo amekanusha.

Akionekana mwenye bashasha, Padri Rimisho alifanya mahojiano maalumu na Mwananchi jana juu ya maisha yake hadi kuwa mtumishi wa kiroho, mwenye mafunzo ya kijeshi na wakati huohuo akiwa msanifu wa majengo.

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuingia nyumbani kwa Paroko wa parokia ya Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambako aliandaliwa hafla ya kupongezwa kwa mafanikio hayo jana, Padri Rimisho alisema mafanikio yote aliyoyapata yametokana na mapenzi ya Mungu.

Mbele ya wanafunzi kadhaa ambao ni waumini wa Kanisa Katoliki parokiani hapo, Padri Rimisho alisimulia pia safari yake ya maisha ya kijeshi na kiusalama tangu akiwa mtoto wa miaka sita.

Aenda mafunzoni Cuba
Anasema alichukuliwa na kupelekwa nchini Cuba kwa mafunzo ya kiusalama akiwa bado mdogo.
“Mimi sikuwa najua lolote ila wazazi wangu nakumbuka waliwaambia watu walionifuata, kuwa wanichukue ikiwa wanaona ninawafaa. Nilikaa nchini Cuba kwa mwaka mmoja ambako nilikutana na mambo mazito sana,” anasema.

Anasema ni utamaduni wa shirika lao kutoa mafunzo ya kijeshi kwa mapadri wake na kwamba, hivi sasa wako 12 ambao wamekuwa wakipelekwa kwenye maeneo mbalimbali yenye machafuko.

“Hata mkuu wangu wa shirika anaitwa Benjamin aliyeko nchini Kenya, ana cheo cha Jenerali,” anasema.

Akizungumzia madai kwamba ni yeye komandoo, padri huyo anabainisha kuwa yeye hakufikia ngazi hiyo, bali katika mafunzo ya kijeshi aliishia ngazi ya kapteni na kufafanua kuwa kama angeendelea kidogo, angefikia ngazi ya ukomandoo.

Anafafanua kuwa ili mtu afuzu na kuitwa komando anapaswa kupitia maumivu fulani ikiwa ni pamoja na kukaa msituni kwa miezi miwili, ingawa alisema wapo wengine wanaohitimu vyuoni.

Alivyoenda Dafur
Padri, Rimisho anasema katika utumishi wake aliwahi kutumwa nchini Sudan kwa ajili ya operesheni ya Umoja wa Mataifa ya kusitisha mapigano.

Alipoulizwa kuhusu mgongano wa kimajukumu na kiimani katika kushiriki vita na huduma yake kama kiongozi kiroho, padri huyo anasema akiwa Darfur, nchini Sudan hakuwa na jukumu la kushiriki mapigano katika mstari wa mbele.
“Jukumu langu kama ilivyo kwa viongozi wengine wa kiroho, wakiwemo masheikh wanaokuwepo katika mazingira kama hayo, ilikuwa kuwafundisha wananchi jinsi ya kujilinda na kutoa huduma za mazishi,” anasema.

Baadaye anasema alipelekewa nchini Uganda ambako alifanya kazi katika seminari ndogo inayomilikiwa na shirika lake, kama baibu gombera wa seminari hiyo

Padre huyo mwenye mikanda ya rangi nyeusi katika michezo ya judo, karate na kungfuu, anaongeza, “ujuzi tulionao wa kushika silaha mbalimbali za moto unatusaidia katika kujilinda na kutoa mafunzo kwa wananchi lakini si kwa ajili ya mapambano mstari wa mbele.”

Usanifu majengo
Mwaka 2007 alijiunga na ARU kwa masomo ya Shahada ya Kwanza ya Usanifu wa majengo na baadaye akabakishwa shuleni hapo kama msaidizi wa mafunzo na mwanafunzi wa shahada ya uzamili.

Anasema baada ya kuhitimu shahada ya uzamili aliendelea na masomo ya miaka mitano ya shahada ya uzamivu (PhD) aliyohitimu Jumamosi iliyopita.

“Kama padri na mhitimu wa PhD katika fani ya usanifu majengo, wenzangu wameniambia hata baada ya kutafuta mtandaoni kuwa mimi ninakuwa wa kwanza barani Afrika na Ulaya,” anasema.

Anasema katika kutekeleza majukumu yake kama mhadhiri wa ARU, padri na vilevile kama msanifu wa majengo katika fani ambayo amesomea anahitaji muda wa kutosha na huitaji kuupangilia vizuri,” anasema.

Ili kumudu kutekeleza majukumu hayo kwa wakati mmoja, anasema amepanga ratiba yake kuhudumia wagonjwa, watawa na wananchi wengine na kuhakikisha anakuwa darasani kwa wakati muafaka bila kuathiri ratiba ya ufundishaji.

Kabla ya mafunzo ARU, pia alisoma falsafa na theolojia kwa muda wa miaka mitatu ili kukidhi matakwa ya shirika ya kustahili daraja la upadri na baadaye kuendelea na masomo ya miaka miwili katika Chuo cha Yesu jijini Nairobi nchini Kenya.

Anasema licha ya kusoma masomo ya sanaa (HGE) kidato cha sita aliomba maofisa wa ARU kutompima kwa tahasusi aliyochukua, bali uwezo wake na hivyo akafanikiwa kuanza masomo mwaka 2007 kupitia tahasusi ya EGM.

Padri Rimisho anasema anafarijika sana kuwatumikia watu wa mataifa mbalimbali katika nafasi zake kama kiongozi wa kiroho, mhadhiri na msanifu wa majengo.

Akizungumzia jinsi gani alivutwa na fani hizo mbili, Dk Rimisho anasema msingi wa hatima ya wanafunzi wa shule za sekondari za seminari ni wosia (will) ambao unaandikwa na mwanafunzi mwenyewe.

“Katika wosia nilisema nataka kuwa padri na msanifu nwa majengo. Lakini nilipofika Sudan na kushuhudia majengo yalivyokuwa yanaporomoka, niliona sijakosea kuchagua fani hii kwa kuwa lengo la kusaidia wananchi litatimia,” alisema.

Machapisho kibao
Katika picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Dk Rimisho anaonekana amepiga picha na idadi kubwa ya vitabu, alipoulizwa maana ya picha hizo alisema.

“Vitabu hivi 45 vinaonyesha jinsi gani nilikuwa karibu na wasimamizi wa shahada yangu ya uzamivu ambao ni Profesa Livin Mosha na Profesa Wilbard Kombe ambao katika ngazi ya PhD wanakuwa wanakupa maelekezo na mwongozo,” anasema na kuongeza.

“Kwa upande wangu nilikuwa naandika sana, lakini ukienda kwa msimamizi anakwambia hapana umekosea rudia tena. Vitabu hivi ni ushuhuda kuwa nilikuwa nafanya halafu narudishiwa hadi nilipofanikiwa baada ya kuandika kilichokubaliwa.”

Anasema alijitahidi kupambana hasa baada ya kukumbuka kuwa alishawatangazia ndugu, jamaa na marafiki kuwa ameanza masomo ya shahada ya uzamivu.

Anasimulia pia kuwa katika kipindi hicho akishirikiana na mwanafunzi mmoja aliyemchagua walishiriki katika mashindano ya kupendekeza usanifu wa nyumba za gharama nafuu, miongoni mwa vyuo vya usanifu wa majengo duniani.

“Kati ya nchi 150 zilizoshiriki mashindano hayo, mimi na mwanafunzi mwenzangu tulishika nafasi ya nne duniani na nafasi ya pili barani Afrika,” anasema.

Dk Rimisho alizaliwa Januari 29, 1969 katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam akiwa ni mtoto wa pili kati ya watoto sita wa Jacob Henry Rimisho na mama yake Filomena Jacob Rimisho ambao sasa ni marehemu.

Padri huyo anayehusudu michezo kama karate, kungfuu, judo, kuogelea na kunyanyua vitu vizito amewataka Watanzania kutokata tamaa na kujaribu kufanya kila wanachoamini ni ndoto zao.

Source:Padri alivyopata mafunzo ya kijeshi nchini Cuba, Kenya | Mwananchi
 
Mimi ndo maana mambo ya kwenda kuungama dhambi kwa hawa mapadri nilishakataaga huo upuuzi. Hawa wengi ni wazee wa kitengo. Ukijifanya kuwaamini na kuwabwatukia madhambi yako umekwisha .
Kwamba umefanya matukio ambayo Serikali ikikusikia ukikiri utaenda Jela Mkuu?
 
Kwamba umefanya matukio ambayo Serikali ikikusikia ukikiri utaenda Jela Mkuu?
Siyo hayo ya kuvunja sheria za nchi tu, hata mambo ya anasa yanamtachi maana na yeye ni binadamu!

Hapo unaungama sasa..."nimezini mara6"..."nimetamani mwanamke asiye mke wangu mara kumi"...

Halafu unayemuungamia ana usongo na mambo hayo na yanampa shida kuyapata, yaani wewe ni bingwa kuliko yeye.

Akikuangalia hauna haiba ya kutekeleza dhambi zote hizo anavyokupima yeye, anakuonea gere umewezaje kufanya mara kibao namna hiyo wee lofa!

Anaghadhabika, anakupiga adhabu ya kitubio kusali baba yetu mara 20 na salamu Maria mara 30 kukukomoa!

Utasali hadi unasahau ngapi umesali na ngapi umebakiza!

Maungamo matakatifu ni yale ya kumuungamia M/Mungu mwenyewe, kujuta dhambi na kuacha kufanya maovu hayo tena, lakini si kwa mwanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo hayo ya kuvunja sheria za nchi tu, hata mambo ya anasa yanamtachi maana na yeye ni binadamu!

Hapo unaungama sasa..."nimezini mara6"..."nimetamani mwanamke asiye mke wangu mara kumi"...

Halafu unayemuungamia ana usongo na mambo hayo na yanampa shida kuyapata, yaani wewe ni bingwa kuliko yeye.

Akikuangalia hauna haiba ya kutekeleza dhambi zote hizo anavyokupima yeye, anakuonea gere umewezaje kufanya mara kibao namna hiyo wee lofa!

Anaghadhabika, anakupiga adhabu ya kitubio kusali baba yetu mara 20 na salamu Maria mara 30 kukukomoa!

Utasali hadi unasahau ngapi umesali na ngapi umebakiza!

Maungamo matakatifu ni yale ya kumuungamia M/Mungu mwenyewe, kujuta dhambi na kuacha kufanya maovu hayo tena, lakini si kwa mwanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maungamo ya kweli kwa mujibu wa maagizo ya nani?, Huna haja ya kupata taabu angalia tu, YESU KRISTO aliagiza nini? na Mitume wa YESU KRISTO waliagiza nini?, NJE YA HAPO NI KUPOTEZA MUDA( Kwasababu, utakuwa unajibu SWALI ulilotunga wewe mwenyewe halafu unategemea MUNGU akupe maksi. Ni kichekesho).
 
Back
Top Bottom