History E. Literature D. Math F. Civics D. Biology D. Kiswahili B. English C. Geography C. Chemistry D Samahanini jamani je kwa matokeo yangu haya naweza nikasoma combination yenye history????? Plzzzzz
ndiyo unaweza kusoma kombi zenye somo la History ila katika shule za binafsi.
HGK inakuhusu
Kitu ambacho sijaelewa hapa inakuwaje E na F zote zina hadhi sawa yaani Fail. Kama E ina hadhi sawa na F, kulikuwa na sababu gani ya kuianzisha mpaka imesababisha mkanganyiko wa madaraja watu wanaopata pointi sawa kuanzia 41-45. Hii inachanganya watu bila sababu ya msingi. Yaani NECTA wameifa tu kuwa nchi nyingine zina makundi mengi bila kutueleza ndani ya hayo makundi kuna nini. Tusifanye kazi kwa mazoea na kuiga tuangalie inaongeza thamani gani katika elimu ya taifa letu
Inasemekana wamebadilisha mawazo wakafanya tofauti na ilivyopangwa awali:
"Kwa mfumo huu, alama ya ufaulu ilikuwa iwe E na CA zilitakiwa kuchangia asilimia 40. Hata hivyo mfumo huo haukutumika kama ilivyotangazwa na badala yake alama ya ufaulu imekuwa D na CA zimechangia 30, jambo ambalo bado halijawafurahisha wadau."
(SOURCE: Mwananachi)