Clemence Baraka
JF-Expert Member
- Sep 4, 2012
- 1,694
- 649
Leo hii asubuhi katika pita pita zangu za huku na kule, nilicho shuhudia ni kwamba watu wengi wanaamini Zitto ni msariti na wengi waowamekua wakimkandia kwa zile tuhuma ambazo CDM imekua ikizitoa dhidi ya Zitto.
CDM kama taasisi ikae ikijua kama tuhuma walizo elekeza kwa Zitto ni za kubuni na ni uzushi ikae ijkujua itafikia tamati, maana uongo auna uhai wa mda mrefu kama ukweli. Na hapo hawa wanao mkandia Zitto ndio watakua adui zao wakubwa na matokeo yake chama kitakufa.
Na kama tuhuma ni za kweli basi Zitto inampasa kukili madhaifu na ajisafishe, maana hakuna binadamu mkamilifu. Nae endapo hato fanya hivyo atakua na hali mbaya kisisiasa.
Zitto, wananchi wenye imani na wewe bado tupo wengi kutokana na utendaji wako, chukua fursa hii kuweka mambo sawa.
:dance:Kwani kuna shida gani? Hata ccm wamewahi mara chungu mzima kuondoa wanachama uoongozini tena wa ngazi ya juu na chama kikaendelea na kinaendelea. Haiwezekani watu wasio waaminifu na wasaliti waendelee kubaki kwenye uongozi na pengine hata chamani. Hata hivyo maudhui yaliyo kwenye waraka uliomfukuza Zitto na wenzake una hoja nzito na kama ni kweli ni lazima upande mwingine wa shilling uangaliwe. Hayo mapunguvu yaliyoko katika uongozi wa juu wa chama ni sharti yarekebishwe haraka. Kwa kuwa Chadema ni chama kikubwa na chenye wanachama wengi nchi nzima na ambacho ni tegemeo kubwa kwa wananchi wote bila itikadi, inabidi sasa mkutano mkuu uitwe haraka ili kasoro hizo zirekebishwe na chama kisonge mbele. Ni upuuzi wanachama kusema watakiacha chama chao kutokana na maamuzi ya kumwondolea Zitto madaraka. Kwa upande mwingine pande zote mbili ni za kulaumu. Upande wa Uongozi wa juu wa chadema, na Upande wa zitto. Ni uvumilivu tu umekosekana. Ni miaka miwili tu imebaki ambapo hicho chama wanachosema wao kimeletwa na Mungu ama kingeshika dola au kula sahani maja na ccm kwa maana kuwa na idadi ya wabunge wa kukaribiana sana. Hilo litawezekana tu kama kasoro zilizoelezwa kwenye waraka zitarekebishwa kwa spidi ya haraka ili chama kiongozwe kidemokrasia zaidi.